聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

1 Timothy

3

1作监督的资格
1Msemo huu ni wa kweli: mtu akitaka kuwa kiongozi katika kanisa, huyo anatamani kazi nzuri.
2所以作监督的,必须无可指摘,只作一个妻子的丈夫,有节制,自律,庄重,乐意接待客旅,善于教导,
2Basi, kiongozi wa kanisa anapaswa awe mtu asiye na lawama; anapaswa awe na mke mmoja tu, awe mwenye kiasi, nidhamu na utaratibu; ni lazima awe mkarimu na anayeweza kufundisha;
3不好酒,不打人,只要温和,与人无争,不贪财,
3asiwe mlevi au mtu wa matata, bali awe mpole, apendaye amani; asiwe mtu wa kupenda fedha;
4好好管理自己的家,使儿女凡事敬重顺服。
4anapaswa awe mtu awezaye kuongoza vema nyumba yake, na kuwafanya watoto wake wawe watii kwa heshima yote.
5(人若不知道怎样管理自己的家,怎能照料 神的教会呢?)
5Maana kama mtu hawezi kuongoza vema nyumba yake, atawezaje kulitunza kanisa la Mungu?
6初信主的不可作监督,恐怕他骄傲,就落在魔鬼所受的刑罚里。
6Mtu ambaye hajakomaa bado katika imani asifanywe kuwa kiongozi katika kanisa, asije akajaa majivuno na kuhukumiwa kama vile Ibilisi alivyohukumiwa.
7作监督的也必须在教外有好声誉,免得他被人毁谤,就落在魔鬼的陷阱里。
7Anapaswa awe mwenye sifa njema kati ya watu walio nje ya kanisa, ili asije akalaumiwa na kuanguka katika mtego wa Ibilisi.
8作执事的资格照样,执事也必须庄重,不一口两舌,不酗酒,不贪不义之财,
8Wasaidizi katika kanisa wanapaswa pia kuwa watu wenye tabia njema na wanyofu; wasiwe wanywaji mno wa divai au wenye tamaa ya fedha;
9用清洁的良心持守信仰的奥秘。
9wanapaswa kuzingatia kwa dhamiri njema ukweli wa ndani wa imani.
10他们也必须先受考验,若没有可责之处,然后才让他们作执事。
10Ni lazima kwanza wathibitishwe, na wakionekana kuwa wanafaa, basi, watoe huduma yao.
11照样,他们的妻子(“他们的妻子”可解作“女执事”)也要庄重,不说谗言,有节制,凡事忠心。
11Wake zao wanapaswa pia kuwa na tabia njema, wasiowasengenya watu, wenye kiasi na waaminifu katika mambo yote.
12执事只可以作一个妻子的丈夫,善于管理儿女和自己的家。
12Msaidizi katika kanisa lazima awe na mke moja tu, na awezaye kuongoza vema watoto wake na nyumba yake.
13那善于作执事的,就为自己得了好的位分,也因着相信基督耶稣得到大大的胆量。
13Maana wasaidizi wanaofanya kazi yao vizuri hujipatia msimamo mzuri, na wanaweza kusema bila hofu juu ya imani yao katika Kristo Yesu.
14伟大的敬虔奥秘我把这些事写给你,希望不久可以到你那里去;
14Ninakuandikia barua hii nikiwa na matumaini ya kuja kwako hivi karibuni.
15假如我来迟了,你也可以知道在 神的家里应该怎样行。这家就是永活 神的教会、真理的柱石和根基。
15Lakini kama nikicheleweshwa, basi, barua hii itakufahamisha mwenendo tunaopaswa kuwa nao katika nyumba ya Mungu, ambayo ni kanisa la Mungu aliye hai, na ambalo ni nguzo na msingi wa ukweli.
16敬虔的奥秘真伟大啊,这是众人所公认的,就是:“他在肉身显现,在圣灵里称义,被天使看见;被传于列国,被世人信服,被接到荣耀里。”
16Hakuna mashaka yoyote juu ya ukuu wa siri ya dini yetu: Alionekana katika umbo la kibinadamu alithibitishwa na Roho kuwa ni mwadilifu, akaonekana na malaika. Alihubiriwa kati ya mataifa, aliaminiwa popote ulimwenguni, akachukuliwa juu mbinguni katika utukufu.