1"Nimewaambieni hayo kusudi msiiache imani yenu.
1 “These things have I spoken to you, so that you wouldn’t be caused to stumble.
2Watu watawatenga ninyi na masunagogi yao. Tena, wakati unakuja ambapo kila atakayewaua ninyi atadhani anamhudumia Mungu.
2 They will put you out of the synagogues. Yes, the time comes that whoever kills you will think that he offers service to God.
3Watawatendeeni mambo hayo kwa sababu hawamjui Baba, wala hawanijui mimi.
3 They will do these things TR adds “to you” because they have not known the Father, nor me.
4Basi, nimewaambieni mambo haya ili saa yake itakapofika mkumbuke kwamba niliwaambieni. "Sikuwaambieni mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.
4 But I have told you these things, so that when the time comes, you may remember that I told you about them. I didn’t tell you these things from the beginning, because I was with you.
5Lakini sasa namwendea yule aliyenituma; na hakuna hata mmoja wenu anayeniuliza: Unakwenda wapi?
5 But now I am going to him who sent me, and none of you asks me, ‘Where are you going?’
6Kwa kuwa nimewaambieni mambo hayo mmejaa huzuni mioyoni mwenu.
6 But because I have told you these things, sorrow has filled your heart.
7Lakini, nawaambieni ukweli: afadhali kwenu mimi niende zangu, maana nisipokwenda Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda, basi, nitamtuma kwenu.
7 Nevertheless I tell you the truth: It is to your advantage that I go away, for if I don’t go away, the Counselor won’t come to you. But if I go, I will send him to you.
8Naye atakapokuja atawathibitishia walimwengu kwamba wamekosea kuhusu dhambi, uadilifu na hukumu ya Mungu.
8 When he has come, he will convict the world about sin, about righteousness, and about judgment;
9Wamekosea kuhusu dhambi kwa sababu hawaniamini;
9 about sin, because they don’t believe in me;
10kuhusu uadilifu, kwa sababu naenda zangu kwa Baba, nanyi hamtaniona tena;
10 about righteousness, because I am going to my Father, and you won’t see me any more;
11kuhusu hukumu kwa sababu mkuu wa ulimwengu huu amekwisha hukumiwa.
11 about judgment, because the prince of this world has been judged.
12"Ninayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili.
12 “I have yet many things to tell you, but you can’t bear them now.
13Lakini atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza kwenye ukweli wote; maana hatasema kwa mamlaka yake mwenyewe, bali atawaambieni yote atakayosikia, na atasema mambo yatakayokuwa yanakuja.
13 However when he, the Spirit of truth, has come, he will guide you into all truth, for he will not speak from himself; but whatever he hears, he will speak. He will declare to you things that are coming.
14Yeye atanitukuza mimi kwa kuwa atawaambieni yale atakayopata kutoka kwangu.
14 He will glorify me, for he will take from what is mine, and will declare it to you.
15Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu; ndiyo maana nimesema kwamba huyo Roho Mtakatifu atawaambieni yale atakayopata kutoka kwangu.
15 All things whatever the Father has are mine; therefore I said that he takes TR reads “will take” instead of “takes” of mine, and will declare it to you.
16"Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona!"
16 A little while, and you will not see me. Again a little while, and you will see me.”
17Hapo baadhi ya wanafunzi wake wakaulizana, "Ana maana gani anapotwambia: Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona? Tena anasema: Kwa kuwa ninakwenda kwa Baba!"
17Some of his disciples therefore said to one another, “What is this that he says to us, ‘A little while, and you won’t see me, and again a little while, and you will see me;’ and, ‘Because I go to the Father?’ ”
18Basi, wakawa wanaulizana, "Ana maana gani anaposema: Bado kitambo kidogo? Hatuelewi anaongelea nini."
18They said therefore, “What is this that he says, ‘A little while?’ We don’t know what he is saying.”
19Yesu alijua kwamba walitaka kumwuliza, basi akawaambia, "Je, mnaulizana juu ya yale niliyosema: Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona?
19Therefore Jesus perceived that they wanted to ask him, and he said to them, “Do you inquire among yourselves concerning this, that I said, ‘A little while, and you won’t see me, and again a little while, and you will see me?’
20Nawaambieni kweli, ninyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi: mtaona huzuni lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.
20 Most certainly I tell you, that you will weep and lament, but the world will rejoice. You will be sorrowful, but your sorrow will be turned into joy.
21Wakati mama anapojifungua huona huzuni kwa sababu saa ya maumivu imefika; lakini akisha jifungua hayakumbuki tena maumivu hayo kwa sababu ya furaha kwamba mtu amezaliwa duniani.
21 A woman, when she gives birth, has sorrow, because her time has come. But when she has delivered the child, she doesn’t remember the anguish any more, for the joy that a human being is born into the world.
22Ninyi pia mna huzuni sasa; lakini nitawajieni tena, nanyi mtajaa furaha mioyoni mwenu, na furaha hiyo hakuna mtu atakayeiondoa kwenu.
22 Therefore you now have sorrow, but I will see you again, and your heart will rejoice, and no one will take your joy away from you.
23Siku hiyo hamtaniomba chochote. Kweli nawaambieni, chochote mtakachomwomba Baba kwa jina langu, atawapeni.
23 “In that day you will ask me no questions. Most certainly I tell you, whatever you may ask of the Father in my name, he will give it to you.
24Mpaka sasa hamjaomba chochote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu ikamilike.
24 Until now, you have asked nothing in my name. Ask, and you will receive, that your joy may be made full.
25"Nimewaambieni mambo hayo kwa mafumbo. Lakini wakati utakuja ambapo sitasema tena nanyi kwa mafumbo, bali nitawaambieni waziwazi juu ya Baba.
25 I have spoken these things to you in figures of speech. But the time is coming when I will no more speak to you in figures of speech, but will tell you plainly about the Father.
26Siku hiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambii kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu;
26 In that day you will ask in my name; and I don’t say to you, that I will pray to the Father for you,
27maana yeye mwenyewe anawapenda ninyi, kwa sababu ninyi mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Mungu.
27 for the Father himself loves you, because you have loved me, and have believed that I came forth from God.
28Mimi nilitoka kwa Baba, nikaja ulimwenguni; na sasa nauacha ulimwengu na kurudi kwa Baba."
28 I came out from the Father, and have come into the world. Again, I leave the world, and go to the Father.”
29Basi, wanafunzi wake wakamwambia, "Ahaa! Sasa unasema waziwazi kabisa bila kutumia mafumbo.
29His disciples said to him, “Behold, now you speak plainly, and speak no figures of speech.
30Sasa tunajua kwamba wewe unajua kila kitu, na huna haja ya kuulizwa maswali na mtu yeyote; kwa hiyo tunaamini kwamba umetoka kwa Mungu."
30Now we know that you know all things, and don’t need for anyone to question you. By this we believe that you came forth from God.”
31Yesu akawajibu, "Je, mnaamini sasa?
31Jesus answered them, “Do you now believe?
32Wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo ninyi nyote mtatawanyika kila mtu kwake, nami nitaachwa peke yangu. Kumbe, lakini mimi siko peke yangu, maana Baba yu pamoja nami.
32 Behold, the time is coming, yes, and has now come, that you will be scattered, everyone to his own place, and you will leave me alone. Yet I am not alone, because the Father is with me.
33Nimewaambieni mambo haya ili mpate kuwa na amani katika kuungana nami. Ulimwenguni mtapata masumbuko; lakini jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu!"
33 I have told you these things, that in me you may have peace. In the world you have oppression; but cheer up! I have overcome the world.”