1Yahusu sasa vyakula vilivyotambikiwa sanamu: Tunajua kwamba sisi sote tuna ujuzi, lakini ujuzi huo huwafanya watu wawe na majivuno; lakini mapendo hujenga.
1Now concerning things sacrificed to idols: We know that we all have knowledge. Knowledge puffeth up, but love edifieth.
2Anayefikiri kwamba anajua kitu, kwa kweli hajui chochote kama inavyompasa.
2If any man thinketh that he knoweth anything, he knoweth not yet as he ought to know;
3Lakini anayempenda Mungu huyo anajulikana naye.
3but if any man loveth God, the same is known by him.
4Kwa hiyo, kuhusu vyakula vilivyotambikiwa sanamu, twajua kwamba sanamu si kitu duniani; twajua kwamba Mungu ni mmoja tu.
4Concerning therefore the eating of things sacrificed to idols, we know that no idol is [anything] in the world, and that there is no God but one.
5Hata kama viko vitu viitwavyo miungu duniani au mbinguni, na hata kama wako miungu na mabwana wengi,
5For though there be that are called gods, whether in heaven or on earth; as there are gods many, and lords many;
6hata hivyo, kwetu sisi yuko Mungu mmoja tu: Baba, Muumba wa vyote, ambaye kwa ajili yake sisi tuko. Pia yuko Bwana mmoja tu, Yesu Kristo, ambaye kwa njia yake vitu vyote viliumbwa, na sisi twaishi kwa njia yake.
6yet to us there is one God, the Father, of whom are all things, and we unto him; and one Lord, Jesus Christ, through whom are all things, and we through him.
7Lakini, si kila mtu anao ujuzi huu. Maana wako watu wengine waliokwisha zoea sanamu, watu ambao mpaka hivi sasa wanapokula vyakula huviona bado kama vyakula vilivyotambikiwa sanamu. Na kwa vile dhamiri zao ni dhaifu, hutiwa unajisi.
7Howbeit there is not in all men that knowledge: but some, being used until now to the idol, eat as [of] a thing sacrificed to an idol; and their conscience being weak is defiled.
8Lakini chakula hakiwezi kutupeleka karibu zaidi na Mungu. Tukiacha kukila hatupungukiwi kitu, tukikila hatuongezewi kitu.
8But food will not commend us to God: neither, if we eat not, are we the worse; nor, if we eat, are we the better.
9Lakini, jihadharini: huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katika dhambi.
9But take heed lest by any means this liberty of yours become a stumblingblock to the weak.
10Maana, mtu ambaye dhamiri yake ni dhaifu, akikuona wewe mwenye ujuzi unakula vyakula hivyo ndani ya hekalu la sanamu, je, hatatiwa moyo wa kula vyakula vilivyotambikiwa sanamu?
10For if a man see thee who hast knowledge sitting at meat in an idol's temple, will not his conscience, if he is weak, be emboldened to eat things sacrificed to idols?
11Hivyo, huyo ndugu yako dhaifu ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake, atapotea kwa sababu ya ujuzi wako.
11For through thy knowledge he that is weak perisheth, the brother for whose sake Christ died.
12Kama mkiwakosesha ndugu zenu jinsi hiyo na kuzijeruhi dhamiri zao dhaifu, mtakuwa mmemkosea Kristo.
12And thus, sinning against the brethren, and wounding their conscience when it is weak, ye sin against Christ.
13Kwa hiyo, ikiwa chakula husababisha kuanguka kwa ndugu yangu, sitakula nyama kamwe, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke katika dhambi.
13Wherefore, if meat causeth my brother to stumble, I will eat no flesh for evermore, that I cause not my brother to stumble.