1Siku sita kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu alifika Bethania alikoishi Lazaro ambaye Yesu alikuwa amemfufua kutoka wafu.
1Jesus therefore six days before the passover came to Bethany, where Lazarus was, whom Jesus raised from the dead.
2Huko walimwandalia chakula cha jioni, naye Martha akawa anawatumikia. Lazaro alikuwa mmoja wa wale waliokuwa mezani pamoja na Yesu.
2So they made him a supper there: and Martha served; but Lazarus was one of them that sat at meat with him.
3Basi, Maria alichukua chupa ya marashi ya nardo safi ya thamani kubwa, akampaka Yesu miguu na kuipangusa kwa nywele zake. Nyumba yote ikajaa harufu ya marashi.
3Mary therefore took a pound of ointment of pure nard, very precious, and anointed the feet of Jesus, and wiped his feet with her hair: and the house was filled with the odor of the ointment.
4Basi, Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili ambaye ndiye atakayemsaliti Yesu, akasema,
4But Judas Iscariot, one of his disciples, that should betray him, saith,
5"Kwa nini marashi hayo hayakuuzwa kwa fedha dinari mia tatu, wakapewa maskini?"
5Why was not this ointment sold for three hundred shillings, and given to the poor?
6Alisema hivyo, si kwa kuwa alijali chochote juu ya maskini, bali kwa sababu alikuwa mweka hazina, na kwa kuwa alikuwa mwizi, mara kwa mara aliiba kutoka katika hiyo hazina.
6Now this he said, not because he cared for the poor; but because he was a thief, and having the bag took away what was put therein.
7Lakini Yesu akasema, "Msimsumbue huyu mama! Mwacheni ayaweke kwa ajili ya siku ya mazishi yangu.
7Jesus therefore said, Suffer her to keep it against the day of my burying.
8Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini hamtakuwa nami siku zote."
8For the poor ye have always with you; but me ye have not always.
9Wayahudi wengi walisikia kwamba Yesu alikuwa Bethania. Basi, wakafika huko si tu kwa ajili ya kumwona Yesu, ila pia wapate kumwona Lazaro ambaye Yesu alimfufua kutoka wafu.
9The common people therefore of the Jews learned that he was there: and they came, not for Jesus' sake only, but that they might see Lazarus also, whom he had raised from the dead.
10Makuhani wakuu waliamua pia kumwua Lazaro,
10But the chief priests took counsel that they might put Lazarus also to death;
11Maana kwa sababu ya Lazaro Wayahudi wengi waliwaasi viongozi wao, wakamwamini Yesu.
11because that by reason of him many of the Jews went away, and believed on Jesus.
12Kesho yake, kundi kubwa la watu waliokuja kwenye sikukuu walisikia kuwa Yesu alikuwa njiani kuja Yerusalemu.
12On the morrow a great multitude that had come to the feast, when they heard that Jesus was coming to Jerusalem,
13Basi, wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki; wakapaaza sauti wakisema: "Hosana! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana. Abarikiwe mfalme wa Israeli."
13took the branches of the palm trees, and went forth to meet him, and cried out, Hosanna: Blessed [is] he that cometh in the name of the Lord, even the King of Israel.
14Yesu akampata mwana punda mmoja akapanda juu yake kama yasemavyo Maandiko:
14And Jesus, having found a young ass, sat thereon; as it is written,
15"Usiogope mji wa Sioni! Tazama, Mfalme wako anakuja, Amepanda mwana punda."
15Fear not, daughter of Zion: behold, thy King cometh, sitting on an ass's colt.
16Wakati huo wanafunzi wake hawakuelewa mambo hayo, lakini Yesu alipokwisha tukuzwa, ndipo walipokumbuka kwamba hayo yalikuwa yameandikwa juu yake, na kwamba watu walikuwa wamemtendea hivyo.
16These things understood not his disciples at the first: but when Jesus was glorified, then remembered they that these things were written of him, and that they had done these things unto him.
17Kundi la watu wale waliokuwa pamoja naye wakati alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua kutoka wafu, walisema yaliyotukia.
17The multitude therefore that was with him when he called Lazarus out of the tomb, and raised him from the dead, bare witness.
18Kwa hiyo umati huo wa watu ulimlaki, maana wote walisikia kwamba Yesu alikuwa amefanya ishara hiyo.
18For this cause also the multitude went and met him, for that they heard that he had done this sign.
19Basi, Mafarisayo wakaambiana, "Mnaona? Hatuwezi kufanya chochote! Tazameni, ulimwengu wote unamfuata."
19The Pharisees therefore said among themselves, Behold how ye prevail nothing: lo, the world is gone after him.
20Kulikuwa na Wagiriki kadhaa miongoni mwa watu waliokuwa wamefika Yerusalemu kuabudu wakati wa sikukuu hiyo.
20Now there were certain Greeks among those that went up to worship at the feast:
21Hao walimwendea Filipo, mwenyeji wa Bethsaida katika Galilaya, wakasema, "Mheshimiwa, tunataka kumwona Yesu."
21these therefore came to Philip, who was of Bethsaida of Galilee, and asked him, saying, Sir, we would see Jesus.
22Filipo akaenda akamwambia Andrea, nao wawili wakaenda kumwambia Yesu.
22Philip cometh and telleth Andrew: Andrew cometh, and Philip, and they tell Jesus.
23Yesu akawaambia, "Saa ya kutukuzwa kwa Mwana wa Mtu imefika!
23And Jesus answereth them, saying, The hour is come, that the Son of man should be glorified.
24Kweli nawaambieni, punje ya ngano hubaki punje tu isipokuwa ikianguka katika udongo na kufa. Kama ikifa, basi huzaa matunda mengi.
24Verily, verily, I say unto you, Except a grain of wheat fall into the earth and die, it abideth by itself alone; but if it die, it beareth much fruit.
25Anayependa maisha yake, atayapoteza; anayeyachukia maisha yake katika ulimwengu huu, atayaweka kwa ajili ya uzima wa milele.
25He that loveth his life loseth it; and he that hateth his life in this world shall keep it unto life eternal.
26Anayetaka kunitumikia ni lazima anifuate, hivyo kwamba popote pale nilipo mimi ndipo na mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu yeyote anayenitumikia Baba yangu atampa heshima.
26If any man serve me, let him follow me; and where I am, there shall also my servant be: if any man serve me, him will the Father honor.
27"Sasa roho yangu imefadhaika, na niseme nini? Je, niseme: Baba, usiruhusu saa hii inifikie? Lakini ndiyo maana nimekuja--ili nipite katika saa hii.
27Now is my soul troubled; and what shall I say? Father, save me from this hour. But for this cause came I unto this hour.
28Baba, ulitukuze jina lako." Hapo sauti ikasema kutoka mbinguni, "Nimelitukuza, na nitalitukuza tena."
28Father, glorify thy name. There came therefore a voice out of heaven, [saying], I have both glorified it, and will glorify it again.
29Umati wa watu waliokuwa wamesimama hapo walisikia sauti hiyo, na baadhi yao walisema, "Malaika ameongea naye!"
29The multitude therefore, that stood by, and heard it, said that it had thundered: others said, An angel hath spoken to him.
30Lakini Yesu akawaambia, "Sauti hiyo haikutokea kwa ajili yangu mimi, ila kwa ajili yenu.
30Jesus answered and said, This voice hath not come for my sake, but for your sakes.
31Sasa ndio wakati wa ulimwengu huu kuhukumiwa; sasa mtawala wa ulimwengu huu atapinduliwa.
31Now is the judgment of this world: now shall the prince of this world be cast out.
32Nami nitakapoinuliwa juu ya nchi nitamvuta kila mmoja kwangu."
32And I, if I be lifted up from the earth, will draw all men unto myself.
33(Kwa kusema hivyo alionyesha atakufa kifo gani).
33But this he said, signifying by what manner of death he should die.
34Basi, umati huo ukamjibu, "Sisi tunaambiwa na Sheria yetu kwamba Kristo atadumu milele. Wawezaje basi, kusema ati Mwana wa Mtu anapaswa kuinuliwa? Huyo Mwana wa Mtu ni nani?"
34The multitude therefore answered him, We have heard out of the law that the Christ abideth for ever: and how sayest thou, The Son of man must be lifted up? who is this Son of man?
35Yesu akawaambia, "Mwanga bado uko nanyi kwa muda mfupi. Tembeeni mngali mnao huo mwanga ili giza lisiwapate; maana atembeaye gizani hajui aendako.
35Jesus therefore said unto them, Yet a little while is the light among you. Walk while ye have the light, that darkness overtake you not: and he that walketh in the darkness knoweth not whither he goeth.
36Basi, wakati mnao huo mwanga uaminini ili mpate kuwa watu wa mwanga." Baada ya kusema maneno hayo, Yesu alikwenda zake na kujificha mbali nao.
36While ye have the light, believe on the light, that ye may become sons of light. These things spake Jesus, and he departed and hid himself from them.
37Ingawa Yesu alifanya miujiza hii yote mbele yao, wao hawakumwamini.
37But though he had done so many signs before them, yet they believed not on him:
38Hivyo maneno aliyosema nabii Isaya yakatimia: "Bwana, nani aliyeuamini ujumbe wetu? Na uwezo wa Bwana umedhihirishwa kwa nani?"
38that the word of Isaiah the prophet might be fulfilled, which he spake, Lord, who hath believed our report? And to whom hath the arm of the Lord been revealed?
39Hivyo hawakuweza kuamini, kwani Isaya tena alisema:
39For this cause they could not believe, for that Isaiah said again,
40"Mungu ameyapofusha macho yao, amezipumbaza akili zao; wasione kwa macho yao, wasielewe kwa akili zao; wala wasinigeukie, asema Bwana, ili nipate kuwaponya."
40He hath blinded their eyes, and he hardened their heart; Lest they should see with their eyes, and perceive with their heart, And should turn, And I should heal them.
41Isaya alisema maneno haya kwa sababu aliuona utukufu wa Yesu, akasema habari zake.
41These things said Isaiah, because he saw his glory; and he spake of him.
42Hata hivyo, wengi wa viongozi wa Wayahudi walimwamini Yesu. Lakini kwa sababu ya Mafarisayo, hawakumkiri hadharani kwa kuogopa kwamba watatengwa na sunagogi.
42Nevertheless even of the rulers many believed on him; but because of the Pharisees they did not confess [it], lest they should be put out of the synagogue:
43Walipendelea kusifiwa na watu kuliko kusifiwa na Mungu
43for they loved the glory [that is] of men more than the glory [that is] of God.
44Kisha Yesu akasema kwa sauti kubwa, "Mtu aliyeniamini, haniamini mimi tu, ila anamwamini pia yule aliyenituma.
44And Jesus cried and said, He that believeth on me, believeth not on me, but on him that sent me.
45Anayeniona mimi anamwona pia yule aliyenituma.
45And he that beholdeth me beholdeth him that sent me.
46Mimi ni mwanga, nami nimekuja ulimwenguni ili wote wanaoniamini wasibaki gizani.
46I am come a light into the world, that whosoever believeth on me may not abide in the darkness.
47Anayeyasikia maneno yangu lakini hayashiki mimi sitamhukumu; maana sikuja kuhukumu ulimwengu bali kuuokoa.
47And if any man hear my sayings, and keep them not, I judge him not: for I came not to judge the world, but to save the world.
48Asiyeyashika maneno yangu anaye wa kumhukumu: neno lile nililosema ni hakimu wake siku ya mwisho.
48He that rejecteth me, and receiveth not my sayings, hath one that judgeth him: the word that I spake, the same shall judge him in the last day.
49Mimi sikunena kwa mamlaka yangu mwenyewe, ila Baba aliyenituma ndiye aliyeniamuru niseme nini na niongee nini.
49For I spake not from myself; but the Father that sent me, he hath given me a commandment, what I should say, and what I should speak.
50Nami najua kuwa amri yake huleta uzima wa milele. Basi, mimi nasema tu yale Baba aliyoniagiza niyaseme."
50And I know that his commandment is life eternal: the things therefore which I speak, even as the Father hath said unto me, so I speak.