1James, bondman of God and of [the] Lord Jesus Christ, to the twelve tribes which [are] in the dispersion, greeting.
1Mimi Yakobo, mtumishi wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo, nawaandikia ninyi, makabila kumi na mawili, yaliyotawanyika ulimwenguni! Salaam!
2Count it all joy, my brethren, when ye fall into various temptations,
2Ndugu zangu, muwe na furaha mnapopatwa na majaribu mbalimbali,
3knowing that the proving of your faith works endurance.
3kwani mwajua kwamba imani yenu ikisha stahimili, itawapatieni uvumilivu.
4But let endurance have [its] perfect work, that ye may be perfect and complete, lacking in nothing.
4Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.
5But if any one of you lack wisdom, let him ask of God, who gives to all freely and reproaches not, and it shall be given to him:
5Lakini kama mmoja wenu ametindikiwa hekima, basi, anapaswa kumwomba Mungu ambaye atampatia; kwani Mungu huwapa wote kwa wingi na kwa ukarimu.
6but let him ask in faith, nothing doubting. For he that doubts is like a wave of the sea driven by the wind and tossed about;
6Lakini anapaswa kuomba kwa imani bila mashaka yoyote. Mtu aliye na mashaka ni kama mawimbi ya bahari ambayo husukumwa na kutupwatupwa na upepo.
7for let not that man think that he shall receive anything from the Lord;
7Mtu wa namna hiyo, mwenye nia mbili na asiye na msimamo katika mwenendo wake wote,
8[he is] a double-minded man, unstable in all his ways.
8asidhani ya kwamba atapata chochote kile kutoka kwa Bwana.
9But let the brother of low degree glory in his elevation,
9Ndugu aliye maskini anapaswa kufurahi wakati Mungu anapomkweza,
10and the rich in his humiliation, because as [the] grass's flower he will pass away.
10naye tajiri anapaswa kufurahi anaposhushwa na Mungu. Maana tajiri atatoweka kama ua la porini.
11For the sun has risen with its burning heat, and has withered the grass, and its flower has fallen, and the comeliness of its look has perished: thus the rich also shall wither in his goings.
11Jua huchomoza na kwa joto lake kali hukausha mimea, nayo maua yake huanguka, na uzuri wake wote huharibika. Vivyo hivyo, tajiri ataangamizwa katika shughuli zake.
12Blessed [is the] man who endures temptation; for, having been proved, he shall receive the crown of life, which He has promised to them that love him.
12Heri mtu anayebaki mwaminifu katika majaribu, kwani akisha stahimili atapewa tuzo la uzima ambalo Mungu aliwaahidia wale wanaompenda.
13Let no man, being tempted, say, I am tempted of God. For God cannot be tempted by evil things, and himself tempts no one.
13Kama mtu akijaribiwa, asiseme: "Ninajaribiwa na Mungu." Maana Mungu hawezi kujaribiwa na uovu, wala yeye hamjaribu mtu yeyote.
14But every one is tempted, drawn away, and enticed by his own lust;
14Lakini mtu hujaribiwa anapovutwa na kunaswa na tamaa zake mbaya.
15then lust, having conceived, gives birth to sin; but sin fully completed brings forth death.
15Tamaa ikiiva huzaa dhambi; nayo dhambi ikikomaa huzaa kifo.
16Do not err, my beloved brethren.
16Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike!
17Every good gift and every perfect gift comes down from above, from the Father of lights, with whom is no variation nor shadow of turning.
17Kila kipaji chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni; hutoka kwa Baba, Muumba wa mianga, ambaye habadiliki wala hana alama yoyote ya ugeugeu.
18According to his own will begat he us by the word of truth, that we should be a certain first-fruits of *his* creatures.
18Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa kwa neno lake la ukweli, ili tuwe namna ya matunda ya kwanza miongoni mwa viumbe vyake.
19So that, my beloved brethren, let every man be swift to hear, slow to speak, slow to wrath;
19Ndugu zangu wapenzi, kumbukeni jambo hili! Kila mtu na awe mwepesi wa kusikia lakini asiwe mwepesi wa kusema wala mwepesi wa kukasirika.
20for man's wrath does not work God's righteousness.
20Mwenye hasira hawezi kutimiza matakwa ya Mungu yaliyo ya haki.
21Wherefore, laying aside all filthiness and abounding of wickedness, accept with meekness the implanted word, which is able to save your souls.
21Kwa hiyo, tupilieni mbali mwenendo mchafu na tabia zote mbovu; jiwekeni chini ya Mungu na kupokea ule ujumbe uliopandwa mioyoni mwenu, ambao waweza kuziokoa nafsi zenu.
22But be ye doers of [the] word and not hearers only, beguiling yourselves.
22Msijidanganye wenyewe kwa kusikiliza tu neno lake, bali litekelezeni kwa vitendo.
23For if any man be a hearer of [the] word and not a doer, *he* is like to a man considering his natural face in a mirror:
23Yeyote anayesikiliza hilo neno lakini halitekelezi, huyo ni kama mtu anayejiangalia sura yake mwenyewe katika kioo.
24for he has considered himself and is gone away, and straightway he has forgotten what he was like.
24Hujiangalia mwenyewe, kisha huenda zake, na mara husahau jinsi alivyo.
25But *he* that fixes his view on [the] perfect law, that of liberty, and abides in [it], being not a forgetful hearer but a doer of [the] work, *he* shall be blessed in his doing.
25Lakini mtu anayeangalia kwa makini sheria kamilifu ambayo huwapa watu uhuru, mtu anayeendelea kuizingatia, na si kuisikia tu na kuisahau baadaye, bali anaitekeleza, mtu huyo atabarikiwa katika kila kitu anachofanya.
26If any one think himself to be religious, not bridling his tongue, but deceiving his heart, this man's religion is vain.
26Kama mtu akijiona kuwa ni mtu mwenye dini, lakini hawezi kuutawala ulimi wake, dini yake haifai kitu, na anajidanganya mwenyewe.
27Pure and undefiled religion before God and the Father is this: to visit orphans and widows in their affliction, to keep oneself unspotted from the world.
27Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.