Swahili: New Testament

World English Bible

Matthew

27

1Kulipopambazuka, makuhani wakuu wote na wazee wa watu walifanya mashauri juu ya Yesu wapate kumwua.
1Now when morning had come, all the chief priests and the elders of the people took counsel against Jesus to put him to death:
2Wakamfunga pingu, wakamchukua, wakamkabidhi kwa Pilato, mkuu wa mkoa.
2and they bound him, and led him away, and delivered him up to Pontius Pilate, the governor.
3Hapo, Yuda ambaye ndiye aliyemsaliti, alipoona kwamba wamekwisha mhukumu Yesu, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu zile sarafu thelathini za fedha.
3Then Judas, who betrayed him, when he saw that Jesus was condemned, felt remorse, and brought back the thirty pieces of silver to the chief priests and elders,
4Akawaambia, "Nimekosa kwa kumtoa mtu asiye na hatia auawe." Lakini wao wakasema, "Yatuhusu nini sisi? Hilo ni shauri lako."
4saying, “I have sinned in that I betrayed innocent blood.” But they said, “What is that to us? You see to it.”
5Naye akazitupa zile fedha Hekaluni, akatoka nje, akaenda akajinyonga.
5He threw down the pieces of silver in the sanctuary, and departed. He went away and hanged himself.
6Makuhani wakuu wakazichukua zile fedha, wakasema, "Haifai kuziweka katika hazina ya Hekalu kwa maana ni fedha za damu."
6The chief priests took the pieces of silver, and said, “It’s not lawful to put them into the treasury, since it is the price of blood.”
7Basi, wakashauriana, wakazitumia kununua shamba la mfinyanzi liwe mahali pa kuzika wageni.
7They took counsel, and bought the potter’s field with them, to bury strangers in.
8Ndiyo maana mpaka leo shamba hilo linaitwa Shamba la Damu.
8Therefore that field was called “The Field of Blood” to this day.
9Hivyo maneno ya nabii Yeremia yakatimia: "Walizichukua sarafu thelathini za fedha, thamani ya yule ambaye watu wa Israeli walipanga bei,
9Then that which was spoken through Jeremiah the prophet was fulfilled, saying, “They took the thirty pieces of silver, the price of him upon whom a price had been set, whom some of the children of Israel priced,
10wakanunua nazo shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniagiza."
10and they gave them for the potter’s field, as the Lord commanded me.”
11Yesu alisimamishwa mbele ya mkuu wa mkoa. Basi, mkuu wa mkoa akamwuliza, "Je, wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?" Yesu akamwambia, "Wewe umesema."
11Now Jesus stood before the governor: and the governor asked him, saying, “Are you the King of the Jews?” Jesus said to him, “So you say.”
12Lakini makuhani wakuu na wazee walipokuwa wanamshtaki, hakujibu neno.
12When he was accused by the chief priests and elders, he answered nothing.
13Hivyo Pilato akamwuliza, "Je, husikii mashtaka hayo yote wanayotoa juu yako?"
13Then Pilate said to him, “Don’t you hear how many things they testify against you?”
14Lakini Yesu hakumjibu hata neno moja; hata huyo mkuu wa mkoa akashangaa sana.
14He gave him no answer, not even one word, so that the governor marveled greatly.
15Ilikuwa kawaida wakati wa Sikukuu ya Pasaka mkuu wa mkoa kuwafungulia Wayahudi mfungwa mmoja waliyemtaka.
15Now at the feast the governor was accustomed to release to the multitude one prisoner, whom they desired.
16Wakati huo kulikuwa na mfungwa mmoja, jina lake Baraba.
16They had then a notable prisoner, called Barabbas.
17Hivyo, watu walipokusanyika pamoja, Pilato akawauliza, "Mwataka nimfungue yupi kati ya wawili hawa, Baraba ama Yesu aitwae Kristo?"
17When therefore they were gathered together, Pilate said to them, “Whom do you want me to release to you? Barabbas, or Jesus, who is called Christ?”
18Alisema hivyo maana alijua wazi kwamba walimleta kwake kwa sababu ya wivu.
18For he knew that because of envy they had delivered him up.
19Pilato alipokuwa amekaa katika kiti cha hukumu, mke wake akampelekea ujumbe: "Usijitie katika shauri la mtu huyu mwema, maana leo nimeteseka sana katika ndoto kwa sababu yake."
19While he was sitting on the judgment seat, his wife sent to him, saying, “Have nothing to do with that righteous man, for I have suffered many things this day in a dream because of him.”
20Lakini makuhani wakuu na wazee wakawashawishi watu waombe Baraba afunguliwe na Yesu auawe.
20Now the chief priests and the elders persuaded the multitudes to ask for Barabbas, and destroy Jesus.
21Mkuu wa mkoa akawauliza, "Ni yupi kati ya hawa wawili mnayetaka nimfungue?" Wakamjibu, "Baraba!"
21But the governor answered them, “Which of the two do you want me to release to you?” They said, “Barabbas!”
22Pilato akawauliza, "Sasa, nifanye nini na Yesu aitwaye Kristo?" Wote wakasema, "Asulubiwe!"
22Pilate said to them, “What then shall I do to Jesus, who is called Christ?” They all said to him, “Let him be crucified!”
23Pilato akauliza, "Kwa nini? Amefanya kosa gani?" Wao wakazidi kupaaza sauti: "Asulubiwe!"
23But the governor said, “Why? What evil has he done?” But they cried out exceedingly, saying, “Let him be crucified!”
24Basi, Pilato alipotambua kwamba hafanikiwi chochote na kwamba maasi yalikuwa yanaanza, alichukua maji, akanawa mikono mbele ya ule umati wa watu, akasema, "Mimi sina lawama juu ya kifo cha mtu huyu; shauri lenu wenyewe."
24So when Pilate saw that nothing was being gained, but rather that a disturbance was starting, he took water, and washed his hands before the multitude, saying, “I am innocent of the blood of this righteous person. You see to it.”
25Watu wote wakasema, "Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!"
25All the people answered, “May his blood be on us, and on our children!”
26Hapo Pilato akawafungulia Baraba kutoka gerezani, lakini akamtoa Yesu asulubiwe.
26Then he released to them Barabbas, but Jesus he flogged and delivered to be crucified.
27Kisha askari wa mkuu wa mkoa wakamwingiza Yesu ndani ya ikulu, wakamkusanyikia kikosi kizima.
27Then the governor’s soldiers took Jesus into the Praetorium, and gathered the whole garrison together against him.
28Wakamvua nguo zake, wakamvika joho la rangi nyekundu.
28They stripped him, and put a scarlet robe on him.
29Kisha wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani, wakamwekea pia mwanzi katika mkono wake wa kulia. Wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki wakisema, "Shikamoo mfalme wa Wayahudi!"
29They braided a crown of thorns and put it on his head, and a reed in his right hand; and they kneeled down before him, and mocked him, saying, “Hail, King of the Jews!”
30Wakamtemea mate, wakauchukua ule mwanzi, wakampiga nao kichwani.
30They spat on him, and took the reed and struck him on the head.
31Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
31When they had mocked him, they took the robe off of him, and put his clothes on him, and led him away to crucify him.
32Walipokuwa wakienda, wakamkuta mtu mmoja jina lake Simoni, mwenyeji wa Kurene, wakamlazimisha kuuchukua msalaba wake Yesu.
32As they came out, they found a man of Cyrene, Simon by name, and they compelled him to go with them, that he might carry his cross.
33Walipofika mahali paitwapo Golgotha, maana yake, "Mahali pa Fuvu la kichwa,"
33They came to a place called “Golgotha,” that is to say, “The place of a skull.”
34wakampa mchanganyiko wa divai na nyongo. Lakini Yesu alipoonja akakataa kunywa.
34They gave him sour wine to drink mixed with gall. When he had tasted it, he would not drink.
35Walimsulubisha, kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
35When they had crucified him, they divided his clothing among them, casting lots,
36Wakaketi, wakawa wanamchunga.
36and they sat and watched him there.
37Juu ya kichwa chake wakaweka shtaka dhidi yake lilioandikwa, "Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi."
37They set up over his head the accusation against him written, “THIS IS JESUS, THE KING OF THE JEWS.”
38Wanyang'anyi wawili walisulubishwa pia pamoja naye, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia.
38Then there were two robbers crucified with him, one on his right hand and one on the left.
39Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana wakitikisa vichwa vyao na kusema,
39Those who passed by blasphemed him, wagging their heads,
40"Wewe! Si ulijidai kulivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu? Sasa jiokoe mwenyewe. Kama wewe ni Mwana wa Mungu, basi shuka msalabani!"
40and saying, “You who destroy the temple, and build it in three days, save yourself! If you are the Son of God, come down from the cross!”
41Hali kadhalika na makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria na wazee walimdhihaki wakisema,
41Likewise the chief priests also mocking, with the scribes, the Pharisees, and the elders, said,
42"Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi! Eti yeye ni mfalme wa Wayahudi! Basi, sasa na ashuke msalabani, nasi tutamwamini.
42“He saved others, but he can’t save himself. If he is the King of Israel, let him come down from the cross now, and we will believe in him.
43Alimtumainia Mungu na kusema eti yeye ni Mwana wa Mungu; basi, Mungu na amwokoe kama anamtaka."
43He trusts in God. Let God deliver him now, if he wants him; for he said, ‘I am the Son of God.’”
44Hali kadhalika na wale waliosulubiwa pamoja naye wakamtukana.
44The robbers also who were crucified with him cast on him the same reproach.
45Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi yote ikawa katika giza.
45Now from the sixth hour there was darkness over all the land until the ninth hour.
46Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kubwa, "Eli, Eli, lema sabakthani?" Maana yake, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?"
46About the ninth hour Jesus cried with a loud voice, saying, “Eli, Eli, lima sabachthani?” That is, “My God, my God, why have you forsaken me?”
47Lakini wale waliosimama pale waliposikia hivyo wakasema, "Anamwita Eliya."
47Some of them who stood there, when they heard it, said, “This man is calling Elijah.”
48Mmoja wao akakimbia, akachukua sifongo, akaichovya katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe.
48Immediately one of them ran, and took a sponge, and filled it with vinegar, and put it on a reed, and gave him a drink.
49Wengine wakasema, "Acha tuone kama Eliya anakuja kumwokoa."
49The rest said, “Let him be. Let’s see whether Elijah comes to save him.”
50Basi, Yesu akalia tena kwa sauti kubwa, akakata roho.
50Jesus cried again with a loud voice, and yielded up his spirit.
51Hapo pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili, toka juu mpaka chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
51Behold, the veil of the temple was torn in two from the top to the bottom. The earth quaked and the rocks were split.
52makaburi yakafunguka na watu wengi wa Mungu waliokufa wakafufuliwa;
52The tombs were opened, and many bodies of the saints who had fallen asleep were raised;
53nao, baada ya kufufuka kwake, wakatoka makaburini, wakaingia katika Mji Mtakatifu, wakaonekana na watu wengi.
53and coming out of the tombs after his resurrection, they entered into the holy city and appeared to many.
54Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, "Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu."
54Now the centurion, and those who were with him watching Jesus, when they saw the earthquake, and the things that were done, feared exceedingly, saying, “Truly this was the Son of God.”
55Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia.
55Many women were there watching from afar, who had followed Jesus from Galilee, serving him.
56Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo.
56Among them were Mary Magdalene, Mary the mother of James and Joses, and the mother of the sons of Zebedee.
57Ilipokuwa jioni, akaja mtu mmoja tajiri mwenyeji wa Armathaya, jina lake Yosefu. Yeye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.
57When evening had come, a rich man from Arimathaea, named Joseph, who himself was also Jesus’ disciple came.
58Akamwendea Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu. Basi, Pilato akaamuru apewe.
58This man went to Pilate, and asked for Jesus’ body. Then Pilate commanded the body to be given up.
59Yosefu akauchukua ule mwili akauzungushia sanda safi ya kitani,
59Joseph took the body, and wrapped it in a clean linen cloth,
60akauweka ndani ya kaburi lake jipya alilokuwa amelichonga katika mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
60and laid it in his own new tomb, which he had cut out in the rock, and he rolled a great stone to the door of the tomb, and departed.
61Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikuwa wameketi kulielekea kaburi.
61Mary Magdalene was there, and the other Mary, sitting opposite the tomb.
62Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile ya Maandalio, makuhani wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato,
62Now on the next day, which was the day after the Preparation Day, the chief priests and the Pharisees were gathered together to Pilate,
63Wakasema, "Mheshimiwa, tunakumbuka kwamba yule mdanganyifu alisema kabla ya kufa ati, Baada ya siku tatu nitafufuka.
63saying, “Sir, we remember what that deceiver said while he was still alive: ‘After three days I will rise again.’
64Kwa hiyo amuru kaburi lilindwe mpaka siku ya tatu ili wanafunzi wake wasije wakamwiba na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Uongo huu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa awali."
64Command therefore that the tomb be made secure until the third day, lest perhaps his disciples come at night and steal him away, and tell the people, ‘He is risen from the dead;’ and the last deception will be worse than the first.”
65Pilato akawaambia, "Haya, mnao walinzi; nendeni mkalinde kadiri mjuavyo."
65Pilate said to them, “You have a guard. Go, make it as secure as you can.”
66Basi, wakaenda, wakalilinda kaburi, wakatia mhuri juu ya lile jiwe na kuacha hapo askari walinzi.
66So they went with the guard and made the tomb secure, sealing the stone.