Swahili: New Testament

World English Bible

Matthew

26

1Yesu alipomaliza kusema hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake,
1It happened, when Jesus had finished all these words, that he said to his disciples,
2"Mnajua kwamba baada ya siku mbili tutakuwa na sikukuu ya Pasaka, na Mwana wa Mtu atatolewa ili asulubiwe."
2 “You know that after two days the Passover is coming, and the Son of Man will be delivered up to be crucified.”
3Wakati huo makuhani wakuu na wazee wa watu walikutana pamoja katika ukumbi wa Kayafa, Kuhani Mkuu.
3Then the chief priests, the scribes, and the elders of the people were gathered together in the court of the high priest, who was called Caiaphas.
4Wakashauriana jinsi ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue.
4They took counsel together that they might take Jesus by deceit, and kill him.
5Lakini wakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wa sikukuu, kusije kukatokea ghasia kati ya watu.
5But they said, “Not during the feast, lest a riot occur among the people.”
6Yesu alipokuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni, aitwaye Mkoma,
6Now when Jesus was in Bethany, in the house of Simon the leper,
7mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya thamani kubwa, alimjia pale mezani alipokuwa amekaa kula chakula, akammiminia hayo marashi kichwani.
7a woman came to him having an alabaster jar of very expensive ointment, and she poured it on his head as he sat at the table.
8Wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, "Ya nini hasara hii?
8But when his disciples saw this, they were indignant, saying, “Why this waste?
9Marashi haya yangaliweza kuuzwa kwa bei kubwa, maskini wakapewa hizo fedha."
9For this ointment might have been sold for much, and given to the poor.”
10Yesu alitambua mawazo yao, akawaambia, "Mbona mnamsumbua huyu mama? Yeye amenitendea jambo jema.
10However, knowing this, Jesus said to them, “Why do you trouble the woman? Because she has done a good work for me.
11Maskini mnao daima pamoja nanyi, lakini mimi sitakuwapo pamoja nanyi daima.
11 For you always have the poor with you; but you don’t always have me.
12Huyu mama amenimiminia marashi ili kunitayarisha kwa maziko.
12 For in pouring this ointment on my body, she did it to prepare me for burial.
13Nawaambieni kweli, popote ambapo hii Habari Njema itahubiriwa ulimwenguni, kitendo hiki alichofanya mama huyu kitatajwa kwa kumkumbuka yeye."
13 Most certainly I tell you, wherever this Good News is preached in the whole world, what this woman has done will also be spoken of as a memorial of her.”
14Kisha, Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili, akaenda kwa makuhani wakuu,
14Then one of the twelve, who was called Judas Iscariot, went to the chief priests,
15akawaambia, "Mtanipa kitu gani kama nikimkabidhi Yesu kwenu?" Wakamhesabia sarafu thelathini za fedha;
15and said, “What are you willing to give me, that I should deliver him to you?” They weighed out for him thirty pieces of silver.
16na tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta nafasi ya kumsaliti.
16From that time he sought opportunity to betray him.
17Siku ya kwanza kabla ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wanafunzi walimwendea Yesu wakamwuliza, "Unataka tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?"
17Now on the first day of unleavened bread, the disciples came to Jesus, saying to him, “Where do you want us to prepare for you to eat the Passover?”
18Yeye akawajibu, "Nendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie: Mwalimu anasema, wakati wangu umefika; kwako nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu."
18He said, “Go into the city to a certain person, and tell him, ‘The Teacher says, “My time is at hand. I will keep the Passover at your house with my disciples.”’”
19Wanafunzi wakafanya kama Yesu alivyowaagiza, wakaandaa Pasaka.
19The disciples did as Jesus commanded them, and they prepared the Passover.
20Kulipokuwa jioni, Yesu akakaa mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili.
20Now when evening had come, he was reclining at the table with the twelve disciples.
21Walipokuwa wakila, Yesu akasema, "Nawaambieni kweli, mmoja wenu atanisaliti."
21As they were eating, he said, “Most certainly I tell you that one of you will betray me.”
22Wanafunzi wakahuzunika sana, wakaanza kuuliza mmojammoja, "Bwana! Je, ni mimi?"
22They were exceedingly sorrowful, and each began to ask him, “It isn’t me, is it, Lord?”
23Yesu akajibu, "Atakayechovya mkate pamoja nami katika bakuli ndiye atakayenisaliti.
23He answered, “He who dipped his hand with me in the dish, the same will betray me.
24Naam, Mwana wa Mtu anakwenda zake kama Maandiko Matakatifu yasemavyo, lakini ole wake mtu yule atakayemsaliti Mwana wa Mtu! Ingalikuwa afadhali kwa mtu huyo kama hangalizaliwa."
24 The Son of Man goes, even as it is written of him, but woe to that man through whom the Son of Man is betrayed! It would be better for that man if he had not been born.”
25Yuda, ambaye ndiye aliyetaka kumsaliti, akamwuliza, "Mwalimu! Je, ni mimi?" Yesu akamjibu, "Wewe umesema."
25Judas, who betrayed him, answered, “It isn’t me, is it, Rabbi?” He said to him, “You said it.”
26Walipokuwa wanakula, Yesu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema, "Twaeni mle; huu ni mwili wangu."
26As they were eating, Jesus took bread, gave thanks for it, and broke it. He gave to the disciples, and said, “Take, eat; this is my body.”
27Kisha akatwaa kikombe, akamshukuru Mungu, akawapa akisema, "Nyweni nyote;
27He took the cup, gave thanks, and gave to them, saying, “All of you drink it,
28maana hii ni damu yangu inayothibitisha agano, damu inayomwagwa kwa ajili ya watu wengi ili kuwaondolea dhambi.
28 for this is my blood of the new covenant, which is poured out for many for the remission of sins.
29Nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka siku ile nitakapoinywa mpya pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba yangu."
29 But I tell you that I will not drink of this fruit of the vine from now on, until that day when I drink it anew with you in my Father’s Kingdom.”
30Baada ya kuimba wimbo, wakaondoka, wakaenda katika mlima wa Mizeituni.
30When they had sung a hymn, they went out to the Mount of Olives.
31Kisha Yesu akawaambia, "Usiku huu wa leo, ninyi nyote mtakuwa na mashaka nami, maana Maandiko Matakatifu yasema: Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika.
31Then Jesus said to them, “All of you will be made to stumble because of me tonight, for it is written, ‘I will strike the shepherd, and the sheep of the flock will be scattered.’
32Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulieni Galilaya."
32 But after I am raised up, I will go before you into Galilee.”
33Petro akamwambia Yesu "Hata kama wote watakuwa na mashaka nawe na kukuacha, mimi sitakuacha kamwe."
33But Peter answered him, “Even if all will be made to stumble because of you, I will never be made to stumble.”
34Yesu akamwambia, "Kweli nakwambia, usiku huu kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu."
34Jesus said to him, “Most certainly I tell you that tonight, before the rooster crows, you will deny me three times.”
35Petro akamwambia, "Hata kama ni lazima nife pamoja nawe, sitakukana kamwe." Wale wanafunzi wengine wote wakasema vivyo hivyo.
35Peter said to him, “Even if I must die with you, I will not deny you.” All of the disciples also said likewise.
36Kisha Yesu akaenda pamoja nao bustanini Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, "Kaeni hapa nami niende pale mbele kusali."
36Then Jesus came with them to a place called Gethsemane, and said to his disciples, “Sit here, while I go there and pray.”
37Akawachukua Petro na wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuwa na huzuni na mahangaiko.
37He took with him Peter and the two sons of Zebedee, and began to be sorrowful and severely troubled.
38Hapo akawaambia, "Nina huzuni kubwa moyoni hata karibu kufa. Kaeni hapa mkeshe pamoja nami."
38Then he said to them, “My soul is exceedingly sorrowful, even to death. Stay here, and watch with me.”
39Basi, akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akasali: "Baba yangu, kama inawezekana, aacha kikombe hiki cha mateso kinipite; lakini isiwe nitakavyo mimi, ila utakavyo wewe."
39He went forward a little, fell on his face, and prayed, saying, “My Father, if it is possible, let this cup pass away from me; nevertheless, not what I desire, but what you desire.”
40Akawaendea wale wanafunzi, akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, "Ndiyo kusema hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?
40He came to the disciples, and found them sleeping, and said to Peter, “What, couldn’t you watch with me for one hour?
41Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho i tayari lakini mwili ni dhaifu."
41 Watch and pray, that you don’t enter into temptation. The spirit indeed is willing, but the flesh is weak.”
42Akaenda tena mara ya pili akasali: "Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kinipite bila mimi kukinywa, basi, mapenzi yako yafanyike."
42Again, a second time he went away, and prayed, saying, “My Father, if this cup can’t pass away from me unless I drink it, your desire be done.”
43Akawaendea tena, akawakuta wamelala, maana macho yao yalikuwa yamebanwa na usingizi.
43He came again and found them sleeping, for their eyes were heavy.
44Basi, akawaacha, akaenda tena kusali mara ya tatu kwa maneno yaleyale.
44He left them again, went away, and prayed a third time, saying the same words.
45Kisha akawaendea wale wanafunzi, akawaambia, "Je, mngali mmelala na kupumzika? Tazameni! Saa yenyewe imefika, na Mwana wa Mtu atatolewa kwa watu wenye dhambi.
45Then he came to his disciples, and said to them, “Sleep on now, and take your rest. Behold, the hour is at hand, and the Son of Man is betrayed into the hands of sinners.
46Amkeni, twendeni zetu. Tazameni! Anakuja yule atakayenisaliti."
46 Arise, let’s be going. Behold, he who betrays me is at hand.”
47Basi, Yesu alipokuwa bado anasema nao, mara akaja Yuda, mmoja wa wale kumi na wawili. Pamoja naye walikuja watu wengi wenye mapanga na marungu ambao walitumwa na makuhani wakuu na wazee wa watu.
47While he was still speaking, behold, Judas, one of the twelve, came, and with him a great multitude with swords and clubs, from the chief priest and elders of the people.
48Huyo aliyetaka kumsaliti Yesu, alikuwa amekwisha wapa ishara akisema: "Yule nitakayembusu ndiye; mkamateni."
48Now he who betrayed him gave them a sign, saying, “Whoever I kiss, he is the one. Seize him.”
49Basi, Yuda akamkaribia Yesu, akamwambia, "Shikamoo, Mwalimu!" Kisha akambusu.
49Immediately he came to Jesus, and said, “Hail, Rabbi!” and kissed him.
50Yesu akamwambia, "Rafiki, fanya ulichokuja kufanya." Hapo wale watu wakaja, wakamkamata Yesu, wakamtia nguvuni.
50Jesus said to him, “Friend, why are you here?” Then they came and laid hands on Jesus, and took him.
51Mmoja wa wale waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono, akauchomoa upanga wake, akampiga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.
51Behold, one of those who were with Jesus stretched out his hand, and drew his sword, and struck the servant of the high priest, and struck off his ear.
52Hapo Yesu akamwambia, "Rudisha upanga wako alani, maana yeyote anayeutumia upanga, atakufa kwa upanga.
52Then Jesus said to him, “Put your sword back into its place, for all those who take the sword will die by the sword.
53Je, hamjui kwamba ningeweza kumwomba Baba yangu naye mara angeniletea zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?
53 Or do you think that I couldn’t ask my Father, and he would even now send me more than twelve legions of angels?
54Lakini yatatimiaje Maandiko Matakatifu yasemayo kwamba ndivyo inavyopaswa kuwa?"
54 How then would the Scriptures be fulfilled that it must be so?”
55Wakati huohuo Yesu akauambia huo umati wa watu waliokuja kumtia nguvuni, "Je, mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu kama kwamba mimi ni mnyang'anyi? Kila siku nilikuwa Hekaluni nikifundisha, na hamkunikamata!
55In that hour Jesus said to the multitudes, “Have you come out as against a robber with swords and clubs to seize me? I sat daily in the temple teaching, and you didn’t arrest me.
56Lakini haya yote yametendeka ili Maandiko ya manabii yatimie." Kisha wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.
56 But all this has happened, that the Scriptures of the prophets might be fulfilled.” Then all the disciples left him, and fled.
57Basi, hao watu waliomkamata Yesu walimpeleka nyumbani kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, walikokusanyika walimu wa Sheria na wazee.
57Those who had taken Jesus led him away to Caiaphas the high priest, where the scribes and the elders were gathered together.
58Petro alimfuata kwa mbali mpaka uani kwa Kuhani Mkuu, akaingia ndani pamoja na walinzi ili apate kuona mambo yatakavyokuwa.
58But Peter followed him from a distance, to the court of the high priest, and entered in and sat with the officers, to see the end.
59Basi, makuhani wakuu na Baraza lote wakatafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu wapate kumwua,
59Now the chief priests, the elders, and the whole council sought false testimony against Jesus, that they might put him to death;
60lakini hawakupata ushahidi wowote, ingawa walikuja mashahidi wengi wa uongo. Mwishowe wakaja mashahidi wawili,
60and they found none. Even though many false witnesses came forward, they found none. But at last two false witnesses came forward,
61wakasema, "Mtu huyu alisema: Ninaweza kuliharibu Hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu."
61and said, “This man said, ‘I am able to destroy the temple of God, and to build it in three days.’”
62Kuhani Mkuu akasimama, akamwuliza Yesu, "Je, hujibu neno? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?"
62The high priest stood up, and said to him, “Have you no answer? What is this that these testify against you?”
63Lakini Yesu akakaa kimya. Kuhani Mkuu akamwambia, "Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, twambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu!"
63But Jesus held his peace. The high priest answered him, “I adjure you by the living God, that you tell us whether you are the Christ, the Son of God.”
64Yesu akamwambia, "Wewe umesema! Lakini nawaambieni, tangu sasa mtamwona Mwana wa Mtu ameketi upande wa kulia wa Mwenyezi, akija juu ya mawingu ya mbinguni."
64Jesus said to him, “You have said it. Nevertheless, I tell you, after this you will see the Son of Man sitting at the right hand of Power, and coming on the clouds of the sky.”
65Hapo, Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akasema, "Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi? Sasa mmesikia kufuru yake.
65Then the high priest tore his clothing, saying, “He has spoken blasphemy! Why do we need any more witnesses? Behold, now you have heard his blasphemy.
66Ninyi mwaonaje?" Wao wakamjibu, "Anastahili kufa!"
66What do you think?” They answered, “He is worthy of death!”
67Kisha wakamtemea mate usoni, wakampiga makofi. Wengine wakiwa wanampiga makofi,
67Then they spit in his face and beat him with their fists, and some slapped him,
68wakasema, "Haya Kristo, tutabirie; ni nani amekupiga!"
68saying, “Prophesy to us, you Christ! Who hit you?”
69Petro alikuwa ameketi nje uani. Basi, mtumishi mmoja wa kike akamwendea, akasema, "Wewe ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya."
69Now Peter was sitting outside in the court, and a maid came to him, saying, “You were also with Jesus, the Galilean!”
70Petro akakana mbele ya wote akisema, "Sijui hata unasema nini."
70But he denied it before them all, saying, “I don’t know what you are talking about.”
71Alipokuwa akitoka mlangoni, mtumishi mwingine wa kike akamwona, akawaambia wale waliokuwa pale, "Mtu huyu alikuwa pamoja na Yesu wa Nazareti."
71When he had gone out onto the porch, someone else saw him, and said to those who were there, “This man also was with Jesus of Nazareth.”
72Petro akakana tena kwa kiapo: "Simjui mtu huyo."
72Again he denied it with an oath, “I don’t know the man.”
73Baadaye kidogo, watu waliokuwa pale wakamwendea Petro, wakamwambia, "Hakika, wewe pia ni mmoja wao, maana msemo wako unakutambulisha."
73After a little while those who stood by came and said to Peter, “Surely you are also one of them, for your speech makes you known.”
74Hapo Petro akaanza kujilaani na kuapa akisema, "Simjui mtu huyo!" Mara jogoo akawika.
74Then he began to curse and to swear, “I don’t know the man!” Immediately the rooster crowed.
75Petro akakumbuka maneno aliyoambiwa na Yesu: "Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu." Basi, akatoka nje akalia sana.
75Peter remembered the word which Jesus had said to him, “Before the rooster crows, you will deny me three times.” He went out and wept bitterly.