聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

1 Timothy

2

1要为万人祷告
1Kwanza kabisa, basi naomba dua, sala, maombi na sala za shukrani zitolewe kwa Mungu kwa ajili ya watu wote,
2
2kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema.
3在我们的救主 神看来,这是美好的,可蒙悦纳的。
3Jambo hili ni jema na lampendeza Mungu Mwokozi wetu,
4他愿意万人得救,并且充分认识真理。
4ambaye anataka watu wote waokolewe na wapate kuujua ukweli.
5因为 神只有一位,在 神和人中间也只有一位中保,就是降世为人的基督耶稣。
5Maana yuko Mungu mmoja, na pia yuko mmoja anayewapatanisha watu na Mungu, binadamu Kristo Yesu,
6他舍了自己作万人的赎价,到了适当的时候,这事就证实了。
6ambaye alijitoa mwenyewe kuwakomboa watu wote. Huo ulikuwa uthibitisho, wakati ufaao ulipowadia.
7为了这事,我也被派作传道的和使徒(我说的是真话,不是谎言),在信仰和真理上作外族人的教师。
7Kwa sababu hiyo mimi nilitumwa niwe mtume na mwalimu wa watu wa mataifa, niutangaze ujumbe wa imani na ukweli. Nasema ukweli; sisemi uongo!
8敬畏 神的女人因此,我愿意男人没有忿怒,没有争论,举起圣洁的手随处祷告。
8Basi, popote mnapokutana kufanya ibada nataka wanaume wasali, watu waliojitolea kweli na ambao wanaweza kuinua mikono yao wakisali bila hasira wala ubishi.
9照样,我也愿意女人以端正、娴淑、自律为装饰;不要以鬈发、金饰、珠宝,或名贵衣裳为装饰,
9Hali kadhalika, nawataka wanawake wawe wanyofu na wenye busara kuhusu mavazi yao; wavae sawasawa na si kwa urembo wa mitindo ya kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa,
10却要以善行作装饰,这才配称为敬畏 神的女人。
10bali kwa matendo mema kama iwapasavyo wanawake wamchao Mungu.
11女人应该安静而又完全顺服地学习。
11Wanawake wanapaswa kukaa kimya na kuwa wanyenyekevu wakati wa kujifunza.
12我不准女人教训男人,辖制男人;女人总要安静。
12Mimi simruhusu mwanamke amfundishe au amtawale mwanamume; anapaswa kukaa kimya.
13因为先造的是亚当,后造的是夏娃;
13Maana Adamu aliumbwa kwanza, halafu Hawa.
14不是亚当受了引诱,而是女人受了引诱,陷在过犯里面。
14Na wala si Adamu aliyedanganywa; bali mwanamke ndiye aliyedanganywa, akaivunja sheria ya Mungu.
15然而女人要是常常存着信心、爱心、圣洁自律,在她生育的事上必定得救。
15Hata hivyo, mwanamke ataokolewa kwa kupata watoto, kama akidumu katika imani, upendo, utakatifu na unyofu.