1Siku moja, saa tisa alasiri, Petro na Yohane walikuwa wanakwenda Hekaluni, wakati wa sala.
1And Peter and John were going up at the same time to the temple, at the hour of the prayer, the ninth [hour],
2Na pale karibu na mlango wa Hekalu uitwao "Mlango Mzuri", palikuwa na mtu mmoja, kiwete tangu kuzaliwa. Watu walimbeba huyo mtu kila siku na kumweka hapo ili aombe chochote kwa wale waliokuwa wakiingia Hekaluni.
2and a certain man, being lame from the womb of his mother, was being carried, whom they were laying every day at the gate of the temple, called Beautiful, to ask a kindness from those entering into the temple,
3Alipowaona Petro na Yohane wakiingia Hekaluni, aliwaomba wampe chochote.
3who, having seen Peter and John about to go into the temple, was begging to receive a kindness.
4Petro na Yohane walimkodolea macho, naye Petro akamwambia, "Tutazame!"
4And Peter, having looked stedfastly toward him with John, said, `Look toward us;`
5Naye akawageukia, akitazamia kupata kitu kutoka kwao.
5and he was giving heed to them, looking to receive something from them;
6Kisha Petro akamwambia, "Sina fedha wala dhahabu lakini kile nilicho nacho nitakupa. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, tembea!"
6and Peter said, `Silver and gold I have none, but what I have, that I give to thee; in the name of Jesus Christ of Nazareth, rise up and be walking.`
7Halafu, akamshika mkono wa kulia, akamwinua. Papo hapo miguu na magoti yake yakapata nguvu.
7And having seized him by the right hand, he raised [him] up, and presently his feet and ankles were strengthened,
8Akaruka, akasimama na kuanza kutembea. Halafu akaingia pamoja nao Hekaluni, akitembea na kurukaruka huku akimtukuza Mungu.
8and springing up, he stood, and was walking, and did enter with them into the temple, walking and springing, and praising God;
9Watu wote waliokuwa hapo walimwona akitembea na kumsifu Mungu.
9and all the people saw him walking and praising God,
10Walipomtambua kuwa ndiye yule aliyekuwa anaombaomba karibu na ule "Mlango Mzuri" wa Hekalu, wakashangaa mno hata wasiweze kuelewa yaliyompata.
10they were knowing him also that this it was who for a kindness was sitting at the Beautiful gate of the temple, and they were filled with wonder and amazement at what hath happened to him.
11Watu wote, wakiwa na mshangao mkubwa wakaanza kukimbilia mahali palipoitwa "Ukumbi wa Solomoni," ambapo yule mtu alikuwa bado anaandamana na Petro na Yohane.
11And at the lame man who was healed holding Peter and John, all the people ran together unto them in the porch called Solomon`s — greatly amazed,
12Basi, Petro alipowaona watu hao akawaambia, "Wananchi wa Israeli, kwa nini mnashangazwa na jambo hili? Mbona mnatukodolea macho kana kwamba ni kwa nguvu zetu au utakatifu wetu sisi wenyewe tumemfanya mtu huyu aweze kutembea?
12and Peter having seen, answered unto the people, `Men, Israelites! why wonder ye at this? or on us why look ye so earnestly, as if by our own power or piety we have made him to walk?
13Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, Mungu wa baba zetu amemtukuza Yesu mtumishi wake. Yeye ndiye yuleyule mliyemtia mikononi mwa wakuu na kumkataa mbele ya Pilato hata baada ya Pilato kuamua kumwacha huru.
13`The God of Abraham, and of Isaac, and of Jacob, the God of our fathers, did glorify His child Jesus, whom ye delivered up, and denied him in the presence of Pilate, he having given judgment to release [him],
14Alikuwa mtakatifu na mwema; lakini ninyi mlimkataa, mkataka mtu mwingine aliyekuwa muuaji afunguliwe.
14and ye the Holy and Righteous One did deny, and desired a man — a murderer — to be granted to you,
15Basi, mlimuua yule ambaye ni chanzo cha uzima. Lakini Mungu alimfufua, na sisi ni mashahidi wa tukio hilo.
15and the Prince of the life ye did kill, whom God did raise out of the dead, of which we are witnesses;
16Jina la Yesu na imani katika jina hilo ndivyo vilivyompa nguvu mtu huyu mnayemwona na kumfahamu. Imani kwa Yesu ndiyo iliyomponya kabisa mtu huyu kama mnavyoona nyote.
16and on the faith of his name, this one whom ye see and have known, his name made strong, even the faith that [is] through him did give to him this perfect soundness before you all.
17"Sasa ndugu zangu, nafahamu kwamba ninyi na wakuu wenu mlitenda hayo kwa sababu ya kutojua kwenu.
17`And now, brethren, I have known that through ignorance ye did [it], as also your rulers;
18Lakini ndivyo Mungu alivyotimiza yale aliyotangaza zamani kwa njia ya manabii wote, kwamba ilikuwa lazima Kristo wake ateseke.
18and God, what things before He had declared through the mouth of all His prophets, that the Christ should suffer, He did thus fulfil;
19Basi, tubuni mkamrudie Mungu ili afute dhambi zenu.
19reform ye, therefore, and turn back, for your sins being blotted out, that times of refreshing may come from the presence of the Lord,
20Fanyeni hivyo ili Bwana awape nyakati za kuburudika rohoni na kuwaletea yule Kristo aliyemteua ambaye ndiye Yesu.
20and He may send Jesus Christ who before hath been preached to you,
21Ni lazima yeye abaki huko mbinguni mpaka utakapofika wakati wa kurekebishwa vitu vyote, kama Mungu alivyosema kwa njia ya manabii wake watakatifu wa tangu zamani.
21whom it behoveth heaven, indeed, to receive till times of a restitution of all things, of which God spake through the mouth of all His holy prophets from the age.
22Kwa maana Mose alisema, Bwana Mungu wenu atawapelekeeni nabii kama mimi kutoka kati yenu ninyi wenyewe.
22`For Moses, indeed, unto the fathers said — A prophet to you shall the Lord your God raise up out of your brethren, like to me; him shall ye hear in all things, as many as he may speak unto you;
23Yeyote yule ambaye hatamsikiliza nabii huyo atatengwa mbali na watu wa Mungu na kuangamizwa.
23and it shall be, every soul that may not hear that prophet shall be utterly destroyed out of the people;
24Manabii wote, kuanzia Samweli na wale waliomfuata, walitangaza habari za mambo haya ambayo yamekuwa yakitendeka siku hizi.
24and also all the prophets from Samuel and those following in order, as many as spake, did also foretell of these days.
25Ahadi zile Mungu alizotoa kwa njia ya manabii ni kwa ajili yenu; na mnashiriki lile agano Mungu alilofanya na babu zenu, kama alivyomwambia Abrahamu: Kwa njia ya wazawa wako, jamaa zote za dunia zitabarikiwa.
25`Ye are sons of the prophets, and of the covenant that God made unto our fathers, saying unto Abraham: And in thy seed shall be blessed all the families of the earth;
26Basi, ilikuwa kwa ajili yenu kwanza kwamba Mungu alimfufua mtumishi wake, alimtuma awabariki kwa kumfanya kila mmoja wenu aachane kabisa na maovu yake."
26to you first, God, having raised up His child Jesus, did send him, blessing you, in the turning away of each one from your evil ways.`