1Wakati huo, mtawala Herode alisikia sifa za Yesu.
1في ذلك الوقت سمع هيرودس رئيس الربع خبر يسوع.
2Basi, akawaambia watumishi wake, "Mtu huyu ni Yohane mbatizaji, amefufuka kutoka wafu; ndiyo maana nguvu za miujiza zinafanya kazi ndani yake."
2فقال لغلمانه هذا هو يوحنا المعمدان. قد قام من الاموات ولذلك تعمل به القوات
3Herode ndiye aliyekuwa amemtia Yohane nguvuni, akamfunga minyororo na kumtia gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake. Sababu hasa ni
3فان هيرودس كان قد امسك يوحنا واوثقه وطرحه في سجن من اجل هيروديا امرأة فيلبس اخيه.
4kwamba alikuwa amemwambia Herode, "Si halali kwako kuishi na huyo mwanamke!"
4لان يوحنا كان يقول له لا يحل ان تكون لك.
5Herode alitaka kumwua Yohane, lakini aliogopa watu kwa sababu kwao Yohane alikuwa nabii.
5ولما اراد ان يقتله خاف من الشعب. لانه كان عندهم مثل نبي.
6Katika sherehe za sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya wageni. Herode alifurahiwa,
6ثم لما صار مولد هيرودس رقصت ابنة هيروديا في الوسط فسرّت هيرودس.
7hata akaahidi kwa kiapo kumpa huyo msichana chochote atakachoomba.
7من ثم وعد بقسم انه مهما طلبت يعطيها.
8Naye, huku akichochewa na mama yake, akaomba, "Nipe papahapa katika sinia kichwa cha Yohane mbatizaji."
8فهي اذ كانت قد تلقنت من امها قالت أعطيني ههنا على طبق راس يوحنا المعمدان.
9Mfalme alihuzunika, lakini kwa sababu ya kile kiapo chake na kwa sababu ya wale wageni karamuni, akaamuru apewe.
9فاغتم الملك. ولكن من اجل الاقسام والمتكئين معه أمر ان يعطى.
10Basi, Herode akatuma mtu gerezani amkate kichwa Yohane.
10فارسل وقطع راس يوحنا في السجن.
11Kichwa chake kikaletwa katika sinia, wakampa yule msichana, naye akampelekea mama yake.
11فأحضر رأسه على طبق ودفع الى الصبية. فجاءت به الى امها.
12Wanafunzi wa Yohane wakaja, wakauchukua mwili wake, wakauzika. Kisha wakaenda kumpasha habari Yesu.
12فتقدم تلاميذه ورفعوا الجسد ودفنوه. ثم أتوا واخبروا يسوع
13Yesu alipopata habari hiyo, aliondoka mahali pale kwa mashua, akaenda mahali pa faragha peke yake. Lakini watu walipata habari, wakamfuata kwa miguu toka mijini.
13فلما سمع يسوع انصرف من هناك في سفينة الى موضع خلاء منفردا. فسمع الجموع وتبعوه مشاة من المدن
14Basi, aliposhuka pwani, aliona umati mkubwa wa watu, akawaonea huruma, akawaponya wagonjwa wao.
14فلما خرج يسوع ابصر جمعا كثيرا فتحنن عليهم وشفى مرضاهم.
15Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, "Mahali hapa ni nyikani, na saa zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula."
15ولما صار المساء تقدم اليه تلاميذه قائلين الموضع خلاء والوقت قد مضى. اصرف الجموع لكي يمضوا الى القرى ويبتاعوا لهم طعاما.
16Yesu akawaambia, "Si lazima waende, wapeni ninyi chakula."
16فقال لهم يسوع لا حاجة لهم ان يمضوا. اعطوهم انتم ليأكلوا.
17Lakini wao wakamwambia, "Tunayo mikate mitano tu na samaki wawili."
17فقالوا له ليس عندنا ههنا الا خمسة ارغفة وسمكتان.
18Yesu akawaambia, "Nileteeni hapa."
18فقال ايتوني بها الى هنا.
19Akawaamuru watu waketi katika nyasi. Kisha akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akamshukuru Mungu. Halafu akaimega hiyo mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu.
19فامر الجموع ان يتكئوا على العشب. ثم اخذ الارغفة الخمسة والسمكتين ورفع نظره نحو السماء وبارك وكسر واعطى الارغفة للتلاميذ والتلاميذ للجموع.
20Watu wote wakala, wakashiba. Kisha wanafunzi wakakusanya mabaki, wakajaza vikapu kumi na viwili.
20فأكل الجميع وشبعوا. ثم رفعوا ما فضل من الكسر اثنتي عشر قفة مملوءة.
21Jumla ya waliokula ilikuwa wanaume wapatao elfu tano, bila kuhesabu wanawake na watoto.
21والآكلون كانوا نحو خمسة آلاف رجل ما عدا النساء والاولاد
22Mara, Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua, wamtangulie ng'ambo ya ziwa wakati yeye anawaaga watu.
22وللوقت ألزم يسوع تلاميذه ان يدخلوا السفينة ويسبقوه الى العبر حتى يصرف الجموع.
23Baada ya kuwaaga, alipanda mlimani peke yake kusali. Ilipokuwa jioni, yeye alikuwa huko peke yake,
23وبعدما صرف الجموع صعد الى الجبل منفردا ليصلّي. ولما صار المساء كان هناك وحده.
24na wakati huo ile mashua ilikwishafika karibu katikati ya ziwa, lakini ilikuwa inakwenda mrama kwa sababu upepo ulikuwa unaipinga.
24واما السفينة فكانت قد صارت في وسط البحر معذبة من الامواج. لان الريح كانت مضادة.
25Usiku, karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji.
25وفي الهزيع الرابع من الليل مضى اليهم يسوع ماشيا على البحر.
26Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji waliingiwa na hofu, wakasema, "Ni mzimu!" Wakapiga kelele kwa hofu.
26فلما ابصره التلاميذ ماشيا على البحر اضطربوا قائلين انه خيال. ومن الخوف صرخوا.
27Mara, Yesu akasema nao, "Tulieni, ni mimi. Msiogope!"
27فللوقت كلمهم يسوع قائلا تشجعوا. انا هو. لا تخافوا.
28Petro akamwambia, "Bwana, ikiwa ni wewe kweli, amuru nitembee juu ya maji nije kwako."
28فاجابه بطرس وقال يا سيد ان كنت انت هو فمرني ان آتي اليك على الماء.
29Yesu akasema, "Haya, njoo." Basi, Petro akashuka kutoka ile mashua, akatembea juu ya maji, akamwendea Yesu.
29فقال تعال. فنزل بطرس من السفينة ومشى على الماء ليأتي الى يسوع.
30Lakini alipouona ule upepo, aliogopa, akaanza kuzama; akalia kwa sauti, "Bwana, niokoe!"
30ولكن لما رأى الريح شديدة خاف واذ ابتدأ يغرق صرخ قائلا يا رب نجني.
31Hapo, Yesu akaunyosha mkono wake, akamshika na kumwambia, "Ewe mwenye imani haba! Kwa nini uliona shaka?"
31ففي الحال مدّ يسوع يده وامسك به وقال له يا قليل الايمان لماذا شككت.
32Basi, wakapanda mashuani, na upepo ukatulia.
32ولما دخلا السفينة سكنت الريح.
33Wote waliokuwa ndani ya mashua walimsujudia, wakasema, "Hakika wewe ni Mwana wa Mungu."
33والذين في السفينة جاءوا وسجدوا له قائلين بالحقيقة انت ابن الله
34Walivuka ziwa, wakafika nchi ya Genesareti.
34فلما عبروا جاءوا الى ارض جنيسارت.
35Watu wa huko walipomtambua, wakaeneza habari pote katika sehemu hizo. Basi, wakamletea Yesu wagonjwa wote,
35فعرفه رجال ذلك المكان. فارسلوا الى جميع تلك الكورة المحيطة واحضروا اليه جميع المرضى.
36wakamwomba awaruhusu waguse tu pindo la vazi lake; wote waliomgusa walipona.
36وطلبوا اليه ان يلمسوا هدب ثوبه فقط. فجميع الذين لمسوه نالوا الشفاء