Swahili: New Testament

American Standard Version

1 Corinthians

7

1Yahusu sasa mambo yale mliyoandika: naam, ni vizuri kama mtu haoi;
1Now concerning the things whereof ye wrote: It is good for a man not to touch a woman.
2lakini kwa sababu ya hatari ya uzinzi, basi, kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.
2But, because of fornications, let each man have his own wife, and let each woman have her own husband.
3Mume atimize wajibu alio nao kwa mkewe, naye mke atimize wajibu alio nao kwa mumewe.
3Let the husband render unto the wife her due: and likewise also the wife unto the husband.
4Mke hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mumewe anayo; hali kadhalika naye mume, hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mkewe anayo.
4The wife hath not power over her own body, but the husband: and likewise also the husband hath not power over his own body, but the wife.
5Msinyimane haki zenu, isipokuwa kama mnaafikiana kufanya hivyo kwa kitambo tu, ili mpate nafasi nzuri ya kusali. Kisha rudianeni tena mara, ili Shetani asije akawajaribu kwa sababu ya udhaifu wenu.
5Defraud ye not one the other, except it be by consent for a season, that ye may give yourselves unto prayer, and may be together again, that Satan tempt you not because of your incontinency.
6Ninayowaambieni sasa ni mawaidha, si amri.
6But this I say by way of concession, not of commandment.
7Ningependa watu wote wawe kama mimi nilivyo; lakini kila mmoja anacho kipaji chake kutoka kwa Mungu; mmoja kipaji hiki na mwingine kile.
7Yet I would that all men were even as I myself. Howbeit each man hath his own gift from God, one after this manner, and another after that.
8Basi, wale ambao hawajaoana na wale walio wajane nawaambia kwamba ni vema kuendelea kuwa kama mimi nilivyo.
8But I say to the unmarried and to widows, It is good for them if they abide even as I.
9Hata hivyo, kama mtu hawezi kujizuia basi, na aoe; maana ni afadhali zaidi kuoa kuliko kuwaka tamaa.
9But if they have not continency, let them marry: for it is better to marry than to burn.
10Kwa wale waliooa ninayo amri, tena si yangu, ila ni ya Bwana: mke asiachane na mumewe;
10But unto the married I give charge, [yea] not I, but the Lord, That the wife depart not from her husband
11lakini kama akiachana naye, basi abaki bila kuolewa; ama la, apatanishwe na mume wake. Mume naye asimpe talaka mkewe.
11(but should she depart, let her remain unmarried, or else be reconciled to her husband); and that the husband leave not his wife.
12Kwa wale wengine, (mimi binafsi, si Bwana) nasema hivi: Ikiwa mwanamume Mkristo anaye mke asiyeamini, na huyo mwanamke akakubali kuendelea kuishi naye, asimpe talaka.
12But to the rest say I, not the Lord: If any brother hath an unbelieving wife, and she is content to dwell with him, let him not leave her.
13Na, kama mwanamke Mkristo anaye mume asiyeamini, na huyo mwanamume akakubali kuendelea kuishi naye, basi, asimpe talaka mumewe.
13And the woman that hath an unbelieving husband, and he is content to dwell with her, let her not leave her husband.
14Kwa maana huyo mume asiyeamini hupokelewa kwa Mungu kwa kuungana na mkewe; na huyo mke asiyeamini hupokelewa kwa Mungu kwa kuungana na mumewe. Vinginevyo watoto wao wangekuwa si wa Mungu; kumbe sasa ni watoto wake Mungu.
14For the unbelieving husband is sanctified in the wife, and the unbelieving wife is sanctified in the brother: else were your children unclean; but now are they holy.
15Hata hivyo, ikiwa yule asiyeamini anataka kumwacha mwenzake aliye Mkristo, basi, na amwache tu. Hapo huyo Mkristo, mume au mke, atakuwa huru. Maana Mungu amewaiteni ninyi muishi kwa amani.
15Yet if the unbelieving departeth, let him depart: the brother or the sister is not under bondage in such [cases]: but God hath called us in peace.
16Wewe mama Mkristo, unawezaje kuwa na hakika kwamba hutaweza kumwokoa mume wako? Au wewe mume Mkristo, unawezaje kuwa na hakika kwamba hutaweza kumwokoa mkeo?
16For how knowest thou, O wife, whether thou shalt save thy husband? Or how knowest thou, O husband, whether thou shalt save thy wife?
17Kwa vyovyote kila mmoja na aishi kufuatana na vipaji alivyogawiwa na Bwana, na kama alivyoitwa na Mungu. Hili ndilo agizo langu kwa makanisa yote.
17Only, as the Lord hath distributed to each man, as God hath called each, so let him walk. And so ordain I in all the churches.
18Kama mtu aliitwa akiwa ametahiriwa, basi asijisingizie kwamba hakutahiriwa; na kama alipoitwa hakuwa ametahiriwa, basi na asitahiriwe.
18Was any man called being circumcised? Let him not become uncircumcised. Hath any been called in uncircumcision? Let him not be circumcised.
19Maana kutahiriwa au kutotahiriwa si kitu; kilicho muhimu ni kuzishika amri za Mungu.
19Circumcision is nothing, and uncircumcision is nothing; but the keeping of the commandments of God.
20Basi, kila mmoja na abaki kama alivyokuwa wakati alipoitwa.
20Let each man abide in that calling wherein he was called.
21Je, wewe ulikuwa mtumwa wakati ulipoitwa? Sawa, usijali; lakini ukipata fursa ya kuwa huru, itumie.
21Wast thou called being a bondservant? Care not for it: nay, even if thou canst become free, use [it] rather.
22Maana yeye aliyeitwa na Bwana akiwa mtumwa huyo huwa mtu huru wa Bwana. Hali kadhalika naye aliyeitwa akiwa mtu huru, huwa mtumwa wa Kristo.
22For he that was called in the Lord being a bondservant, is the Lord's freedman: likewise he that was called being free, is Christ's bondservant.
23Nyote mmenunuliwa kwa bei; kwa hiyo msiwe tena watumwa wa watu.
23Ye were bought with a price; become not bondservants of men.
24Ndugu zangu, kila mmoja wenu basi, na abaki na Mungu kama alivyokuwa wakati alipoitwa.
24Brethren, let each man, wherein he was called, therein abide with God.
25Sasa, kuhusu mabikira na waseja, sina amri kutoka kwa Bwana; lakini natoa maoni yangu mimi ambaye kwa huruma yake Bwana nastahili kuaminiwa.
25Now concerning virgins I have no commandment of the Lord: but I give my judgment, as one that hath obtained mercy of the Lord to be trustworthy.
26Basi, kutokana na shida iliyopo sasa nadhani ingefaa mtu abaki kama alivyo.
26I think therefore that this is good by reason of the distress that is upon us, [namely,] that it is good for a man to be as he is.
27Je, umeoa? Basi, usitake kuachana na mkeo. Wewe hukuoa? Basi, usitake kuoa.
27Art thou bound unto a wife? Seek not to be loosed. Art thou loosed from a wife? Seek not a wife.
28Lakini ikiwa utaoa hutakuwa umetenda dhambi; na msichana akiolewa hatakuwa ametenda dhambi. Hao watakaooana watapatwa na matatizo ya dunia hii, lakini mimi ningependa hayo yasiwapate ninyi.
28But shouldest thou marry, thou hast not sinned; and if a virgin marry, she hath not sinned. Yet such shall have tribulation in the flesh: and I would spare you.
29Ndugu, nataka kusema hivi: muda uliobaki ni mfupi. Na tangu sasa wale waliooa na waishi kama vile hawakuoa;
29But this I say, brethren, the time is shortened, that henceforth both those that have wives may be as though they had none;
30wenye kulia wawe kama hawalii, na wenye kufurahi wawe kama hawafurahi; wanaonunua wawe kama hawana kitu;
30and those that weep, as though they wept not; and those that rejoice, as though they rejoiced not; and those that buy, as though they possessed not;
31nao wenye shughuli na dunia hii wawe kama vile hawana shughuli sana nayo. Maana ulimwengu huu, kama tuujuavyo, unapita.
31and those that use the world, as not using it to the full: for the fashion of this world passeth away.
32Ningependa ninyi msiwe na wasiwasi. Mtu asiye na mke hujishughulisha na kazi ya Bwana jinsi atakavyompendeza Bwana.
32But I would have you to be free from cares. He that is unmarried is careful for the things of the Lord, how he may please the Lord:
33Mtu aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia jinsi atakavyompendeza mkewe,
33but he that is married is careful for the things of the world, how he may please his wife,
34naye amegawanyika. Mwanamke asiyeolewa au bikira hujishughulisha na mambo ya Bwana apate kujitolea mwili na roho kwa Bwana. Lakini mwanamke aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii jinsi atakavyompendeza mumewe.
34and is divided. [So] also the woman that is unmarried and the virgin is careful for the things of the Lord, that she may be holy both in body and in spirit: but she that is married is careful for the things of the world, how she may please her husband.
35Nawaambieni haya kwa faida yenu, na si kwa kuwawekeeni kizuio. Nataka tu muwe na mpango unaofaa, mpate kumtumikia Bwana kwa moyo na nia moja.
35And this I say for your own profit; not that I may cast a snare upon you, but for that which is seemly, and that ye may attend upon the Lord without distraction.
36Kama mtu anaona kwamba hamtendei vyema mchumba wake asipomwoa, na kama tamaa zake zinamshinda, na afanye atakavyo; waoane tu; hatakuwa ametenda dhambi.
36But if any man thinketh that he behaveth himself unseemly toward his virgin [daughter], if she be past the flower of her age, and if need so requireth, let him do what he will; he sinneth not; let them marry.
37Lakini kama huyo mwanamume akiamua kwa hiari moyoni mwake kutooa na kama anaweza kuzitawala tamaa zake na kuamua namna ya kufanya, basi, anafanya vizuri zaidi asipomwoa huyo mwenzake bikira.
37But he that standeth stedfast in his heart, having no necessity, but hath power as touching in his own heart, to keep his own virgin [daughter], shall do well.
38Kwa maneno mengine: yule anayeamua kumwoa huyo mchumba wake anafanya vema; naye anayeamua kutomwoa anafanya vema zaidi.
38So then both he that giveth his own virgin [daughter] in marriage doeth well; and he that giveth her not in marriage shall do better.
39Mwanamke huwa amefungwa na mumewe kwa muda wote mumewe aishipo. Lakini mumewe akifa, mama huyo yuko huru, na akipenda anaweza kuolewa na mtu yeyote, mradi tu iwe Kikristo.
39A wife is bound for so long time as her husband liveth; but if the husband be dead, she is free to be married to whom she will; only in the Lord.
40Lakini, nionavyo mimi, atakuwa na heri zaidi kama akibaki hivyo alivyo. Hayo ni maoni yangu, na nafikiri mimi pia ninaye Roho wa Mungu.
40But she is happier if she abide as she is, after my judgment: and I think that I also have the Spirit of God.