1In those days, there being again a great crowd, and they having nothing that they could eat, having called his disciples to [him], he says to them,
1Wakati huo umati mkubwa wa watu ulikusanyika tena, na hawakuwa na chakula. Basi, Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia,
2I have compassion on the crowd, because they have stayed with me already three days and they have not anything they can eat,
2"Nawahurumia watu hawa kwa sababu wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu, wala hawana chakula.
3and if I should dismiss them to their home fasting, they will faint on the way; for some of them are come from far.
3Nikiwaacha waende nyumbani wakiwa na njaa watazimia njiani, maana baadhi yao wametoka mbali."
4And his disciples answered him, Whence shall one be able to satisfy these with bread here in a desert place?
4Wanafunzi wake wakamwuliza, "Hapa nyikani itapatikana wapi mikate ya kuwashibisha watu hawa wote?"
5And he asked them, How many loaves have ye? And they said, Seven.
5Yesu akawauliza, "Mnayo mikate mingapi?" Nao wakamjibu, "Saba."
6And he commanded the crowd to sit down on the ground. And having taken the seven loaves, he gave thanks, and broke [them] and gave [them] to his disciples, that they might set [them] before [them]; and they set [them] before the crowd.
6Basi, akawaamuru watu wakae chini. Akaitwaa ile mikate saba, akamshukuru Mungu, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu, nao wakawagawia.
7And they had a few small fishes, and having blessed them, he desired these also to be set before [them].
7Walikuwa pia na visamaki vichache. Yesu akavibariki, akaamuru vigawiwe watu vilevile.
8And they ate and were satisfied. And they took up of fragments that remained seven baskets.
8Watu wakala, wakashiba. Wakaokota mabaki yaliyosalia wakajaza makapu saba.
9And they [that had eaten] were about four thousand; and he sent them away.
9Nao waliokula walikuwa watu wapatao elfu nne. Yesu akawaaga,
10And immediately going on board ship with his disciples, he came into the parts of Dalmanutha.
10na mara akapanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akaenda wilaya ya Dalmanutha.
11And the Pharisees went out and began to dispute against him, seeking from him a sign from heaven, tempting him.
11Mafarisayo walikuja, wakaanza kujadiliana na Yesu. Kwa kumjaribu, wakamtaka awafanyie ishara kuonyesha anayo idhini kutoka mbinguni.
12And groaning in his spirit, he says, Why does this generation seek a sign? Verily I say unto you, A sign shall in no wise be given to this generation.
12Yesu akahuzunika rohoni, akasema, "Mbona kizazi hiki kinataka ishara? Kweli nawaambieni, kizazi hiki hakitapewa ishara yoyote!"
13And he left them, and going again on board ship, went away to the other side.
13Basi, akawaacha, akapanda tena mashua, akaanza safari kwenda ng'ambo ya pili ya ziwa.
14And they forgot to take bread, and save one loaf, they had not [any] with them in the ship.
14Wanafunzi walikuwa wamesahau kuchukua mikate; walikuwa na mkate mmoja tu katika mashua.
15And he charged them, saying, Take heed, beware of the leaven of the Pharisees and [of] the leaven of Herod.
15Yesu akawaonya, "Angalieni sana! Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode."
16And they reasoned with one another, [saying], It is because we have no bread.
16Wanafunzi wakaanza kujadiliana wao kwa wao, "Anasema hivyo kwa kuwa hatuna mikate."
17And Jesus knowing [it], says to them, Why reason ye because ye have no bread? Do ye not yet perceive nor understand? Have ye your heart [yet] hardened?
17Yesu alitambua hayo, akawaambia, "Mbona mnajadiliana juu ya kutokuwa na mikate? Je, bado hamjafahamu, wala hamjaelewa? Je, mioyo yenu imeshupaa?
18Having eyes, see ye not? and having ears, hear ye not? and do ye not remember?
18Je, Mnayo macho na hamwoni? Mnayo masikio na hamsikii? Je, hamkumbuki
19When I broke the five loaves for the five thousand, how many hand-baskets full of fragments took ye up? They say to him, Twelve.
19wakati ule nilipoimega ile mikate mitano na kuwapa watu elfu tano? Mlikusanya vikapu vingapi vya mabaki ya makombo?" Wakamjibu, "Kumi na viwili."
20And when the seven for the four thousand, the filling of how many baskets of fragments took ye up? And they said, Seven.
20"Na nilipoimega ile mikate saba na kuwapa watu elfu nne, mlikusanya makapu mangapi ya makombo?" Wakamjibu, "Saba."
21And he said to them, How do ye not yet understand?
21Basi, akawaambia, "Na bado hamjaelewa?"
22And he comes to Bethsaida; and they bring him a blind man, and beseech him that he might touch him.
22Yesu alifika Bethsaida pamoja na wanafunzi wake. Huko watu wakamletea kipofu mmoja, wakamwomba amguse.
23And taking hold of the hand of the blind man he led him forth out of the village, and having spit upon his eyes, he laid his hands upon him, and asked him if he beheld anything.
23Yesu akamshika mkono huyo kipofu, akampeleka nje ya kijiji. Akamtemea mate machoni, akamwekea mikono, akamwuliza, "Je, unaweza kuona kitu?"
24And having looked up, he said, I behold men, for I see [them], as trees, walking.
24Huyo kipofu akatazama, akasema, "Ninawaona watu wanaoonekana kama miti inayotembea."
25Then he laid his hands again upon his eyes, and he saw distinctly, and was restored and saw all things clearly.
25Kisha Yesu akamwekea tena mikono machoni, naye akakaza macho, uwezo wake wa kuona ukamrudia, akaona kila kitu sawasawa.
26And he sent him to his house, saying, Neither enter into the village, nor tell [it] to any one in the village.
26Yesu akamwambia aende zake nyumbani na kumwamuru, "Usirudi kijijini!"
27And Jesus went forth and his disciples, into the villages of Caesarea-Philippi. And by the way he asked his disciples, saying unto them, Who do men say that I am?
27Kisha Yesu na wanafunzi wake walikwenda katika vijiji vya Kaisarea Filipi. Walipokuwa njiani, Yesu aliwauliza wanafunzi wake, "Watu wanasema mimi ni nani?"
28And they answered him, saying, John the baptist; and others, Elias; but others, One of the prophets.
28Wakamjibu, "Wengine wanasema wewe ni Yohane Mbatizaji, wengine Eliya na wengine mmojawapo wa manabii."
29And he asked them, But *ye*, who do ye say that I am? And Peter answering says to him, *Thou* art the Christ.
29Naye akawauliza, "Na ninyi je, mnasema mimi ni nani?" Petro akamjibu, "Wewe ndiwe Kristo."
30And he charged them straitly, in order that they should tell no man about him.
30Kisha Yesu akawaonya wasimwambie mtu yeyote habari zake.
31And he began to teach them that the Son of man must suffer many things, and be rejected of the elders and of the chief priests and of the scribes, and be killed, and after three days rise [again].
31Yesu alianza kuwafundisha wanafunzi wake: "Ni lazima Mwana wa Mtu apatwe na mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu na walimu wa Sheria. Atauawa na baada ya siku tatu atafufuka."
32And he spoke the thing openly. And Peter, taking him to [him], began to rebuke him.
32Yesu aliwaambia jambo hilo waziwazi. Basi, Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea.
33But he, turning round and seeing his disciples, rebuked Peter, saying, Get away behind me, Satan, for thy mind is not on the things that are of God, but on the things that are of men.
33Lakini Yesu akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro akisema, "Ondoka mbele yangu, Shetani! Fikira zako si za kimungu ila ni za kibinadamu!"
34And having called the crowd with his disciples, he said to them, Whoever desires to come after me, let him deny himself, and take up his cross and follow me.
34Kisha akauita umati wa watu pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, "Mtu yeyote akitaka kuwa mfuasi wangu, lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.
35For whosoever shall desire to save his life shall lose it, but whosoever shall lose his life for my sake and the gospel's shall save it.
35Maana mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza, lakini mtu atakayepoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Habari Njema, atayaokoa.
36For what shall it profit a man if he gain the whole world and suffer the loss of his soul?
36Je, kuna faida gani mtu kuupata ulimwengu wote na kuyapoteza maisha yake?
37for what should a man give in exchange for his soul?
37Ama mtu atatoa kitu gani badala ya maisha yake?
38For whosoever shall be ashamed of me and of my words in this adulterous and sinful generation, of him shall the Son of man also be ashamed when he shall come in the glory of his Father with the holy angels.
38Mtu yeyote katika kizazi hiki kiovu na kisichomjali Mungu anayenionea aibu mimi na mafundisho yangu, Mwana wa Mtu atamwonea aibu mtu huyo wakati atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu."