1Lakini wewe unapaswa kuhubiri mafundisho safi.
1Sina räägi aga seda, mis on kohane tervele õpetusele!
2Waambie wazee kwamba wanapaswa kuwa na kiasi, wawe na busara na wataratibu; wanapaswa kuwa timamu katika imani yao, upendo na uvumilivu.
2Vanad mehed olgu kained, väärikad, mõõdukad, terved usus, armastuses, kannatlikkuses.
3Hali kadhalika waambie wanawake wazee wawe na mwenendo wa uchaji wa Mungu; wasiwe wachongezi, au watumwa wa pombe. Wanapaswa kufundisha mambo mema,
3Niisamuti käitugu vanad naised pühalikult: ärgu olgu keelepeksjad, ärgu orjaku liigselt veini, vaid õpetagu head,
4ili wawazoeze kina mama vijana kuwapenda waume zao na watoto,
4et nad suudaksid mõistlikult juhatada noori naisi armastama mehi ja lapsi.
5wawe na kiasi na safi, waangalie vizuri mambo ya nyumbani, na wawatii waume zao, ili ujumbe wa Mungu usije ukadharauliwa.
5Nad peavad olema mõõdukad, puhta meelega, virgad majatalituses, head, alistunud oma meestele, et Jumala sõna ei teotataks.
6Kadhalika, wahimize vijana wawe na kiasi.
6Niisamuti manitse nooremaid mehi olema mõõdukad igas suhtes,
7Katika mambo yote wewe mwenyewe unapaswa kuwa mfano wa matendo mema. Uwe mnyofu na uwe na uzito katika mafundisho yako.
7näidates iseennast heade tegude eeskujuna ja pakkudes rikkumatut, väärikat õpetust,
8Maneno yako yasiwe na hitilafu yoyote ili adui zako waaibike wasipopata chochote kibaya cha kusema juu yetu.
8tervet vastuvaidlematut sõna, et vastane häbeneks, kui tal pole meist rääkida midagi halba.
9Watumwa wanapaswa kuwatii wakuu wao na kuwapendeza katika mambo yote. Wasibishane nao,
9Orjad alistugu oma peremeestele kõiges, olgu nende meele järgi, ärgu rääkigu vastu,
10au kuiba vitu vyao. Badala yake wanapaswa kuonyesha kwamba wao ni wema na waaminifu daima, ili, kwa matendo yao yote, wayapatie sifa njema mafundisho juu ya Mungu, Mwokozi wetu.
10ärgu näpaku, vaid osutagu kõigiti ustavust, et nad ehiksid igati Jumala, meie Päästja õpetust.
11Maana neema ya Mungu imedhihirishwa kwa ajili ya wokovu wa watu wote.
11Jah, Jumala arm on ilmunud päästvana kõigile inimestele
12Neema hiyo yatufunza kuachana na uovu wote na tamaa za kidunia; tuwe na kiasi, tuishi maisha adili na ya kumcha Mungu katika ulimwengu huu wa sasa,
12ja kasvatab meid, et me, öeldes lahti jumalakartmatusest ja ilmalikest himudest, elaksime praegusel ajal mõõdukalt ja õiglaselt ja jumalakartlikult,
13tukiwa tunangojea siku ile ya heri tunayoitumainia, wakati utakapotokea utukufu wa Mungu Mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo.
13oodates õndsa lootuse täitumist ning suure Jumala ja meie Päästja Jeesuse Kristuse kirkuse ilmumist.
14Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe kutoka katika uovu wote na kutufanya watu safi walio wake yeye mwenyewe, watu walio na hamu ya kutenda mema.
14Tema on loovutanud iseenda meie eest, et meid lunastada kõigest ülekohtust ja puhastada endale pärisrahvaks, innukaks headele tegudele.
15Basi, fundisha mambo hayo na tumia mamlaka yako yote ukiwahimiza na kuwaonya wasikilizaji wako. Mtu yeyote na asikudharau.
15Seda räägi ja manitse ning veena nõudlikult! Ükski ärgu alahinnaku sind!