1不求自己的喜悦
1Sisi tulio imara katika imani tunapaswa kuwasaidia wale walio dhaifu wayakabili matatizo yao. Tusijipendelee sisi wenyewe tu.
2我们各人务要叫邻舍喜悦,好让他得到益处、得到造就。
2Kila mmoja wetu anapaswa kumpendeza jirani yake kwa wema ili huyo apate kujijenga katika imani.
3因为连基督也不求自己的喜悦;反而像经上所记的:“辱骂你的人的辱骂,都落在我的身上。”
3Maana Kristo hakujipendelea mwenyewe; ila alikuwa kama yasemavyo Maandiko: "Kashfa zote walizokutolea wewe zimenipata mimi."
4从前经上所写的,都是为教训我们而写的,好使我们借着忍耐和圣经中的安慰得着盼望。
4Maana yote yalioandikwa yameandikwa kwa ajili ya kutufundisha sisi ili kutokana na saburi na faraja tupewayo na Maandiko hayo Matakatifu tupate kuwa na matumaini.
5愿赐忍耐和安慰的 神,使你们彼此同心,效法基督耶稣,
5Mungu aliye msingi wa saburi na faraja yote, awajalieni ninyi kuwa na msimamo mmoja kufuatana na mfano wake Kristo Yesu,
6同心一致地荣耀我们主耶稣基督的父 神。
6ili ninyi nyote, kwa nia moja na sauti moja, mumtukuze Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
7外族人蒙恩颂赞 神因此,你们应当彼此接纳,就像基督接纳了你们一样,使荣耀归于 神。
7Basi, karibishaneni kwa ajili ya utukufu wa Mungu kama naye Kristo alivyowakaribisheni.
8我说,基督为了 神的真理,成了受割礼的人的仆人,为的是要证实对祖先的应许,
8Maana, nawaambieni Kristo aliwatumikia Wayahudi apate kuonyesha uaminifu wa Mungu, na zile ahadi Mungu alizowapa babu zetu zipate kutimia;
9使外族人因着所蒙的怜悯荣耀 神;如经上所记:“因此我要在列邦中称赞你,歌颂你的名。”
9ili nao watu wa mataifa mengine wapate kumtukuza Mungu kwa sababu ya huruma yake. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Kwa sababu hiyo, nitakusifu miongoni mwa watu wa mataifa. Nitaziimba sifa za jina lako."
10又说:“列邦啊,当与他的子民一同快乐。”
10Tena Maandiko yasema: "Furahini, enyi watu wa mataifa; furahini pamoja na watu wake."
11又说:“万国啊,你们当赞美主;愿万民都颂赞他。”
11Na tena: "Enyi mataifa yote, msifuni Bwana; enyi watu wote, msifuni."
12以赛亚也说:“将来必有耶西的根,就是那兴起来治理列邦的;列邦都寄望于他。”
12Tena Isaya asema: "Atatokea mtu katika ukoo wa Yese, naye atawatawala watu wa mataifa; nao watamtumainia."
13愿那赐盼望的 神,因着你们的信,把一切喜乐平安充满你们,使你们靠着圣灵的大能满有盼望。
13Basi, Mungu aliye msingi wa matumaini, awajazeni furaha yote na amani kutokana na imani yenu; tumaini lenu lipate kuongezeka kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.
14不在传过基督的地方传福音我的弟兄们,我个人深信你们自己也满有良善,充满丰富的知识,也能够彼此劝导。
14Ndugu zangu, mimi binafsi nina hakika kwamba ninyi pia mmejaa wema, elimu yote, na mnaweza kushauriana ninyi kwa ninyi.
15但有些地方,我写得稍为大胆一点,是要提醒你们;我因着 神赐给我的恩典,
15Lakini nimewaandikia hapa na pale katika barua hii bila woga, nipate kuwakumbusheni juu ya mambo fulani. Nimefanya hivyo kwa sababu ya neema aliyonijalia Mungu
16为外族人作了基督耶稣的仆役,作了 神福音的祭司,使所献上的外族人得蒙悦纳,靠着圣灵成为圣洁。
16ya kuwa mtumishi wa Yesu Kristo kwa watu wa mataifa. Ni jukumu langu la kikuhani kuihubiri Habari Njema ya Mungu ili watu wa mataifa mengine wapate kuwa dhabihu inayokubaliwa na Mungu, dhabihu iliyotakaswa na Roho Mtakatifu.
17所以,在 神的事上,我在基督耶稣里倒有可以引以为荣的。
17Kwa hiyo, nikiwa nimeungana na Kristo Yesu, naweza kujivunia huduma yangu kwa ajili ya Mungu.
18别的我不敢说,我只说基督借着我所作的事,就是用言语行为,借着神迹和奇事的大能,以及圣灵的大能,使外族人顺服;这样,我从耶路撒冷直到以利里古,把基督的福音都传开了。
18Sithubutu kusema kitu kingine chochote isipokuwa tu kile ambacho Kristo Yesu amekifanya kwa kunitumia mimi ili watu wa mataifa wapate kutii. Amefanya hivyo kwa maneno na vitendo,
19
19kwa nguvu ya miujiza na maajabu, na kwa nguvu ya Roho wa Mungu. Basi, kwa kusafiri kila mahali, tangu kule Yerusalemu mpaka Iluriko, nimeihubiri kikamilifu Habari Njema ya Kristo.
20我立定主意,不在宣扬过基督的地方传福音,免得建立在别人的根基上,
20Nia yangu imekuwa daima kuihubiri Habari Njema popote pale ambapo jina la Kristo halijapata kusikika, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine.
21反而照经上所记:“那对他一无所闻的,将要看见;那没有听过的,将要明白。”
21Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Watu wote ambao hawakuambiwa habari zote wataona; nao wale ambao hawajapata kusikia, wataelewa."
22保罗计划到罗马去因此,我多次受到拦阻,不能到你们那里去。
22Kwa sababu hiyo nilizuiwa mara nyingi kuja kwenu.
23但现在这一带再没有可传的地方,而我多年来又很想去见你们,
23Lakini maadam sasa nimemaliza kazi yangu pande hizi, na kwa kuwa kwa miaka mingi nimekuwa na nia kubwa ya kuja kwenu,
24所以,无论我什么时候到西班牙去,都希望趁我路过时和你们见面,先稍微满足我的心愿,然后由你们给我送行到那里去。
24natumaini kufanya hivyo sasa. Ningependa kuwaoneni nikiwa safarini kwenda Spania na kupata msaada wenu kwa safari hiyo baada ya kufurahia kuwa kwa muda pamoja nanyi.
25不过,我现在为了供应圣徒的事要往耶路撒冷去;
25Lakini, kwa sasa nakwenda kuwahudumia watu wa Mungu kule Yerusalem.
26因为马其顿和亚该亚人乐意捐了一些钱,给耶路撒冷圣徒中的穷人。
26Maana makanisa ya Makedonia na Akaya yemeamua kutoka mchango wao kuwasaidia watu wa Mungu walio maskini huko Yerusalem.
27他们是乐意的,而且那也是他们的本分(“本分”原文作“债”),因为外族人既然分享了犹太人属灵的好处,就应该供应他们肉身的需要。
27Wao wenyewe wameamua kufanya hivyo; lakini, kwa kweli, hilo ni jukumu lao kwa hao. Maana, ikiwa watu wa mataifa mengine wameshiriki baraka za kiroho za Wayahudi, wanapaswa nao pia kuwahudumia Wayahudi katika mahitaji yao ya kidunia.
28等我办好这件事,把这笔款项安全地交了给他们,我就要路过你们那里到西班牙去。
28Nitakapokwisha tekeleza kazi hiyo na kuwakabidhi mchango huo uliokusanywa kwa ajili yao, nitawatembeleeni ninyi nikiwa safarini kwenda Spania.
29我知道我到你们那里去的时候,一定会带着基督丰盛的福分。
29Najua ya kuwa nikija kwenu nitawaletea wingi wa baraka za Kristo.
30弟兄们,我靠着我们的主耶稣基督,凭着圣灵的慈爱,劝你们和我一同竭力为我向 神祈祷,
30Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa ajili ya upendo uletwao na Roho, mniunge mkono kwa kuniombea kwa Mungu.
31求 神救我脱离犹太地不信从的人,使我带到耶路撒冷的捐款,可以得到圣徒的悦纳;
31Ombeni nipate kutoka salama miongoni mwa wale wasioamini walioko Uyahudi, nayo huduma yangu huko Yerusalem ipate kukubaliwa na watu wa Mungu walioko huko.
32也使我照着 神的旨意,高高兴兴地到你们那里去,好和你们一同得到安息。
32Hivyo, Mungu akipenda, nitaweza kuja kwenu na moyo wa furaha, nikapumzike pamoja nanyi.
33愿赐平安的 神与你们众人同在。阿们。
33Mungu aliye chanzo cha amani na awe nanyi nyote! Amina!