1"Wakati huo, Ufalme wa mbinguni utafanana na wasichana kumi waliochukua taa zao, wakaenda kumlaki bwana arusi.
1Then shall the kingdom of heaven be likened unto ten virgins, who took their lamps, and went forth to meet the bridegroom.
2Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara.
2And five of them were foolish, and five were wise.
3Wale wapumbavu walichukua taa zao, lakini hawakuchukua akiba ya mafuta.
3For the foolish, when they took their lamps, took no oil with them:
4Lakini wale wenye busara walichukua mafuta katika chupa pamoja na taa zao.
4but the wise took oil in their vessels with their lamps.
5Kwa kuwa bwana arusi alikawia kuja, wale wanawali wote wote walisinzia, wakalala.
5Now while the bridegroom tarried, they all slumbered and slept.
6Usiku wa manane kukawa na kelele: Haya, haya! Bwana arusi anakuja; nendeni kumlaki.
6But at midnight there is a cry, Behold, the bridegroom! Come ye forth to meet him.
7Hapo wale wanawali wote wakaamka, wakazitayarisha taa zao.
7Then all those virgins arose, and trimmed their lamps.
8Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara: Tupeni mafuta yenu kidogo maana taa zetu zinazimika.
8And the foolish said unto the wise, Give us of your oil; for our lamps are going out.
9Lakini wale wenye busara wakawaambia, Hayatatutosha sisi na ninyi! Afadhali mwende dukani mkajinunulie wenyewe!
9But the wise answered, saying, Peradventure there will not be enough for us and you: go ye rather to them that sell, and buy for yourselves.
10Basi, wale wanawali wapumbavu walipokwenda kununua mafuta, bwana arusi akafika, na wale wanawali waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye katika jumba la arusi, kisha mlango ukafungwa.
10And while they went away to buy, the bridegroom came; and they that were ready went in with him to the marriage feast: and the door was shut.
11Baadaye wale wanawali wengine wakaja, wakaita: Bwana, bwana, tufungulie!
11Afterward came also the other virgins, saying, Lord, Lord, open to us.
12Lakini yeye akawajibu, Nawaambieni kweli, siwajui ninyi."
12But he answered and said, Verily I say unto you, I know you not.
13Kisha Yesu akasema, "Kesheni basi, kwa maana hamjui siku wala saa.
13Watch therefore, for ye know not the day nor the hour.
14"Itakuwa kama mtu mmoja aliyetaka kusafiri ng'ambo: aliwaita watumishi wake, akawakabidhi mali yake.
14For [it is] as [when] a man, going into another country, called his own servants, and delivered unto them his goods.
15Alimpa kila mmoja kadiri ya uwezo wake: mmoja sarafu tano za fedha ziitwazo talanta, mwingine talanta mbili na mwingine talanta moja, kisha akasafiri.
15And unto one he gave five talents, to another two, to another one; to each according to his several ability; and he went on his journey.
16Mara yule aliyekabidhiwa talanta tano akafanya kazi nazo akapata faida talanta tano.
16Straightway he that received the five talents went and traded with them, and made other five talents.
17Hali kadhalika na yule aliyekabidhiwa talanta mbili akapata faida talanta mbili.
17In like manner he also that [received] the two gained other two.
18Lakini yule aliyekabidhiwa talanta moja akaenda akachimba shimo ardhini, akaificha fedha ya bwana wake.
18But he that received the one went away and digged in the earth, and hid his lord's money.
19"Baada ya muda mrefu, yule bwana alirudi, akaanza kukagua hesabu ya matumizi na mapato ya fedha yake.
19Now after a long time the lord of those servants cometh, and maketh a reckoning with them.
20Mtumishi aliyekabidhiwa talanta tano akaja amechukua zile talanta tano faida, akamwambia, Bwana, ulinikabidhi talanta tano, hapa pana talanta tano zaidi faida niliyopata.
20And he that received the five talents came and brought other five talents, saying, Lord, thou deliveredst unto me five talents: lo, I have gained other five talents.
21Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.
21His lord said unto him, Well done, good and faithful servant: thou hast been faithful over a few things, I will set thee over many things; enter thou into the joy of thy lord.
22"Mtumishi aliyekabidhiwa talanta mbili akaja, akatoa talanta mbili faida, akisema, Bwana, ulinikabidhi talanta mbili. Chukua talanta mbili zaidi faida niliyopata.
22And he also that [received] the two talents came and said, Lord, thou deliveredst unto me two talents: lo, I have gained other two talents.
23Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.
23His lord said unto him, Well done, good and faithful servant: thou hast been faithful over a few things, I will set thee over many things; enter thou into the joy of thy lord.
24"Lakini yule aliyekabidhiwa talanta moja akaja, akasema, Bwana, najua wewe ni mtu mgumu; wewe huvuna pale ambapo hukupanda, na kukusanya pale ambapo hukutawanya.
24And he also that had received the one talent came and said, Lord, I knew thee that thou art a hard man, reaping where thou didst not sow, and gathering where thou didst not scatter;
25Niliogopa, nikaificha fedha yako katika ardhi. Chukua basi mali yako.
25and I was afraid, and went away and hid thy talent in the earth: lo, thou hast thine own.
26"Bwana wake akamwambia, Wewe ni mtumishi mwovu na mvivu! Unajua kuwa mimi huvuna mahali ambapo sikupanda, na hukusanya pale ambapo sikutawanya.
26But his lord answered and said unto him, Thou wicked and slothful servant, thou knewest that I reap where I sowed not, and gather where I did not scatter;
27Ilikupasa basi, kuiweka fedha yangu katika benki, nami ningelichukua mtaji wangu na faida yake!
27thou oughtest therefore to have put my money to the bankers, and at my coming I should have received back mine own with interest.
28Basi, mnyang'anyeni hiyo fedha mkampe yule mwenye talanta kumi.
28Take ye away therefore the talent from him, and give it unto him that hath the ten talents.
29Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
29For unto every one that hath shall be given, and he shall have abundance: but from him that hath not, even that which he hath shall be taken away.
30Na kuhusu huyu mtumishi asiye na faida, mtupeni nje gizani! Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.
30And cast ye out the unprofitable servant into the outer darkness: there shall be the weeping and the gnashing of teeth.
31"Wakati Mwana wa Mtu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote wakiwa pamoja naye, hapo ataketi juu ya kiti chake cha enzi kitukufu,
31But when the Son of man shall come in his glory, and all the angels with him, then shall he sit on the throne of his glory:
32na mataifa yote yatakusanyika mbele yake, naye atawatenganisha watu kama mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi.
32and before him shall be gathered all the nations: and he shall separate them one from another, as the shepherd separateth the sheep from the goats;
33Atawaweka kondoo upande wake wa kulia na mbuzi upande wake wa kushoto.
33and he shall set the sheep on his right hand, but the goats on the left.
34"Kisha Mfalme atawaambia wale walio upande wake wa kulia, Njoni enyi mliobarikiwa na Baba yangu; pokeeni Ufalme mliotayarishiwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
34Then shall the King say unto them on his right hand, Come, ye blessed of my Father, inherit the kingdom prepared for you from the foundation of the world:
35Maana nilikuwa na njaa nanyi mkanipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi mkanipa maji; nilikuwa mgeni nanyi mkanikaribisha;
35for I was hungry, and ye gave me to eat; I was thirsty, and ye gave me drink; I was a stranger, and ye took me in;
36nilikuwa uchi, mkanivika; nilikuwa mgonjwa nanyi mkaja kunitazama; nilikuwa gerezani nanyi mkaja kunitembelea.
36naked, and ye clothed me; I was sick, and ye visited me; I was in prison, and ye came unto me.
37Hapo, hao watu wema watamjibu mfalme Bwana, ni lini tulikuona mwenye njaa nasi tukakupa chakula, au ukiwa na kiu nasi tukakunywesha maji?
37Then shall the righteous answer him, saying, Lord, when saw we thee hungry, and fed thee? or athirst, and gave thee drink?
38Ni lini tulikuona ukiwa mgeni nasi tukakukaribisha, au bila nguo nasi tukakuvika?
38And when saw we thee a stranger, and took thee in? or naked, and clothed thee?
39Ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au mfungwa nasi tukaja kukutazama?
39And when saw we thee sick, or in prison, and came unto thee?
40Mfalme atawajibu, Kweli nawaambieni, kila kitu mlichomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.
40And the King shall answer and say unto them, Verily I say unto you, Inasmuch as ye did it unto one of these my brethren, [even] these least, ye did it unto me.
41"Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, Ondokeni mbele yangu enyi mliolaaniwa! Nendeni katika moto wa milele aliotayarishiwa Ibilisi na malaika wake.
41Then shall he say also unto them on the left hand, Depart from me, ye cursed, into the eternal fire which is prepared for the devil and his angels:
42Maana nilikuwa na njaa nanyi hamkunipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi hamkunipa maji.
42for I was hungry, and ye did not give me to eat; I was thirsty, and ye gave me no drink;
43Nilikuwa mgeni nanyi hamkunikaribisha; nilikuwa mgonjwa na mfungwa nanyi hamkuja kunitazama.
43I was a stranger, and ye took me not in; naked, and ye clothed me not; sick, and in prison, and ye visited me not.
44"Hapo nao watajibu, Bwana, ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, ukiwa mgeni au bila nguo, ukiwa mgonjwa au mfungwa, nasi hatukuja kukuhudumia?
44Then shall they also answer, saying, Lord, when saw we thee hungry, or athirst, or a stranger, or naked, or sick, or in prison, and did not minister unto thee?
45Naye atawajibu, Nawaambieni kweli, kila mlipokataa kumtendea mambo haya mmojawapo wa hawa wadogo, mlikataa kunitendea mimi.
45Then shall he answer them, saying, Verily I say unto you, Inasmuch as ye did it not unto one of these least, ye did it not unto me.
46Basi, hawa watakwenda kwenye adhabu ya milele, lakini wale waadilifu watakwenda kwenye uzima wa milele."
46And these shall go away into eternal punishment: but the righteous into eternal life.