World English Bible

Swahili: New Testament

Mark

4

1Again he began to teach by the seaside. A great multitude was gathered to him, so that he entered into a boat in the sea, and sat down. All the multitude were on the land by the sea.
1Yesu alianza kufundisha tena akiwa kando ya ziwa. Umati mkubwa wa watu ulimzunguka hata ikambidi aingie katika mashua na kuketi. Watu wakawa wamekaa katika nchi kavu, kando ya ziwa.
2He taught them many things in parables, and told them in his teaching,
2Aliwafundisha mambo mengi kwa mifano, na katika mafundisho yake aliwaambia,
3 “Listen! Behold, the farmer went out to sow,
3"Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.
4 and it happened, as he sowed, some seed fell by the road, and the birds came and devoured it.
4Alipokuwa akipanda, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.
5 Others fell on the rocky ground, where it had little soil, and immediately it sprang up, because it had no depth of soil.
5Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Mbegu hizo ziliota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina.
6 When the sun had risen, it was scorched; and because it had no root, it withered away.
6Jua lilipochomoza, zikachomeka; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka.
7 Others fell among the thorns, and the thorns grew up, and choked it, and it yielded no fruit.
7Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga, nazo hazikuzaa nafaka.
8 Others fell into the good ground, and yielded fruit, growing up and increasing. Some brought forth thirty times, some sixty times, and some one hundred times as much.”
8Nyingine zilianguka katika udongo mzuri, zikakua na kuzaa: moja punje thelathini, moja sitini na nyingine mia."
9He said, “Whoever has ears to hear, let him hear.”
9Kisha akawaambia, "Mwenye masikio na asikie!"
10When he was alone, those who were around him with the twelve asked him about the parables.
10Yesu alipokuwa peke yake, baadhi ya wale waliomsikia walimwendea pamoja na wale kumi na wawili, wakamwuliza juu ya hiyo mifano.
11He said to them, “To you is given the mystery of the Kingdom of God, but to those who are outside, all things are done in parables,
11Naye akawaambia, "Ninyi mmejaliwa kujua siri ya Utawala wa Mungu, lakini wale walio nje wataambiwa kila kitu kwa mifano,
12 that ‘seeing they may see, and not perceive; and hearing they may hear, and not understand; lest perhaps they should turn again, and their sins should be forgiven them.’”
12ili, Watazame kweli, lakini wasione. Wasikie kweli, lakini wasielewe. La sivyo, wangemgeukia Mungu, naye angewasamehe."
13He said to them, “Don’t you understand this parable? How will you understand all of the parables?
13Basi, Yesu akawauliza, "Je, ninyi hamwelewi mfano huu? Mtawezaje basi, kuelewa mfano wowote?
14 The farmer sows the word.
14Mpanzi hupanda neno la Mungu.
15 The ones by the road are the ones where the word is sown; and when they have heard, immediately Satan comes, and takes away the word which has been sown in them.
15Watu wengine ni kama wale walio njiani ambapo mbegu zilianguka. Hawa hulisikia hilo neno lakini mara Shetani huja na kuliondoa neno hilo lililopandwa ndani yao.
16 These in the same way are those who are sown on the rocky places, who, when they have heard the word, immediately receive it with joy.
16Watu wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa penye mawe. Mara tu wanapolisikia hilo neno hulipokea kwa furaha.
17 They have no root in themselves, but are short-lived. When oppression or persecution arises because of the word, immediately they stumble.
17Lakini haliwaingii na kuwa na mizizi ndani yao; huendelea kulizingatia kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya hilo neno mara wanakata tamaa.
18 Others are those who are sown among the thorns. These are those who have heard the word,
18Watu wengine ni kama zile mbegu zilizoanguka penye miti ya miiba. Huo ni mfano wa wale wanaolisikia hilo neno,
19 and the cares of this age, and the deceitfulness of riches, and the lusts of other things entering in choke the word, and it becomes unfruitful.
19lakini wasiwasi wa ulimwengu huu, anasa za mali na tamaa za kila namna huwaingia na kulisonga hilo neno, nao hawazai matunda.
20 Those which were sown on the good ground are those who hear the word, and accept it, and bear fruit, some thirty times, some sixty times, and some one hundred times.”
20Lakini wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa katika udongo mzuri. Hawa hulisikia hilo neno, wakalipokea, wakazaa matunda: wengine thelathini, wengine sitini na wengine mia moja."
21He said to them, “Is the lamp brought to be put under a basket or under a bed? Isn’t it put on a stand?
21Yesu akaendelea kuwaambia, "Je, watu huwasha taa wakaileta ndani na kuifunika kwa pishi au kuiweka mvunguni? La! Huiweka juu ya kinara.
22 For there is nothing hidden, except that it should be made known; neither was anything made secret, but that it should come to light.
22Basi, kila kilichofichwa kitafichuliwa, na kila kilichofunikwa kitafunuliwa.
23 If any man has ears to hear, let him hear.”
23Mwenye masikio na asikie!"
24He said to them, “Take heed what you hear. With whatever measure you measure, it will be measured to you, and more will be given to you who hear.
24Akawaambia pia, "Sikilizeni kwa makini mnachosikia! Kipimo kilekile mnachowapimia watu wengine, ndicho mtakachopimiwa; tena mtazidishiwa.
25 For whoever has, to him will more be given, and he who doesn’t have, even that which he has will be taken away from him.”
25Aliye na kitu atapewa zaidi; asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa."
26He said, “The Kingdom of God is as if a man should cast seed on the earth,
26Yesu akaendelea kusema, "Ufalme wa Mungu ni kama ifuatavyo. Mtu hupanda mbegu shambani.
27 and should sleep and rise night and day, and the seed should spring up and grow, he doesn’t know how.
27Usiku hulala, mchana yu macho na wakati huo mbegu zinaota na kukua; yeye hajui inavyofanyika.
28 For the earth bears fruit: first the blade, then the ear, then the full grain in the ear.
28Udongo wenyewe huiwezesha mimea kukua na kuzaa matunda: kwanza huchipua jani changa, kisha suke, na mwishowe nafaka ndani ya suke.
29 But when the fruit is ripe, immediately he puts forth the sickle, because the harvest has come.”
29Nafaka inapoiva, huyo mtu huanza kutumia mundu wake, maana wakati wa mavuno umefika."
30He said, “How will we liken the Kingdom of God? Or with what parable will we illustrate it?
30Tena, Yesu akasema, "Tuufananishe Utawala wa Mungu na nini? Tuueleze kwa mifano gani?
31 It’s like a grain of mustard seed, which, when it is sown in the earth, though it is less than all the seeds that are on the earth,
31Ni kama mbegu ya haradali ambayo ni ndogo kuliko mbegu zote.
32 yet when it is sown, grows up, and becomes greater than all the herbs, and puts out great branches, so that the birds of the sky can lodge under its shadow.”
32Lakini ikisha pandwa, huota na kuwa mmea mkubwa kuliko mimea yote ya shambani. Matawi yake huwa makubwa hata ndege wa angani huweza kujenga viota vyao katika kivuli chake."
33With many such parables he spoke the word to them, as they were able to hear it.
33Yesu aliwahubiria ujumbe wake kwa mifano mingine mingi ya namna hiyo; aliongea nao kadiri walivyoweza kusikia.
34Without a parable he didn’t speak to them; but privately to his own disciples he explained everything.
34Hakuongea nao chochote bila kutumia mifano; lakini alipokuwa pamoja na wanafunzi wake peke yao alikuwa akiwafafanulia kila kitu.
35On that day, when evening had come, he said to them, “Let’s go over to the other side.”
35Jioni, siku hiyohiyo, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, "Tuvuke ziwa, twende ng'ambo."
36Leaving the multitude, they took him with them, even as he was, in the boat. Other small boats were also with him.
36Basi, wakauacha ule umati wa watu, wakamchukua Yesu katika mashua alimokuwa. Palikuwapo pia mashua nyingine hapo.
37A big wind storm arose, and the waves beat into the boat, so much that the boat was already filled.
37Basi, dhoruba kali ikaanza kuvuma, mawimbi yakaipiga ile mashua hata ikaanza kujaa maji.
38He himself was in the stern, asleep on the cushion, and they woke him up, and told him, “Teacher, don’t you care that we are dying?”
38Yesu alikuwa sehemu ya nyuma ya mashua, amelala juu ya mto. Basi, wanafunzi wakamwamsha na kumwambia, "Mwalimu, je, hujali kwamba sisi tunaangamia?"
39He awoke, and rebuked the wind, and said to the sea, “Peace! Be still!” The wind ceased, and there was a great calm.
39Basi, akaamka, akaukemea ule upepo na kuyaamrisha mawimbi ya ziwa, "Kimya! Tulia!" Hapo upepo ukakoma, kukawa shwari kabisa.
40He said to them, “Why are you so afraid? How is it that you have no faith?”
40Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Mbona mnaogopa? Je, bado hamna imani?"
41They were greatly afraid, and said to one another, “Who then is this, that even the wind and the sea obey him?”
41Nao wakaogopa sana, wakawa wanaulizana, "Huyu ni nani basi, hata upepo na mawimbi vinamtii?"