1Be my imitators, even as *I* also [am] of Christ.
1Niigeni mimi kama ninavyomwiga Kristo.
2Now I praise you, that in all things ye are mindful of me; and that as I have directed you, ye keep the directions.
2Nawapeni hongera kwa sababu mnanikumbuka na kwa sababu mnayashikilia yale maagizo niliyowapeni.
3But I wish you to know that the Christ is the head of every man, but woman's head [is] the man, and the Christ's head God.
3Lakini napenda pia mjue kwamba Kristo ni kichwa cha kila mwanamume, na mwanamume ni kichwa cha mkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo.
4Every man praying or prophesying, having [anything] on his head, puts his head to shame.
4Basi, kila mwanamume anayesali au anayetangaza ujumbe wa Mungu huku amefunika kichwa chake, huyo anamdharau Kristo.
5But every woman praying or prophesying with her head uncovered puts her own head to shame; for it is one and the same as a shaved [woman].
5Na mwanamke akisali au kutangaza ujumbe wa Mungu bila kufunika kichwa chake, anamdharau mumewe; anayefanya hivyo ni sawa tu na mwanamke aliyenyoa kichwa chake.
6For if a woman be not covered, let her hair also be cut off. But if [it be] shameful to a woman to have her hair cut off or to be shaved, let her be covered.
6Mwanamke asiyefunika kichwa chake, afadhali anyoe nywele zake. Lakini ni aibu kwa mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa; basi, afadhali afunike kichwa chake.
7For man indeed ought not to have his head covered, being God's image and glory; but woman is man's glory.
7Haifai mwanamume kufunika kichwa chake, kwa kuwa yeye ni mfano wa Mungu na kioo cha utukufu wake Mungu; lakini mwanamke ni kioo cha utukufu wa mwanamume.
8For man is not of woman, but woman of man.
8Mwanamume hakutoka kwa mwanamke, ila mwanamke alitoka kwa mwanamume.
9For also man was not created for the sake of the woman, but woman for the sake of the man.
9Mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, ila mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanamume.
10Therefore ought the woman to have authority on her head, on account of the angels.
10Ndiyo maana mwanamke hufunika kichwa chake, iwe ishara ya mamlaka yaliyo juu yake, na pia kwa sababu ya malaika.
11However, neither [is] woman without man, nor man without woman, in [the] Lord.
11Hata hivyo, mbele ya Bwana mwanamke si kitu bila mwanamume, naye mwanamume si kitu bila mwanamke.
12For as the woman [is] of the man, so also [is] the man by the woman, but all things of God.
12Kama vile mwanamke alivyotokana na mwanamume, vivyo hivyo mwanamume huzaliwa na mwanamke; kila kitu hutoka kwa Mungu.
13Judge in yourselves: is it comely that a woman should pray to God uncovered?
13Amueni wenyewe: Je, inafaa mwanamke kumwomba Mungu bila kuvaa kitu kichwani?
14Does not even nature itself teach you, that man, if he have long hair, it is a dishonour to him?
14Hata maumbile yenyewe huonyesha wazi kwamba kwa mwanamume kuwa na nywele ndefu ni aibu kwake mwenyewe;
15But woman, if she have long hair, [it is] glory to her; for the long hair is given [to her] in lieu of a veil.
15lakini kwa mwanamke kuwa na nywele ni heshima kwake; nywele zake ndefu amepewa ili zimfunike.
16But if any one think to be contentious, *we* have no such custom, nor the assemblies of God.
16Kama mtu anataka kuleta ubishi juu ya jambo hili, basi, na ajue kwamba sisi hatuna desturi nyingine, wala makanisa ya Mungu hayana desturi nyingine.
17But [in] prescribing [to you on] this [which I now enter on], I do not praise, [namely,] that ye come together, not for the better, but for the worse.
17Nikiwa bado nawapeni maagizo haya, siwezi hata kidogo kuwapa ninyi hongera kuhusu haya yafuatayo: mikutano yenu ninyi waumini yaleta hasara zaidi kuliko faida.
18For first, when ye come together in assembly, I hear there exist divisions among you, and I partly give credit [to it].
18Awali ya yote, nasikia kwamba mnapokutana pamoja hutokea mafarakano kati yenu. Nami naamini kiasi,
19For there must also be sects among you, that the approved may become manifest among you.
19maana ni lazima fikira tofauti ziweko miongoni mwenu, ili wale walio thabiti wapate kutambulikana.
20When ye come therefore together into one place, it is not to eat [the] Lord's supper.
20Kweli mnakutana, lakini si kwa ajili ya kula chakula cha Bwana!
21For each one in eating takes his *own* supper before [others], and one is hungry and another drinks to excess.
21Maana mnapokula kila mmoja hukikalia chakula chake mwenyewe, hata hutokea kwamba baadhi yenu wana njaa, na wengine wamelewa!
22Have ye not then houses for eating and drinking? or do ye despise the assembly of God, and put to shame them who have not? What shall I say to you? shall I praise you? In this [point] I do not praise.
22Je, hamwezi kula na kunywa nyumbani kwenu! Au je, mnalidharau kanisa la Mungu na kuwaaibisha hao wasio na kitu? Niwaambie nini? Niwasifu? La hasha! Si kuhusu jambo hili.
23For *I* received from the Lord, that which I also delivered to you, that the Lord Jesus, in the night in which he was delivered up, took bread,
23Maana mimi nilipokea kwa Bwana yale maagizo niliyowaachieni: kwamba, usiku ule Bwana Yesu aliotolewa, alitwaa mkate,
24and having given thanks broke [it], and said, This is my body, which [is] for you: this do in remembrance of me.
24akamshukuru Mungu, akaumega, akasema: "Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka."
25In like manner also the cup, after having supped, saying, This cup is the new covenant in my blood: this do, as often as ye shall drink [it], in remembrance of me.
25Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe akasema: "Hiki ni kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu. Fanyeni hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka."
26For as often as ye shall eat this bread, and drink the cup, ye announce the death of the Lord, until he come.
26Maana kila mnapokula mkate huu na kunywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja.
27So that whosoever shall eat the bread, or drink the cup of the Lord, unworthily, shall be guilty in respect of the body and of the blood of the Lord.
27Kwa hiyo, kila aulaye mkate huo au kunywa kikombe cha Bwana bila kustahili, atakuwa na hatia dhidi ya mwili na damu ya Bwana.
28But let a man prove himself, and thus eat of the bread, and drink of the cup.
28Basi, kila mtu ajichunguze mwenyewe kwanza, ndipo ale mkate huo na anywe kikombe hicho;
29For [the] eater and drinker eats and drinks judgment to himself, not distinguishing the body.
29maana anayekula na kunywa bila kutambua maana ya mwili wa Bwana, anakula na kunywa hukumu yake yeye mwenyewe.
30On this account many among you [are] weak and infirm, and a good many are fallen asleep.
30Ndiyo maana wengi kati yenu ni dhaifu na wagonjwa, na wengine kadhaa wamekufa.
31But if we judged ourselves, so were we not judged.
31Kama tungejichunguza wenyewe vizuri hatungeadhibiwa hivyo.
32But being judged, we are disciplined of [the] Lord, that we may not be condemned with the world.
32Lakini tunapohukumiwa na Bwana, tunafunzwa tuwe na nidhamu, ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.
33So that, my brethren, when ye come together to eat, wait for one another.
33Kwa hiyo, ndugu zangu, mnapokutana kula chakula cha Bwana, kila mmoja amngoje mwenzake.
34If any one be hungry, let him eat at home, that ye may not come together for judgment. But the other things, whenever I come, I will set in order.
34Na kama kuna yeyote aliye na njaa, na ale nyumbani kwake, ili kukutana kwenu kusisababishe hukumu. Lakini, kuhusu yale mambo mengine, nitawapeni maelezo nitakapokuja.