World English Bible

Swahili: New Testament

Mark

5

1They came to the other side of the sea, into the country of the Gadarenes.
1Basi, wakafika katika nchi ya Wagerase, ng'ambo ya ziwa.
2When he had come out of the boat, immediately a man with an unclean spirit met him out of the tombs.
2Mara tu Yesu aliposhuka mashuani, mtu mmoja aliyepagawa na pepo mchafu alitoka makaburini, akakutana naye.
3He lived in the tombs. Nobody could bind him any more, not even with chains,
3Mtu huyo alikuwa akiishi makaburini wala hakuna mtu aliyeweza tena kumfunga kwa minyororo.
4because he had been often bound with fetters and chains, and the chains had been torn apart by him, and the fetters broken in pieces. Nobody had the strength to tame him.
4Mara nyingi walimfunga kwa pingu na minyororo lakini kila mara aliweza kuikata hiyo minyororo na kuzivunja hizo pingu, wala hakuna mtu aliyeweza kumzuia.
5Always, night and day, in the tombs and in the mountains, he was crying out, and cutting himself with stones.
5Mchana na usiku alikaa makaburini na milimani akipaaza sauti na kujikatakata kwa mawe.
6When he saw Jesus from afar, he ran and bowed down to him,
6Alipomwona Yesu kwa mbali, alimkimbilia, akamwinamia
7and crying out with a loud voice, he said, “What have I to do with you, Jesus, you Son of the Most High God? I adjure you by God, don’t torment me.”
7akisema kwa sauti kubwa, "Una shauri gani nami, wewe Yesu Mwana wa Mungu aliye juu? Kwa jina la Mungu, nakusihi usinitese!"
8For he said to him, “Come out of the man, you unclean spirit!”
8(Alisema hivyo kwa kuwa Yesu alikuwa amemwambia, "Pepo mchafu, mtoke mtu huyu.")
9He asked him, “What is your name?” He said to him, “My name is Legion, for we are many.”
9Basi, Yesu akamwuliza, "Jina lako nani?" Naye akajibu, "Jina langu ni Jeshi, maana sisi tu wengi."
10He begged him much that he would not send them away out of the country.
10Kisha akamsihi Yesu asiwafukuze hao pepo katika nchi ile.
11Now on the mountainside there was a great herd of pigs feeding.
11Kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe malishoni kwenye mteremko wa mlima.
12All the demons begged him, saying, “Send us into the pigs, that we may enter into them.”
12Basi, hao pepo wakamsihi, "Utupeleke kwa hao nguruwe, tuwaingie."
13At once Jesus gave them permission. The unclean spirits came out and entered into the pigs. The herd of about two thousand rushed down the steep bank into the sea, and they were drowned in the sea.
13Naye akawaruhusu. Basi, hao pepo wachafu wakatoka, wakawaingia wale nguruwe. Kundi lote la nguruwe wapatao elfu mbili likaporomoka kwenye ule mteremko mkali mpaka ziwani, likatumbukia majini.
14Those who fed them fled, and told it in the city and in the country. The people came to see what it was that had happened.
14Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakatangaza jambo hilo mjini na mashambani. Watu wakafika kuona yaliyotukia.
15They came to Jesus, and saw him who had been possessed by demons sitting, clothed, and in his right mind, even him who had the legion; and they were afraid.
15Wakamwendea Yesu, wakamwona na mtu yuleyule aliyekuwa amepagawa na jeshi la pepo ameketi chini, amevaa nguo na ana akili yake sawa, wakaogopa.
16Those who saw it declared to them how it happened to him who was possessed by demons, and about the pigs.
16Watu walishuhudia tukio hilo wakaeleza wengine mambo yaliyompata huyo mtu aliyekuwa amepagawa na pepo na juu ya wale nguruwe.
17They began to beg him to depart from their region.
17Basi, wakaanza kumwomba aondoke katika nchi yao.
18As he was entering into the boat, he who had been possessed by demons begged him that he might be with him.
18Yesu alipokuwa anapanda mashuani, yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo akamwomba amruhusu kwenda naye.
19He didn’t allow him, but said to him, “Go to your house, to your friends, and tell them what great things the Lord has done for you, and how he had mercy on you.”
19Lakini Yesu akamkatalia. Badala yake akamwambia, "Nenda nyumbani kwa jamaa yako, ukawaambie mambo yote Bwana aliyokutendea na jinsi alivyokuonea huruma."
20He went his way, and began to proclaim in Decapolis how Jesus had done great things for him, and everyone marveled.
20Basi, huyo mtu akaenda, akaanza kutangaza huko Dekapoli mambo yote Yesu aliyomtendea; watu wote wakashangaa.
21When Jesus had crossed back over in the boat to the other side, a great multitude was gathered to him; and he was by the sea.
21Yesu alivukia tena upande wa pili wa ziwa kwa mashua. Umati mkubwa wa watu ukakusanyika mbele yake, naye akawa amesimama kando ya ziwa.
22Behold, one of the rulers of the synagogue, Jairus by name, came; and seeing him, he fell at his feet,
22Hapo akaja mmojawapo wa maofisa wa sunagogi, jina lake Yairo. Alipomwona Yesu, akajitupa mbele ya miguu yake,
23and begged him much, saying, “My little daughter is at the point of death. Please come and lay your hands on her, that she may be made healthy, and live.”
23akamsihi akisema, "Binti yangu mdogo ni mgonjwa karibu kufa. Twende tafadhali, ukamwekee mikono yako, apate kupona na kuishi."
24He went with him, and a great multitude followed him, and they pressed upon him on all sides.
24Basi, Yesu akaondoka pamoja naye. Watu wengi sana wakamfuata, wakawa wanamsonga kila upande.
25A certain woman, who had an issue of blood for twelve years,
25Mmojawapo alikuwa mwanamke mwenye ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili.
26and had suffered many things by many physicians, and had spent all that she had, and was no better, but rather grew worse,
26Mwanamke huyo alikuwa amekwisha sumbuka sana kuwaendea waganga wengi. Na ingawa alikuwa amekwisha tumia mali yake yote, hakupata nafuu bali hali yake ilizidi kuwa mbaya.
27having heard the things concerning Jesus, came up behind him in the crowd, and touched his clothes.
27Alikuwa amesikia habari za Yesu, na hivyo akaupenya msongamano wa watu kutoka nyuma, akagusa vazi lake.
28For she said, “If I just touch his clothes, I will be made well.”
28Alifanya hivyo, maana alijisemea, "Nikigusa tu vazi lake, nitapona."
29Immediately the flow of her blood was dried up, and she felt in her body that she was healed of her affliction.
29Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, akajisikia mwilini mwake kwamba ameponywa ugonjwa wake.
30Immediately Jesus, perceiving in himself that the power had gone out from him, turned around in the crowd, and asked, “Who touched my clothes?”
30Yesu alitambua mara kwamba nguvu imemtoka. Basi akaugeukia ule umati wa watu, akauliza, "Nani aliyegusa mavazi yangu?"
31His disciples said to him, “You see the multitude pressing against you, and you say, ‘Who touched me?’”
31Wanafunzi wake wakamjibu, "Unaona jinsi watu wanavyokusonga; mbona wauliza nani aliyekugusa?"
32He looked around to see her who had done this thing.
32Lakini Yesu akaendelea kutazama amwone huyo aliyefanya hivyo.
33But the woman, fearing and trembling, knowing what had been done to her, came and fell down before him, and told him all the truth.
33Hapo huyo mwanamke, akifahamu yaliyompata, akajitokeza akitetemeka kwa hofu, akajitupa chini mbele ya Yesu na kusema ukweli wote.
34He said to her, “Daughter, your faith has made you well. Go in peace, and be cured of your disease.”
34Yesu akamwambia, "Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani, upone kabisa ugonjwa wako."
35While he was still speaking, people came from the synagogue ruler’s house saying, “Your daughter is dead. Why bother the Teacher any more?”
35Yesu alipokuwa bado anaongea, watu walifika kutoka nyumbani kwa yule ofisa wa sunagogi, wakamwambia, "Binti yako amekwisha kufa. Ya nini kuendelea kumsumbua Mwalimu?"
36But Jesus, when he heard the message spoken, immediately said to the ruler of the synagogue, “Don’t be afraid, only believe.”
36Lakini, bila kujali walichosema, Yesu akamwambia mkuu wa sunagogi, "Usiogope, amini tu."
37He allowed no one to follow him, except Peter, James, and John the brother of James.
37Wala hakumruhusu mtu yeyote kufuatana naye ila Petro, Yakobo na Yohane nduguye Yakobo.
38He came to the synagogue ruler’s house, and he saw an uproar, weeping, and great wailing.
38Wakafika nyumbani kwa ofisa wa sunagogi naye Yesu akasikia makelele, kilio na maombolezo mengi.
39When he had entered in, he said to them, “Why do you make an uproar and weep? The child is not dead, but is asleep.”
39Akaingia ndani, akawaambia, "Mbona mnapiga kelele na kulia? Msichana hakufa, amelala tu."
40They ridiculed him. But he, having put them all out, took the father of the child, her mother, and those who were with him, and went in where the child was lying.
40Lakini wao wakamcheka. Basi, akawaondoa wote nje, akawachukua baba na mama ya huyo msichana na wale wanafunzi wake, wakaingia chumbani alimokuwa huyo msichana.
41Taking the child by the hand, he said to her, “Talitha cumi!” which means, being interpreted, “Girl, I tell you, get up!”
41Kisha akamshika mkono, akamwambia, "Talitha, kumi," maana yake, "Msichana, nakwambia, amka!"
42Immediately the girl rose up and walked, for she was twelve years old. They were amazed with great amazement.
42Mara msichana akasimama, akaanza kutembea. (Alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili.) Hapo watu wakashangaa kupita kiasi.
43He strictly ordered them that no one should know this, and commanded that something should be given to her to eat.
43Yesu akawakataza sana wasimjulishe mtu jambo hilo. Kisha akawaambia wampe huyo msichana chakula.