1Baada ya Sabato, karibu na mapambazuko ya siku ile ya Jumapili, Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikwenda kutazama lile kaburi.
1And on the eve of the sabbaths, at the dawn, toward the first of the sabbaths, came Mary the Magdalene, and the other Mary, to see the sepulchre,
2Ghafla kutatokea tetemeko kubwa la nchi; malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akalivingirisha lile jiwe, akalikalia.
2and lo, there came a great earthquake, for a messenger of the Lord, having come down out of heaven, having come, did roll away the stone from the door, and was sitting upon it,
3Alionekana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji.
3and his countenance was as lightning, and his clothing white as snow,
4Walinzi wa lile kaburi wakatetemeka kwa hofu kubwa, hata wakawa kama wamekufa.
4and from the fear of him did the keepers shake, and they became as dead men.
5Lakini yule malaika akawaambia wale wanawake, "Ninyi msiogope! Najua kwamba mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa.
5And the messenger answering said to the women, `Fear not ye, for I have known that Jesus, who hath been crucified, ye seek;
6Hayupo hapa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni mkaone mahali alipokuwa amelala.
6he is not here, for he rose, as he said; come, see the place where the Lord was lying;
7Basi, nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake kwamba amefufuka kutoka wafu, na sasa anawatangulieni kule Galilaya; huko mtamwona. Haya, mimi nimekwisha waambieni."
7and having gone quickly, say ye to his disciples, that he rose from the dead; and lo, he doth go before you to Galilee, there ye shall see him; lo, I have told you.`
8Wakiwa wenye hofu na furaha kubwa, hao wanawake walitoka upesi kaburini, wakakimbia kwenda kuwaambia wanafunzi wake.
8And having gone forth quickly from the tomb, with fear and great joy, they ran to tell to his disciples;
9Mara, Yesu akakutana nao, akawasalimu: "Salamu." Hao wanawake wakamwendea, wakapiga magoti mbele yake, wakashika miguu yake.
9and as they were going to tell to his disciples, then lo, Jesus met them, saying, `Hail!` and they having come near, laid hold of his feet, and did bow to him.
10Kisha Yesu akawaambia, "Msiogope! Nendeni mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, na huko wataniona."
10Then saith Jesus to them, `Fear ye not, go away, tell to my brethren that they may go away to Galilee, and there they shall see me.`
11Wale wanawake walipokuwa wanakwenda zao, baadhi ya walinzi wa lile kaburi walikwenda mjini kutoa taarifa kwa makuhani wakuu juu ya mambo yote yaliyotukia.
11And while they are going on, lo, certain of the watch having come to the city, told to the chief priests all the things that happened,
12Basi, wakakutana pamoja na wazee, na baada ya kushauriana, wakawapa wale askari kiasi kikubwa cha fedha
12and having been gathered together with the elders, counsel also having taken, they gave much money to the soldiers,
13wakisema, "Ninyi mtasema hivi: Wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba sisi tukiwa tumelala.
13saying, `Say ye, that his disciples having come by night, stole him — we being asleep;
14Na kama mkuu wa mkoa akijua jambo hili, sisi tutasema naye na kuhakikisha kuwa ninyi hamtapata matatizo."
14and if this be heard by the governor, we will persuade him, and you keep free from anxiety.`
15Wale walinzi wakazichukua zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Habari hiyo imeenea kati ya Wayahudi mpaka leo.
15And they, having received the money, did as they were taught, and this account was spread abroad among Jews till this day.
16Wale wanafunzi kumi na mmoja walikwenda Galilaya kwenye ule mlima aliowaagiza Yesu.
16And the eleven disciples went to Galilee, to the mount where Jesus appointed them,
17Walipomwona, wakamwabudu, ingawa wengine walikuwa na mashaka.
17and having seen him, they bowed to him, but some did waver.
18Yesu akaja karibu, akawaambia, "Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
18And having come near, Jesus spake to them, saying, `Given to me was all authority in heaven and on earth;
19Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu; mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.
19having gone, then, disciple all the nations, (baptizing them — to the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit,
20Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati."
20teaching them to observe all, whatever I did command you,) and lo, I am with you all the days — till the full end of the age.`