1Hatimaye, ndugu zangu, mmejifunza kutoka kwetu namna mnavyopaswa kuishi ili kumpendeza Mungu. Na kweli mmekuwa mnaishi hivyo. Sasa tunawaombeni na kuwasihi kwa jina la Bwana Yesu mfanye vema zaidi.
1Finally then, brothers, we beg and exhort you in the Lord Jesus, that as you received from us how you ought to walk and to please God, that you abound more and more.
2Maana mnayajua yale maagizo tuliyowapeni kwa mamlaka ya Bwana Yesu.
2For you know what instructions we gave you through the Lord Jesus.
3Mungu anataka ninyi muwe watakatifu na mjiepushe kabisa na maisha ya zinaa.
3For this is the will of God: your sanctification, that you abstain from sexual immorality,
4Kila mwanamume anapaswa kujua namna ya kuishi na mkewe kwa utakatifu na heshima,
4that each one of you know how to possess himself of his own vessel in sanctification and honor,
5na si kwa tamaa mbaya kama watu wa mataifa mengine wasiomjua Mungu.
5not in the passion of lust, even as the Gentiles who don’t know God;
6Basi, mtu yeyote asimkosee au kumpunja mwenzake kuhusu jambo hili. Tulikwisha waambieni hayo na kuwaonya kwamba Bwana atawaadhibu wanaofanya mambo hayo.
6that no one should take advantage of and wrong a brother or sister in this matter; because the Lord is an avenger in all these things, as also we forewarned you and testified.
7Mungu hakutuita tuishi maisha ya zinaa, bali tuishi katika utakatifu.
7For God called us not for uncleanness, but in sanctification.
8Kwa hiyo basi, anayedharau mafundisho hayo hamdharau mtu, bali amdharau Mungu mwenyewe anayewapeni Roho wake Mtakatifu.
8Therefore he who rejects this doesn’t reject man, but God, who has also given his Holy Spirit to you.
9Hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya kuwapenda ndugu zenu waumini. Ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu namna mnavyopaswa kupendana.
9But concerning brotherly love, you have no need that one write to you. For you yourselves are taught by God to love one another,
10Na mmekuwa mkiwatendea hivyo ndugu zenu wote kila mahali katika Makedonia. Basi, ndugu tunawaombeni mfanye hata zaidi.
10for indeed you do it toward all the brothers who are in all Macedonia. But we exhort you, brothers, that you abound more and more;
11Muwe na nia ya kuishi maisha ya utulivu, kila mmoja ashughulikie mambo yake mwenyewe na afanye kazi kwa mikono yake mwenyewe kama tulivyowaagiza pale awali.
11and that you make it your ambition to lead a quiet life, and to do your own business, and to work with your own hands, even as we instructed you;
12Kwa namna hiyo mtajipatia sifa nzuri kutoka kwa wale wasio Wakristo, na hamtakuwa na lazima ya kuwategemea wengine kwa mahitaji yenu.
12that you may walk properly toward those who are outside, and may have need of nothing.
13Ndugu, twataka mjue ukweli kuhusu wale ambao wamekwisha fariki dunia, ili msipatwe na huzuni kama watu wengine wasio na matumaini.
13But we don’t want you to be ignorant, brothers, concerning those who have fallen asleep, so that you don’t grieve like the rest, who have no hope.
14Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.
14For if we believe that Jesus died and rose again, even so God will bring with him those who have fallen asleep in Jesus.
15Hili tunalowaambieni ni fundisho la Bwana; sisi tulio hai, ambao tutakuwa tumebaki, wakati Bwana atakapokuja, hakika hatutawatangulia wale waliokwisha fariki dunia.
15For this we tell you by the word of the Lord, that we who are alive, who are left to the coming of the Lord, will in no way precede those who have fallen asleep.
16Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza.
16For the Lord himself will descend from heaven with a shout, with the voice of the archangel, and with God’s trumpet. The dead in Christ will rise first,
17Kisha sisi tulio hai wakati huo tutakusanywa pamoja nao katika mawingu kumlaki Bwana hewani. Na hivyo tutakuwa daima pamoja na Bwana.
17then we who are alive, who are left, will be caught up together with them in the clouds, to meet the Lord in the air. So we will be with the Lord forever.
18Basi, farijianeni kwa maneno haya.
18Therefore comfort one another with these words.