1第五位天使吹号,我就看见一颗星从天上落到地上,有无底坑的钥匙赐给它。
1Kisha malaika wa tano akapiga tarumbeta yake. Nami nikaona nyota iliyokuwa imeanguka juu ya nchi kutoka mbinguni. Nayo ikapewa ufunguo wa shimo la Kuzimu.
2它开了无底坑,就有烟从坑里冒出来,好像大火炉的烟,太阳和天空因这坑的烟就都变黑了。
2Basi, nyota hiyo ikafungua shimo la Kuzimu, kukatoka moshi wa tanuru kubwa. Jua na anga vikatiwa giza kwa moshi huo wa Kuzimu.
3有蝗虫从烟里出来到了地上;有能力赐给它们,好像地上蝎子的能力一样。
3Nzige wakatoka katika moshi huo, wakaingia duniani wakapewa nguvu kama ya ng'e.
4有话吩咐它们,不可伤害地上的草,和所有青翠的东西,以及所有的树木,只可伤害那些额上没有 神印记的人。
4Wakaamrishwa wasiharibu nyasi za nchi wala majani wala miti yoyote, bali wawaharibu wale tu ambao hawakupigwa mhuri wa Mungu katika paji la uso.
5蝗虫没有能力杀死他们,只可使他们受痛苦五个月。他们的痛苦就像人给蝎子螫了的痛苦一样。
5Nzige hao hawakuruhusiwa kuwaua watu, ila kuwatesa tu kwa muda wa miezi mitano. Maumivu watakayosababisha ni kama maumivu yanayompata mtu wakati anapoumwa na ng'e.
6在那些日子,人要求死,却决不得死;切愿要死,死却远离他们。
6Muda huo watu watatafuta kifo lakini hawatakipata; watatamani kufa lakini kifo kitawakimbia.
7蝗虫的形象,好像是预备好了要上阵的战马一样。它们头上戴的好像金冠冕,脸像人的面孔,
7Kwa kuonekana, nzige hao walikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita. Juu ya vichwa vyao walikuwa na taji zilizo kama za dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu.
8它们的头发好像女人的头发,牙齿好像狮子的牙齿;
8Nywele zao zilikuwa kama nywele za wanawake, na meno yao yalikuwa kama meno ya simba.
9它们的胸甲像铁甲,它们翅膀的声音好像许多马车奔驰上阵的声音。
9Vifua vyao vilikuwa vimefunikwa kitu kama ngao ya chuma. Sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya msafara wa magari ya farasi wengi wanaokimbilia vitani.
10它们好像蝎子一样有尾巴和毒刺,它们的尾巴能伤害人五个月。
10Walikuwa na mikia na miiba kama ng'e, na kwa mikia hiyo, walikuwa na nguvu ya kuwadhuru watu kwa muda wa miezi mitano.
11它们有无底坑的使者作王统治它们。这王的名字,希伯来话叫阿巴顿,希腊话叫阿波伦。
11Tena wanaye mfalme anayewatawala, naye ndiye malaika wa kuzimu; jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kigiriki ni Apolioni, yaani mwangamizi.
12第一样灾祸过去了。看哪,以后还有两样灾祸要来!
12Maafa ya kwanza yamepita; bado mengine mawili yanafuata.
13第六位天使吹号,我听见有一个声音从 神面前金坛的四角发出来,
13Kisha malaika wa sita akapiga tarumbeta yake. Nami nikasikia sauti moja kutoka katika pembe nne za madhabahu ya dhahabu iliyokuwa mbele ya Mungu.
14对拿着号筒的第六位天使说:“把捆绑在幼发拉底大河的那四个使者放了吧!”
14Sauti hiyo ikamwambia huyo malaika wa sita mwenye tarumbeta, "Wafungulie malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Eufrate!"
15那四个使者就被释放了,他们已经预备好,要在某年某月某日某时杀害人类的三分之一。
15Naye akawafungulia malaika hao wanne ambao walikuwa wametayarishwa kwa ajili ya saa hiyo ya siku ya mwezi huo, wa mwaka huohuo, kuua theluthi moja ya wanaadamu.
16马兵的数目有二万万;他们这个数目我听见了。
16Nilisikia idadi ya majeshi wapanda farasi ilikuwa milioni mia mbili.
17在异象中,我看见那些马和骑马的是这样:骑马的穿着火红紫青和硫磺色的胸甲,马的头好像狮子头,有火、烟和硫磺从马的口中喷出来。
17Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika hiyo njozi: Walikuwa na ngao vifuani zilizokuwa moto mtupu, zenye rangi ya samawati na njano kama kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vya simba; na moto, moshi, na kiberiti vilikuwa vinatoka kinywani mwao.
18马口中喷出来的火、烟和硫磺这三种灾害,杀死了人类的三分之一。
18Theluthi moja ya wanaadamu waliuawa kwa mabaa hayo matatu yaani, moto, moshi na kiberiti, yaliyokuwa yanatoka katika vinywa vyao;
19马的能力是在口中和尾巴上。它们的尾巴像蛇,并且有头用来伤人。
19maana nguvu ya farasi hao ilikuwa vinywani mwao na katika mikia yao. Mikia yao ilikuwa na vichwa kama nyoka, na waliitumia hiyo kuwadhuru watu.
20其余没有在这些灾难中被杀的人,仍然不为他们手所作的悔改,还是去拜鬼魔和那些金、银、铜、石头、木头做的,不能看、不能听、也不能走路的偶像。
20Wanaadamu wengine waliobaki ambao hawakuuawa na mabaa hayo, hawakugeuka na kuviacha vitu walivyokuwa wametengeneza kwa mikono yao wenyewe; bali wakaendelea kuabudu pepo, sanamu za dhahabu, fedha, shaba, mawe na miti, vitu ambavyo haviwezi kuona, kusikia wala kutembea.
21他们也不为自己的凶杀、邪术、淫乱和偷盗悔改。
21Wala hawakutubu na kuacha kufanya mauaji, uchawi, uzinzi, na wizi.