1Kisha Mafarisayo na walimu wa Sheria wakafika kutoka Yerusalemu, wakamwendea Yesu, wakamwuliza,
1حينئذ جاء الى يسوع كتبة وفريسيون الذين من اورشليم قائلين.
2"Kwa nini wanafunzi wako hawajali mapokeo tuliyopokea kutoka kwa wazee wetu? Hawanawi mikono yao kama ipasavyo kabla ya kula!"
2لماذا يتعدى تلاميذك تقليد الشيوخ. فانهم لا يغسلون ايديهم حينما ياكلون خبزا.
3Yesu akawajibu, "Kwa nini nanyi mnapendelea mapokeo yenu wenyewe na hamuijali Sheria ya Mungu?
3فاجاب وقال لهم وانتم ايضا لماذا تتعدون وصية الله بسبب تقليدكم.
4Mungu amesema: Waheshimu baba yako na mama yako, na Anayemkashifu baba yake au mama yake, lazima auawe.
4فان الله اوصى قائلا اكرم اباك وامك. ومن يشتم ابا او اما فليمت موتا.
5Lakini ninyi mwafundisha ati mtu akiwa na kitu ambacho angeweza kuwasaidia nacho baba au mama yake, lakini akasema: Kitu hiki nimemtolea Mungu,
5واما انتم فتقولون من قال لابيه او امه قربان هو الذي تنتفع به مني. فلا يكرم اباه او امه.
6basi, hapaswi tena kumheshimu baba yake! Ndivyo mnavyodharau neno la Mungu kwa kufuata mafundisho yenu wenyewe.
6فقد ابطلتم وصية الله بسبب تقليدكم.
7Enyi wanafiki! Isaya alitabiri sawa kabisa juu yenu:
7يا مراؤون حسنا تنبأ عنكم اشعياء قائلا.
8Watu hawa, asema Mungu, huniheshimu kwa maneno tu, lakini mioyoni mwao wako mbali nami.
8يقترب اليّ هذا الشعب بفمه ويكرمني بشفتيه واما قلبه فمبتعد عني بعيدا.
9Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu."
9وباطلا يعبدونني وهم يعلمون تعاليم هي وصايا الناس
10Yesu aliuita ule umati wa watu, akawaambia, "Sikilizeni na muelewe!
10ثم دعا الجمع وقال لهم اسمعوا وافهموا.
11Kitu kinachomtia mtu najisi si kile kiingiacho kinywani, bali kile kitokacho kinywani. Hicho ndicho kimtiacho mtu najisi."
11ليس ما يدخل الفم ينجس الانسان. بل ما يخرج من الفم هذا ينجس الانسان.
12Kisha wanafunzi wakamwendea, wakamwambia, "Je, unajua kwamba Mafarisayo walichukizwa waliposikia maneno yako?"
12حينئذ تقدم تلاميذه وقالوا له اتعلم ان الفريسيين لما سمعوا القول نفروا.
13Lakini yeye akawajibu, "Kila mmea ambao Baba yangu aliye mbinguni hakuupanda, utang'olewa.
13فاجاب وقال كل غرس لم يغرسه ابي السماوي يقلع.
14Waacheni wenyewe! Wao ni vipofu, viongozi wa vipofu; na kipofu akimwongoza kipofu, wote wawili hutumbukia shimoni."
14اتركوهم. هم عميان قادة عميان. وان كان اعمى يقود اعمى يسقطان كلاهما في حفرة.
15Petro akadakia, "Tufafanulie huo mfano."
15فاجاب بطرس وقال له فسّر لنا هذا المثل.
16Yesu akasema, "Hata nyinyi hamwelewi?
16فقال يسوع هل انتم ايضا حتى الآن غير فاهمين.
17Je, hamwelewi kwamba kila kinachoingia kinywani huenda tumboni na baadaye hutupwa nje chooni?
17ألا تفهمون بعد ان كل ما يدخل الفم يمضي الى الجوف ويندفع الى المخرج.
18Lakini yale yatokayo kinywani hutoka moyoni, na hayo ndiyo yanayomtia mtu najisi.
18واما ما يخرج من الفم فمن القلب يصدر. وذلك ينجس الانسان.
19Maana moyoni hutoka mawazo maovu yanayosababisha uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na kashfa.
19لان من القلب تخرج افكار شريرة قتل زنى فسق سرقة شهادة زور تجديف.
20Hayo ndiyo yanayomtia mtu najisi. Lakini kula chakula bila kunawa mikono hakumtii mtu najisi."
20هذه هي التي تنجس الانسان. واما الأكل بايد غير مغسولة فلا ينجس الانسان
21Yesu aliondoka mahali hapo akaenda kukaa katika sehemu za Tiro na Sidoni.
21ثم خرج يسوع من هناك وانصرف الى نواحي صور وصيدا.
22Basi, mama mmoja Mkaanani wa nchi hiyo alimjia, akapaaza sauti: "Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, nionee huruma! Binti yangu anasumbuliwa na pepo."
22واذا امرأة كنعانية خارجة من تلك التخوم صرخت اليه قائلة ارحمني يا سيد يا ابن داود. ابنتي مجنونة جدا.
23Lakini Yesu hakumjibu neno. Basi, wanafunzi wake wakamwendea, wakamwambia, "Mwambie aende zake kwa maana anatufuatafuata akipiga kelele."
23فلم يجبها بكلمة. فتقدم تلاميذه وطلبوا اليه قائلين اصرفها لانها تصيح وراءنا.
24Yesu akajibu, "Sikutumwa ila kwa watu wa Israeli waliopotea kama kondoo."
24فاجاب وقال لم أرسل الا الى خراف بيت اسرائيل الضالة.
25Hapo huyo mama akaja, akapiga magoti mbele yake, akasema, "Mheshimiwa, nisaidie."
25فأتت وسجدت له قائلة يا سيد أعنّي.
26Yesu akamjibu, "Si sawa kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."
26فاجاب وقال ليس حسنا ان يؤخذ خبز البنين ويطرح للكلاب.
27Huyo mama akajibu, "Ni kweli, Mheshimiwa; lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka meza ya bwana wao."
27فقالت نعم يا سيد. والكلاب ايضا تأكل من الفتات الذي يسقط من مائدة اربابها.
28Hapo Yesu akamjibu, "Mama, imani yako ni kubwa; basi, ufanyiwe kama unavyotaka." Yule binti yake akapona tangu saa hiyo wakati huohuo.
28حينئذ اجاب يسوع وقال لها يا امرأة عظيم ايمانك. ليكن لك كما تريدين. فشفيت ابنتها من تلك الساعة
29Yesu alitoka hapo akaenda kando ya ziwa Galilaya, akapanda mlimani, akaketi.
29ثم انتقل يسوع من هناك وجاء الى جانب بحر الجليل. وصعد الى الجبل وجلس هناك.
30Watu wengi sana wakamjia wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaweka mbele ya miguu yake, naye Yesu akawaponya.
30فجاء اليه جموع كثيرة معهم عرج وعمي وخرس وشل وآخرون كثيرون. وطرحوهم عند قدمي يسوع. فشفاهم
31Umati ule wa watu ulishangaa sana ulipoona bubu wakiongea, waliokuwa wamelemaa wamepona, viwete wakitembea na vipofu wakiona; wakamsifu Mungu wa Israeli.
31حتى تعجب الجموع اذ رأوا الخرس يتكلمون والشل يصحّون والعرج يمشون والعمي يبصرون. ومجدوا اله اسرائيل
32Basi, Yesu aliwaita wanafunzi wake, akasema, "Nawaonea watu hawa huruma kwa sababu kwa siku tatu wamekuwa nami, wala hawana chakula. Sipendi kuwaacha waende bila kula wasije wakazimia njiani."
32واما يسوع فدعا تلاميذه وقال اني اشفق على الجمع لان الآن لهم ثلاثة ايام يمكثون معي وليس لهم ما ياكلون. ولست اريد ان اصرفهم صائمين لئلا يخوّروا في الطريق.
33Wanafunzi wakamwambia, "Hapa tuko nyikani; tutapata wapi chakula cha kuwatosha watu wengi hivi?"
33فقال له تلاميذه من اين لنا في البرية خبز بهذا المقدار حتى يشبع جمعا هذا عدده.
34Yesu akawauliza, "Mnayo mikate mingapi?" Wakamjibu, "Saba na visamaki vichache."
34فقال لهم يسوع كم عندكم من الخبز. فقالوا سبعة وقليل من صغار السمك.
35Basi, Yesu akawaamuru watu wakae chini.
35فأمر الجموع ان يتكئوا على الارض.
36Akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akamshukuru Mungu, akavimega, akawapa wanafunzi, nao wakawagawia watu.
36واخذ السبع خبزات والسمك وشكر وكسر واعطى تلاميذه والتلاميذ اعطوا الجمع
37Wote wakala, wakashiba. Kisha wakakusanya makombo, wakajaza vikapu saba.
37فاكل الجميع وشبعوا. ثم رفعوا ما فضل من الكسر سبعة سلال مملوءة.
38Hao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila kuhesabu wanawake na watoto.
38والآكلون كانوا اربعة آلاف رجل ما عدا النساء والاولاد.
39Basi, Yesu akawaaga watu, akapanda mashua, akaenda katika eneo la Magadani.
39ثم صرف الجموع وصعد الى السفينة وجاء الى تخوم مجدل