1And the Pharisees and some of the scribes, coming from Jerusalem, are gathered together to him,
1Baadhi ya Mafarisayo na walimu wa Sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu walikusanyika mbele ya Yesu.
2and seeing some of his disciples eat bread with defiled, that is, unwashed, hands,
2Waliona kwamba baadhi ya wanafunzi wake walikula mikate kwa mikono najisi, yaani bila kunawa.
3(for the Pharisees and all the Jews, unless they wash their hands diligently, do not eat, holding what has been delivered by the ancients;
3Maana Mafarisayo na Wayahudi wengine wote huzingatia mapokeo ya wazee wao: hawali kitu kabla ya kunawa mikono ipasavyo.
4and [on coming] from the market-place, unless they are washed, they do not eat; and there are many other things which they have received to hold, the washing of cups and vessels, and brazen utensils, and couches),
4Tena hawali kitu chochote kutoka sokoni mpaka wamekiosha kwanza. Kuna pia desturi nyingine walizopokea kama vile namna ya kuosha vikombe, sufuria na vyombo vya shaba.
5then the Pharisees and the scribes ask him, Why do thy disciples not walk according to what has been delivered by the ancients, but eat the bread with defiled hands?
5Basi, Mafarisayo na walimu wa Sheria wakamwuliza Yesu, "Mbona wanafunzi wako hawayajali mapokeo tuliyopokea kwa wazee wetu, bali hula chakula kwa mikono najisi?"
6But he answering said to them, Well did Esaias prophesy concerning you hypocrites, as it is written, This people honour me with their lips, but their heart is far away from me.
6Yesu akawajibu, "Wanafiki ninyi! Nabii Isaya alitabiri ukweli juu yenu alipoandika: Watu hawa, asema Mungu, huniheshimu kwa maneno matupu, lakini mioyoni mwao wako mbali nami.
7But in vain do they worship me, teaching [as their] teachings commandments of men.
7Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu.
8[For], leaving the commandment of God, ye hold what is delivered by men [to keep] -- washings of vessels and cups, and many other such like things ye do.
8Ninyi mnaiacha amri ya Mungu na kushikilia maagizo ya watu."
9And he said to them, Well do ye set aside the commandment of God, that ye may observe what is delivered by yourselves [to keep].
9Yesu akaendelea kusema, "Ninyi mnajua kuepa kwa ujanja sheria ya Mungu kwa ajili ya kufuata mapokeo yenu.
10For Moses said, Honour thy father and thy mother; and, he who speaks ill of father or mother, let him surely die.
10Maana Mose aliamuru: Waheshimu baba yako na mama yako, na, Anayemlaani baba au mama, lazima afe.
11But *ye* say, If a man say to his father or his mother, [It is] corban (that is, gift), whatsoever thou mightest have profit from me by ...
11Lakini ninyi mwafundisha, Kama mtu anacho kitu ambacho angeweza kuwasaidia nacho baba au mama yake, lakini akasema kwamba kitu hicho ni Korbani (yaani ni zawadi kwa Mungu),
12And ye no longer suffer him to do anything for his father or his mother;
12basi, halazimiki tena kuwasaidia wazazi wake.
13making void the word of God by your traditional teaching which ye have delivered; and many such like things ye do.
13Hivyo ndivyo mnavyodharau neno la Mungu kwa ajili ya mafundisho mnayopokezana. Tena mnafanya mambo mengi ya namna hiyo."
14And having called again the crowd, he said to them, Hear me, all [of you], and understand:
14Yesu aliuita tena ule umati wa watu, akawaambia, "Nisikilizeni nyote, mkaelewe.
15There is nothing from outside a man entering into him which can defile him; but the things which go out from him, those it is which defile the man.
15Hakuna kitu kinachoingia ndani ya mtu toka nje ambacho chaweza kumtia mtu najisi. Lakini kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia mtu najisi."
16If any one have ears to hear, let him hear.
16Mwenye masikio na asikie!
17And when he went indoors from the crowd, his disciples asked him concerning the parable.
17Alipouacha umati wa watu na kuingia nyumbani, wanafunzi wake walimwuliza maana ya huo mfano.
18And he says to them, Are *ye* also thus unintelligent? Do ye not perceive that all that is outside entering into the man cannot defile him,
18Naye akawaambia, "Je, hata ninyi hamwelewi? Je, hamwelewi kwamba kitu kinachomwingia mtu toka nje hakiwezi kumtia unajisi,
19because it does not enter into his heart but into his belly, and goes out into the draught, purging all meats?
19kwa maana hakimwingii moyoni, ila tumboni, na baadaye hutolewa nje chooni?" (Kwa kusema hivyo, Yesu alivihalalisha vyakula vyote.)
20And he said, That which goes forth out of the man, that defiles the man.
20Akaendelea kusema, "Kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia najisi.
21For from within, out of the heart of men, go forth evil thoughts, adulteries, fornications, murders,
21Kwa maana kutoka ndani, katika moyo wa mtu, hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji,
22thefts, covetousness, wickednesses, deceit, licentiousness, a wicked eye, injurious language, haughtiness, folly;
22uzinzi, uchoyo, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, kashfa, kiburi na upumbavu.
23all these wicked things go forth from within and defile the man.
23Maovu hayo yote yatoka ndani ya mtu, nayo humtia mtu najisi."
24And he rose up and went away thence into the borders of Tyre and Sidon; and having entered into a house he would not have any one know [it], and he could not be hid.
24Yesu aliondoka hapo, akaenda hadi wilaya ya Tiro. Huko aliingia katika nyumba moja na hakutaka mtu ajue; lakini hakuweza kujificha.
25But immediately a woman, whose little daughter had an unclean spirit, having heard of him, came and fell at his feet
25Mwanamke mmoja ambaye binti yake alikuwa na pepo, alisikia habari za Yesu. Basi, akaja akajitupa chini mbele ya miguu yake.
26(and the woman was a Greek, Syrophenician by race), and asked him that he would cast the demon out of her daughter.
26Mama huyo alikuwa Mgiriki, mwenyeji wa Sirofoinike. Basi, akamwomba Yesu amtoe binti yake pepo mchafu.
27But [Jesus] said to her, Suffer the children to be first filled; for it is not right to take the children's bread and cast it to the dogs.
27Yesu akamwambia, "Kwanza watoto washibe; kwa maana si vizuri kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."
28But she answered and says to him, Yea, Lord; for even the dogs under the table eat of the children's crumbs.
28Lakini huyo mama akasema, "Sawa, Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto."
29And he said to her, Because of this word, go thy way, the demon is gone out of thy daughter.
29Yesu akamwambia, "Kwa sababu ya neno hilo, nenda. Pepo amemtoka binti yako!"
30And having gone away to her house she found the demon gone out, and her daughter lying on the bed.
30Basi, akaenda nyumbani kwake, akamkuta mtoto amelala kitandani, na pepo amekwisha mtoka.
31And again having left the borders of Tyre and Sidon, he came to the sea of Galilee, through the midst of the coasts of Decapolis.
31Kisha Yesu aliondoka wilayani Tiro, akapitia Sidoni, akafika ziwa Galilaya kwa kupitia nchi ya Dekapoli.
32And they bring to him a deaf [man] who could not speak right, and they beseech him that he might lay his hand on him.
32Basi, wakamletea bubu-kiziwi, wakamwomba amwekee mikono.
33And having taken him away from the crowd apart, he put his fingers to his ears; and having spit, he touched his tongue;
33Yesu akamtenga na umati wa watu, akamtia vidole masikioni, akatema mate na kumgusa ulimi.
34and looking up to heaven he groaned, and says to him, Ephphatha, that is, Be opened.
34Kisha akatazama juu mbinguni, akapiga kite, akamwambia, "Efatha," maana yake, "Funguka."
35And immediately his ears were opened, and the band of his tongue was loosed and he spoke right.
35Mara masikio yake yakafunguka na ulimi wake ukafunguliwa, akaanza kusema sawasawa.
36And he charged them that they should speak to no one [of it]. But so much the more *he* charged them, so much the more abundantly *they* proclaimed it;
36Yesu akawaamuru wasimwambie mtu juu ya jambo hilo. Lakini kadiri alivyowakataza, ndivyo walivyozidi kutangaza habari hiyo.
37and they were astonished above measure, saying, He does all things well; he makes both the deaf to hear, and the speechless to speak.
37Watu walishangaa sana, wakasema, "Amefanya yote vyema: amewajalia viziwi kusikia, na bubu kusema!"