Swahili: New Testament

American Standard Version

Ephesians

5

1Kwa hiyo, mwigeni Mungu, maana ninyi ni watoto wake wapenzi.
1Be ye therefore imitators of God, as beloved children;
2Upendo uongoze maisha yenu, kama vile Kristo alivyotupenda, na kwa ajili yetu akajitoa mwenyewe kama dhabihu yenye harufu nzuri na tambiko impendezayo Mungu.
2and walk in love, even as Christ also loved you, and gave himself up for us, an offering and a sacrifice to God for an odor of a sweet smell.
3Kwa vile ninyi ni watu wa Mungu, basi uasherati, uchafu wowote ule au choyo visitajwe kamwe miongoni mwenu.
3But fornication, and all uncleanness, or covetousness, let it not even be named among you, as becometh saints;
4Tena maneno ya aibu, ya upuuzi au ubishi, yote hayo hayafai kwenu; maneno ya kumshukuru Mungu ndiyo yanayofaa.
4nor filthiness, nor foolish talking, or jesting, which are not befitting: but rather giving of thanks.
5Jueni wazi kwamba mwasherati yeyote au mchafu au mfisadi, (ufisadi ni sawa na kuabudu sanamu), au mtu yeyote wa aina hiyo hataambulia chochote katika Utawala wa Kristo na wa Mungu.
5For this ye know of a surety, that no fornicator, nor unclean person, nor covetous man, who is an idolater, hath any inheritance in the kingdom of Christ and God.
6Msikubali kudanganywa na mtu kwa maneno matupu; maana, kwa sababu ya mambo kama hayo ghadhabu ya Mungu huwajia wote wasiomtii.
6Let no man deceive you with empty words: for because of these things cometh the wrath of God upon the sons of disobedience.
7Basi, msishirikiane nao.
7Be not ye therefore partakers with them;
8Zamani ninyi mlikuwa gizani, lakini sasa ninyi mko katika mwanga kwa kuungana na Bwana. Ishini kama watoto wa mwanga:
8For ye were once darkness, but are now light in the Lord: walk as children of light
9maana matokeo ya mwanga ni wema kamili, uadilifu na ukweli.
9(for the fruit of the light is in all goodness and righteousness and truth),
10Jaribuni kujua yale yanayompendeza Bwana.
10proving what is well-pleasing unto the Lord;
11Msishiriki katika matendo yasiyofaa, ya giza bali yafichueni.
11and have no fellowship with the unfruitful works of darkness, but rather even reprove them;
12Mambo yanayotendwa kwa siri ni aibu hata kuyataja.
12for the things which are done by them in secret it is a shame even to speak of.
13Lakini mambo yale yanayotendwa katika mwanga, ukweli wake hudhihirishwa;
13But all things when they are reproved are made manifest by the light: for everything that is made manifest is light.
14na kila kilichodhihirishwa huwa mwanga. Ndiyo maana Maandiko yasema: "Amka wewe uliyelala, fufuka kutoka wafu, naye Kristo atakuangaza."
14Wherefore [he] saith, Awake, thou that sleepest, and arise from the dead, and Christ shall shine upon thee.
15Basi, muwe waangalifu jinsi mnavyoishi: Msiishi kama wapumbavu, bali kama wenye hekima.
15Look therefore carefully how ye walk, not as unwise, but as wise;
16Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya.
16redeeming the time, because the days are evil.
17Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana.
17Wherefore be ye not foolish, but understand what the will of the Lord is.
18Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu.
18And be not drunken with wine, wherein is riot, but be filled with the Spirit;
19Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu.
19speaking one to another in psalms and hymns and spiritual songs, singing and making melody with your heart to the Lord;
20Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
20giving thanks always for all things in the name of our Lord Jesus Christ to God, even the Father;
21Kila mmoja amstahi mwenzake kwa sababu ya kumcha Kristo.
21subjecting yourselves one to another in the fear of Christ.
22Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana.
22Wives, [be in subjection] unto your own husbands, as unto the Lord.
23Maana mume anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa kanisa, mwili wake.
23For the husband is the head of the wife, and Christ also is the head of the church, [being] himself the saviour of the body.
24Kama vile kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo, wake wawatii waume zao katika mambo yote.
24But as the church is subject to Christ, so [let] the wives also [be] to their husbands in everything.
25Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake.
25Husbands, love your wives, even as Christ also loved the church, and gave himself up for it;
26Alifanya hivyo, ili kwa neno lake, aliweke wakfu kwa Mungu, baada ya kulifanya safi kwa kuliosha katika maji,
26that he might sanctify it, having cleansed it by the washing of water with the word,
27kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safu kabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo.
27that he might present the church to himself a glorious [church], not having spot or wrinkle or any such thing; but that it should be holy and without blemish.
28Basi, waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe.
28Even so ought husbands also to love their own wives as their own bodies. He that loveth his own wife loveth himself:
29(Hakuna mtu yeyote auchukiaye mwili wake; badala ya kuuchukia, huulisha na kuuvika. Ndivyo naye Kristo anavyolitunza kanisa,
29for no man ever hated his own flesh; but nourisheth and cherisheth it, even as Christ also the church;
30maana sisi ni viungo vya mwili wake.)
30because we are members of his body.
31Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Kwa hiyo, mwanamume atawaacha baba na mama yake, ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja."
31For this cause shall a man leave his father and mother, and shall cleave to his wife; and the two shall become one flesh.
32Kuna ukweli uliofichika katika maneno haya, nami naona kwamba yamhusu Kristo na kanisa lake.
32This mystery is great: but I speak in regard of Christ and of the church.
33Lakini yanawahusu ninyi pia: kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe.
33Nevertheless do ye also severally love each one his own wife even as himself; and [let] the wife [see] that she fear her husband.