1Masters, give to bondmen what is just and fair, knowing that *ye* also have a Master in [the] heavens.
1Nanyi wakuu, watendeeni watumwa wenu kwa uadilifu na haki, mkikumbuka kwamba nanyi pia mnaye Bwana mbinguni.
2Persevere in prayer, watching in it with thanksgiving;
2Dumuni katika sala, na mnaposali muwe waangalifu, mkimshukuru Mungu.
3praying at the same time for us also, that God may open to us a door of the word to speak the mystery of Christ, on account of which also I am bound,
3Vilevile, mtuombee sisi pia ili Mungu atupe fursa ya kuuhubiri ujumbe wake kuhusu siri ya Kristo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasa kifungoni.
4to the end that I may make it manifest as I ought to speak.
4Basi, ombeni ili niweze kusema kama inavyonipasa na kwa namna itakayodhihirisha siri hiyo.
5Walk in wisdom towards those without, redeeming opportunities.
5Muwe na hekima katika uhusiano wenu na watu wasioamini, mkitumia vizuri kila nafasi mliyo nayo.
6[Let] your word [be] always with grace, seasoned with salt, [so as] to know how ye ought to answer each one.
6Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daima mema na ya kuvutia, na mnapaswa kujua jinsi ya kumjibu vizuri kila mmoja.
7Tychicus, the beloved brother and faithful minister and fellow-bondman in [the] Lord, will make known to you all that concerns me;
7Ndugu yetu mpenzi Tukiko, mfanyakazi mwaminifu na mtumishi mwenzetu katika kazi ya Bwana, atawapeni habari zangu zote.
8whom I have sent to you for this very purpose, that he might know your state, and that he might encourage your hearts:
8Ndiyo maana namtuma, ili aichangamshe mioyo yenu kwa kuwaambieni habari zetu.
9with Onesimus, the faithful and beloved brother, who is [one] of you. They shall make known to you everything here.
9Anakuja pamoja na Onesimo, ndugu yetu mpenzi na mwaminifu, ambaye ni mwananchi mwenzenu. Watawapeni habari za mambo yote yanayofanyika hapa.
10Aristarchus my fellow-captive salutes you, and Mark, Barnabas's cousin, concerning whom ye have received orders, (if he come to you, receive him,)
10Aristarko, ambaye yuko kifungoni pamoja nami, anawasalimuni; hali kadhalika Marko, binamu yake Barnaba, (mmekwisha pata maagizo juu yake; akifika kwenu mkaribisheni).
11and Jesus called Justus, who are of the circumcision. These [are the] only fellow-workers for the kingdom of God who have been a consolation to me.
11Naye Yoshua aitwaye Yusto, anawasalimuni. Miongoni mwa Wayahudi waliokwisha pokea imani, hawa tu peke yao, ndio wanaofanya kazi pamoja nami kwa ajili ya Utawala wa Mungu; nao wamekuwa msaada mkubwa kwangu.
12Epaphras, who is [one] of you, [the] bondman of Christ Jesus, salutes you, always combating earnestly for you in prayers, to the end that ye may stand perfect and complete in all [the] will of God.
12Epafra, mwananchi mwenzenu na mtumishi wa Kristo Yesu anawasalimuni. Daima anawaombeeni ninyi kwa bidii ili mpate kusimama imara, mkomae na kuwa thabiti kabisa katika mambo yote anayotaka Mungu.
13For I bear him witness that he labours much for you, and them in Laodicea, and them in Hierapolis.
13Naweza kushuhudia kwamba anafanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu na kwa ajili ya watu wa Laodikea na Hierapoli.
14Luke, the beloved physician, salutes you, and Demas.
14Luka, daktari wetu mpenzi, na Dema, wanawasalimuni.
15Salute the brethren in Laodicea, and Nymphas, and the assembly which [is] in his house.
15Salamu zetu kwa ndugu zetu wa Laodikea; msalimuni dada Nimfa pamoja na jumuiya yote ya waumini inayokutana nyumbani kwake.
16And when the letter has been read among you, cause that it be read also in the assembly of Laodiceans, and that *ye* also read that from Laodicea.
16Mkisha soma barua hii, hakikisheni kwamba inasomwa na Wakristo wa Laodikea; na ninyi fanyeni mpango mpate kuisoma barua waliyoipata kwao.
17And say to Archippus, Take heed to the ministry which thou hast received in [the] Lord, to the end that thou fulfil it.
17Mwambieni Arkipo aitekeleze vizuri ile huduma aliyokabidhiwa na Bwana.
18The salutation by the hand of me Paul. Remember my bonds. Grace [be] with you.
18Naandika haya kwa mkono wangu mwenyewe: Salamu kutoka kwangu, mimi Paulo. Kumbukeni kwamba niko kifungoni. Neema ya Mungu iwe nanyi.