World English Bible

Swahili: New Testament

Ephesians

4

1I therefore, the prisoner in the Lord, beg you to walk worthily of the calling with which you were called,
1Basi, mimi niliye mfungwa kwa kuwa namtumikia Bwana, nawasihi muishi maisha yanayostahili wito mlioitiwa.
2with all lowliness and humility, with patience, bearing with one another in love;
2Muwe daima wanyenyekevu, wapole na wenye saburi; vumilianeni ninyi kwa ninyi kwa mapendo.
3being eager to keep the unity of the Spirit in the bond of peace.
3Fanyeni bidii ya kuhifadhi umoja uletwao na Roho kwa kuzingatia amani iliyo kati yenu.
4There is one body, and one Spirit, even as you also were called in one hope of your calling;
4Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile tumaini mliloitiwa na Mungu ni moja.
5one Lord, one faith, one baptism,
5Kuna Bwana mmoja, imani moja na ubatizo mmoja;
6one God and Father of all, who is over all, and through all, and in us all.
6kuna Mungu mmoja na Baba wa wote, ambaye yuko juu ya wote, afanya kazi katika yote na yuko katika yote.
7But to each one of us was the grace given according to the measure of the gift of Christ.
7Kila mmoja wetu amepewa neema kadiri ya kipimo alichojaliwa na Kristo.
8Therefore he says, “When he ascended on high, he led captivity captive, and gave gifts to men.”
8Kama yasemavyo Maandiko: "Alipopaa mbinguni juu kabisa, alichukua mateka; aliwapa watu zawadi."
9Now this, “He ascended,” what is it but that he also first descended into the lower parts of the earth?
9Basi, inaposemwa: "alipaa juu," ina maana gani? Maana yake ni kwamba, kwanza alishuka mpaka chini kabisa duniani.
10He who descended is the one who also ascended far above all the heavens, that he might fill all things.
10Basi, huyo aliyeshuka hapa duniani, ndiye aliyepaa juu ya mbingu zote apate kuujaza ulimwengu.
11He gave some to be apostles; and some, prophets; and some, evangelists; and some, shepherds and teachers;
11Ndiye aliyewapa watu zawadi: wengine aliwajalia wawe mitume, wengine manabii, wengine wawe waeneza Habari Njema, wengine wachungaji na walimu.
12for the perfecting of the saints, to the work of serving, to the building up of the body of Christ;
12Alifanya hivyo apate kuwatayarisha watu wote wa Mungu kwa ajili ya kazi ya huduma ya Kikristo ili kuujenga mwili wa Kristo,
13until we all attain to the unity of the faith, and of the knowledge of the Son of God, to a full grown man, to the measure of the stature of the fullness of Christ;
13na hivyo sote tuufikie umoja wa imani na kumjua Mwana wa Mungu; tuwe watu waliokomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe.
14that we may no longer be children, tossed back and forth and carried about with every wind of doctrine, by the trickery of men, in craftiness, after the wiles of error;
14Basi, hatutakuwa tena kama watoto, tukitupwa na kupeperushwa huko na huko kwa kila upepo wa mafundisho wanayozua watu wadanganyifu, ili wawapotoshe wengine kwa hila.
15but speaking truth in love, we may grow up in all things into him, who is the head, Christ;
15Ila, sisi tukisema ukweli kwa moyo wa mapendo tutakua zidi katika kila jambo kulingana na Kristo ambaye ndiye kichwa;
16from whom all the body, being fitted and knit together through that which every joint supplies, according to the working in measure of each individual part, makes the body increase to the building up of itself in love.
16chini ya uongozi wake, viungo vyote vya mwili hushikamana pamoja, na mwili wote hutegemezwa kwa msaada wa viungo vyake. Basi, kila kiungo kikitekeleza kazi yake ipasavyo, mwili wote hukua na kujijenga katika upendo.
17This I say therefore, and testify in the Lord, that you no longer walk as the rest of the Gentiles also walk, in the futility of their mind,
17Basi, kwa jina la Bwana, nawaonyeni: msiishi tena kama watu wasiomjua Mungu, ambao fikira zao zimekuwa upuuzi mtupu,
18being darkened in their understanding, alienated from the life of God, because of the ignorance that is in them, because of the hardening of their hearts;
18na akili zao zimo gizani. Wako mbali na uzima wa Mungu, kwa sababu ya upumbavu ulio ndani yao na ukaidi wao.
19who having become callous gave themselves up to lust, to work all uncleanness with greediness.
19Wamepotoka na hawana aibu, wamejitosa katika ufisadi; hufanya kwa pupa kila aina ya mambo ya aibu.
20But you did not learn Christ that way;
20Lakini ninyi hamkujifunza hivyo juu ya Kristo.
21if indeed you heard him, and were taught in him, even as truth is in Jesus:
21Ni dhahiri kwamba mlisikia barabara habari zake, na mkiwa wafuasi wake mkafundishwa ukweli ulivyo katika Yesu.
22that you put away, as concerning your former way of life, the old man, that grows corrupt after the lusts of deceit;
22Basi, acheni mwenendo wenu wa awali, yaani ule utu wenu wa kale uliokuwa unaangamizwa kwa tamaa zake danganyifu.
23and that you be renewed in the spirit of your mind,
23Jirekebisheni upya rohoni na katika fikira zenu.
24and put on the new man, who in the likeness of God has been created in righteousness and holiness of truth.
24Vaeni hali mpya ya utu ambayo imeumbwa kwa mfano wa Mungu na ambayo hujionyesha katika maisha ya kweli ya uadilifu na utakatifu.
25Therefore putting away falsehood, speak truth each one with his neighbor. For we are members of one another.
25Kwa hiyo, acheni uongo. Kila mmoja anapaswa kumwambia mwenzake ukweli, maana kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa Kristo.
26“Be angry, and don’t sin.” Don’t let the sun go down on your wrath,
26Kama mkikasirika, msikubali hasira yenu iwafanye mtende dhambi, na wala msikae na hasira kutwa nzima.
27neither give place to the devil.
27Msimpe Ibilisi nafasi.
28Let him who stole steal no more; but rather let him labor, working with his hands the thing that is good, that he may have something to give to him who has need.
28Aliyekuwa akiiba, asiibe tena, bali na aanze kufanya kazi njema kwa mikono yake, apate kuwa na kitu cha kumsaidia mtu aliye maskini.
29Let no corrupt speech proceed out of your mouth, but such as is good for building up as the need may be, that it may give grace to those who hear.
29Maneno mabaya hata yasisikike kamwe miongoni mwenu; kila mara maneno yenu yawe ya kufaa na ambayo hujenga na kuwasaidia wengine, ili yawaneemeshe wasikilizaji wenu.
30Don’t grieve the Holy Spirit of God, in whom you were sealed for the day of redemption.
30Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu maana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenu kwamba ninyi ni watu wake, na thibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu atawakomboeni.
31Let all bitterness, wrath, anger, outcry, and slander, be put away from you, with all malice.
31Basi, achaneni na uhasama, chuki, hasira, kelele, matusi! Achaneni na kila uovu!
32And be kind to one another, tenderhearted, forgiving each other, just as God also in Christ forgave you.
32Muwe na moyo mwema na wenye kuhurumiana; kila mmoja na amsamehe mwenzake kama naye Mungu alivyowasamehe ninyi kwa njia ya Kristo.