聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Luke

1

1序言(参徒1:1)
1Mheshimiwa Theofilo: Watu wengi wamejitahidi kuandika juu ya mambo yale yaliyotendeka kati yetu.
2按照起初亲眼看见的传道人所传给我们的,编著成书;
2Waliandika kama tulivyoelezwa na wale walioyaona kwa macho yao tangu mwanzo, na waliotangaza ujumbe huo.
3我已经把这些事从头考查过,认为也应该按着次序写给你,
3Inafaa nami pia, Mheshimiwa, baada ya kuchunguza kwa makini mambo yote tangu mwanzo, nikuandikie kwa mpango,
4让你晓得所学到的道理,都是确实的。
4ili nawe uweze kujionea mwenyewe ukweli wa mambo yale uliyofundishwa.
5天使预言施洗约翰出生犹太王希律在位的日子,亚比雅班里有一个祭司,名叫撒迦利亚,他妻子是亚伦的后代,名叫以利沙伯。
5Wakati Herode alipokuwa mfalme wa Yudea, kulikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa kikundi cha Abia. Mke wake alikuwa anaitwa Elisabeti, naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni.
6他们在 神面前都是义人,遵行主的一切诫命规条,无可指摘,
6Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama.
7只是没有孩子,因为以利沙伯不生育,二人又都上了年纪。
7Lakini hawakuwa wamejaliwa watoto kwa vile Elisabeti alikuwa tasa, nao wote wawili walikuwa wazee sana.
8有一次,撒迦利亚在 神面前按着班次执行祭司的职务,
8Siku moja, ilipokuwa zamu yake ya kutoa huduma ya ukuhani mbele ya Mungu,
9照祭司的惯例抽中了签,进入主的圣殿烧香。
9Zakariya alichaguliwa kwa kura, kama ilivyokuwa desturi, kuingia hekaluni ili afukize ubani.
10烧香的时候,众人都在外面祈祷。
10Watu, umati mkubwa, walikuwa wamekusanyika nje wanasali wakati huo wa kufukiza ubani.
11有主的使者站在香坛右边,向他显现。
11Malaika wa Bwana akamtokea humo ndani, akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia ubani.
12撒迦利亚一见就惊慌起来,十分害怕。
12Zakariya alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia.
13天使说:“撒迦利亚,不要怕,因为你的祈求已蒙垂听,你妻子以利沙伯要给你生一个儿子,你要给他起名叫约翰。
13Lakini malaika akamwambia, "Zakariya, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane.
14你必欢喜快乐,许多人因他出生,也必喜乐。
14Utakuwa na furaha kubwa na watu wengi watashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake.
15他在主面前要被尊为大,淡酒浓酒都不喝,未出母腹就被圣灵充满。
15Atakuwa mkuu mbele ya Bwana. Hatakunywa divai wala kileo, atajazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake.
16他要使许多以色列人转向主他们的 神。
16Atawaelekeza wengi wa watu wa Israeli kwa Bwana Mungu wao.
17他必有以利亚的灵和能力,行在主的前面,叫父亲的心转向儿女,叫悖逆的转向义人的意念,为主安排那预备好了的人民。”
17Atamtangulia Bwana akiongozwa na nguvu na roho kama Eliya. Atawapatanisha kina baba na watoto wao; atawafanya wasiotii wawe na fikira za uadilifu, na hivyo amtayarishie Bwana watu wake."
18撒迦利亚对天使说:“我怎么能知道这事呢?我已经老了,我妻子也上了年纪。”
18Zakariya akamwambia huyo malaika, "Ni kitu gani kitakachonihakikishia jambo hilo? Mimi ni mzee, hali kadhalika na mke wangu."
19天使回答:“我是站在 神面前的加百列,奉差遣向你说话,报给你这好消息。
19Malaika akamjibu, "Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele ya Mungu, na nimetumwa niseme nawe, nikuletee hii habari njema.
20看吧!到了时候我的话必要应验;因为你不信我的话,你必成为哑巴,直到这些事成就的那一天,才能说话。”
20Sikiliza, utakuwa bubu kwa sababu huyasadiki haya maneno yatakayotimia kwa wakati wake. Hutaweza kusema mpaka hayo niliyokuambia yatakapotimia."
21众人等候撒迦利亚;因他在圣殿里迟迟不出来,觉得奇怪。
21Wakati huo, wale watu walikuwa wanamngoja Zakariya huku wakishangaa juu ya kukawia kwake Hekaluni.
22等到他出来,却不能讲话,竟成了哑巴,不断地向他们打手式,他们就知道他在圣殿里见了异象。
22Alipotoka nje, hakuweza kusema nao. Ikawa dhahiri kwao kwamba alikuwa ameona maono Hekaluni. Lakini akawa anawapa ishara kwa mikono, akabaki bubu.
23供职的日子满了,他就回家去。
23Zamu yake ya kuhudumu ilipokwisha, alirudi nyumbani.
24过了几天,他妻子以利沙伯怀了孕,隐藏了五个月,说:
24Baadaye Elisabeti mkewe akapata mimba. Akajificha nyumbani kwa muda wa miezi mitano, akisema:
25“主在眷顾的日子,这样看待我,要把我在人间的羞耻除掉。”
25"Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana; ameniangalia na kuniondolea aibu niliyokuwa nayo mbele ya watu."
26天使预言耶稣降生到了第六个月,天使加百列奉 神差遣,往加利利的拿撒勒城去,
26Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya,
27到了一个童贞女那里,她已经和大卫家一个名叫约瑟的人订了婚,童贞女的名字是马利亚。
27kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi.
28天使进去,对她说:“恭喜!蒙大恩的女子,主与你同在!”
28Malaika akamwendea, akamwambia, "Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe."
29她却因这话惊慌起来,反复思想这样祝贺是什么意思。
29Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini?
30天使说:“马利亚,不要怕!因你已从 神那里蒙了恩。
30Malaika akamwambia, "Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema.
31你将怀孕生子,要给他起名叫耶稣。
31Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu.
32他将要被尊为大,称为至高者的儿子,主 神要把他祖大卫的王位赐给他,
32Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake.
33他要作王统治雅各家,直到永远,他的国没有穷尽。”
33Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho."
34马利亚对天使说:“我还没有出嫁,怎能有这事呢?”
34Maria akamjibu, "Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?"
35天使回答:“圣灵要临到你,至高者的能力要覆庇你,因此那将要出生的圣者,必称为 神的儿子。
35Malaika akamjibu, "Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu.
36你看,你亲戚以利沙伯,被称为不生育的,在老年也怀了男胎,现在已是第六个月了,
36Ujue pia kwamba hata Elisabeti, jamaa yako, naye amepata mimba ingawa ni mzee, na sasa ni mwezi wa sita kwake yeye ambaye watu walimfahamu kuwa tasa.
37因为在 神没有一件事是不可能的。”
37Kwa maana hakuna jambo lisilowezekana kwa Mungu."
38马利亚说:“我是主的婢女,愿照你的话成就在我身上!”天使就离开她去了。
38Maria akasema, "Mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe kama ulivyosema." Kisha yule malaika akaenda zake.
39马利亚往见以利沙伯后来,马利亚就起身,急忙向山地去,来到犹大的一座城,
39Siku kadhaa baadaye, Maria alifunga safari akaenda kwa haraka hadi mji mmoja ulioko katika milima ya Yuda.
40进了撒迦利亚的家,向以利沙伯问安。
40Huko, aliingia katika nyumba ya Zakariya, akamsalimu Elisabeti.
41以利沙伯一听见马利亚的问安,腹中的胎儿就跳动,以利沙伯也被圣灵充满,
41Mara tu Elisabeti aliposikia sauti ya Maria, mtoto mchanga tumboni mwake Elisabeti akaruka. Naye Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifiu,
42就高声说:“你在女子中是有福的!你腹中的胎儿也是有福的!
42akasema kwa sauti kubwa, "Umebarikiwa kuliko wanawake wote, naye utakayemzaa amebarikiwa.
43我主的母亲竟然到我这里来。这事怎会临到我呢?
43Mimi ni nani hata mama wa Bwana wangu afike kwangu?
44你看,你问安的声音一进我的耳朵,我腹中的胎儿就欢喜跳跃。
44Nakwambia, mara tu niliposikia sauti yako, mtoto mchanga tumboni mwangu aliruka kwa furaha.
45这相信主传给她的话必要成就的女子是有福的。”
45Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale Bwana aliyokwambia."
46马利亚尊主为大(参撒上2:1-10)马利亚说:“我心尊主为大,
46Naye Maria akasema,
47我灵以 神我的救主为乐,
47"Moyo wangu wamtukuza Bwana, roho yangu inafurahi kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu.
48因为他垂顾他使女的卑微,看哪!今后万代都要称我为有福。
48Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mnyenyekevu. Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri.
49全能者为我行了大事,他的名为圣;
49Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenitendea makuu, jina lake ni takatifu.
50他的怜悯世世代代归与敬畏他的人。
50Huruma yake kwa watu wanaomcha hudumu kizazi hata kizazi.
51他用膀臂施展大能,驱散心里妄想的狂傲人。
51Amefanya mambo makuu kwa mkono wake: amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
52他使有权能的失位,叫卑微的升高,
52amewashusha wenye nguvu kutoka vitu vyao vya enzi, akawakweza wanyenyekevu.
53让饥饿的得饱美食,使富足的空手回去。
53Wenye njaa amewashibisha mema, matajiri amewaacha waende mikono mitupu.
54他扶助了他的仆人以色列,为要记念他的怜悯,
54Amemsaidia Israeli mtumishi wake, akikumbuka huruma yake.
55正如他向我们列祖所说的,恩待亚伯拉罕和他的后裔,直到永远。”
55Kama alivyowaahidia wazee wetu Abrahamu na wazawa wake hata milele."
56马利亚和以利沙伯同住约有三个月,就回家去了。
56Maria alikaa na Elisabeti kwa muda upatao miezi mitatu, halafu akarudi nyumbani kwake.
57施洗约翰出生以利沙伯的产期到了,生了一个儿子。
57Wakati wa kujifungua kwake Elisabeti ulifika, akajifungua mtoto wa kiume.
58邻里亲戚,听见主向她大施怜悯,都和她一同欢乐。
58Jirani na watu wa jamaa yake walipopata habari kwamba Bwana amemwonea huruma kubwa, walifurahi pamoja naye.
59到了第八天,他们来给孩子行割礼,要照他父亲的名字,叫他撒迦利亚。
59Halafu siku ya nane walifika kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la baba yake, Zakariya.
60但他母亲说:“不可,要叫他约翰。”
60Lakini mama yake akasema, "La, sivyo, bali ataitwa Yohane."
61他们说:“你亲族里没有叫这名字的。”
61Wakamwambia, "Mbona hakuna yeyote katika ukoo wake mwenye jina hilo?"
62他们就向孩子的父亲打手式,看他要叫他什么。
62Basi, wakamwashiria baba yake wapate kujua alitaka mtoto wake apewe jina gani.
63他要了一块写字版,写上说:“他的名字是约翰。”众人都希奇。
63Naye akaomba kibao cha kuandikia, akaandika hivi: "Yohane ndilo jina lake." Wote wakastaajabu.
64撒迦利亚的口舌立刻开了,就出声称颂 神。
64Papo hapo midomo na ulimi wake Zakariya vikafunguliwa, akawa anaongea akimsifu Mungu.
65住在周围的人都害怕,这一切事传遍了整个犹太山地,
65Hofu ikawaingia jirani wote, na habari hizo zikaenea kila mahali katika milima ya Yudea.
66凡听见的就把这些事放在心里,说:“这孩子将会成为怎样的人呢?因为主的手与他同在。”
66Wote waliosikia mambo hayo waliyatafakari mioyoni mwao wakisema: "Mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?" Maana, hakika nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye.
67撒迦利亚的预言他的父亲撒迦利亚被圣灵充满,预言说:
67Zakariya, baba yake mtoto, akajazwa Roho Mtakatifu, akatamka ujumbe wa Mungu:
68“主,以色列的 神,是应当称颂的,因他眷顾自己的子民,施行救赎,
68"Asifiwe Bwana Mungu wa Israeli, kwani amekuja kuwasaidia na kuwakomboa watu wake.
69在他仆人大卫家中,为我们兴起救恩的角,
69Ametupatia Mwokozi shujaa, mzawa wa Daudi mtumishi wake.
70正如主自古以来借圣先知口中所说的,
70Aliahidi hapo kale kwa njia ya manabii wake watakatifu,
71救我们脱离仇敌,和恨我们的人的手;
71kwamba atatuokoa mikononi mwa adui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.
72向我们列祖施怜悯,记念他的圣约,
72Alisema atawahurumia wazee wetu, na kukumbuka agano lake takatifu.
73就是他对我们祖先亚伯拉罕所起的誓,
73Kiapo alichomwapia Abrahamu baba yetu, ni kwamba atatujalia sisi
74把我们从仇敌手中救拔出来,叫我们可以坦然无惧,用圣洁公义,在他面前一生一世敬拜他。
74tukombolewe kutoka adui zetu, tupate kumtumikia bila hofu,
75
75kwa unyofu na uadilifu mbele yake, siku zote za maisha yetu.
76孩子啊,你要称为至高者的先知,因为你要行在主的面前,预备他的路,
76Nawe mwanangu, utaitwa, nabii wa Mungu Mkuu, utamtangulia Bwana kumtayarishia njia yake;
77使他的子民,因罪得赦,就知道救恩。
77kuwatangazia watu kwamba wataokolewa kwa kuondolewa dhambi zao.
78因我们 神的怜悯,使清晨的阳光从高天临到我们,
78Mungu wetu ni mpole na mwenye huruma. Atasababisha pambazuko angavu la ukombozi litujie kutoka juu,
79光照那坐在黑暗中死荫里的人,引导我们的脚,走上平安的路。”
79na kuwaangazia wote wanaokaa katika giza kuu la kifo, aongoze hatua zetu katika njia ya amani."
80这孩子渐渐长大,心灵健壮,住在旷野,直到他在以色列人中公开露面的日子。
80Mtoto akakua, akapata nguvu rohoni. Alikaa jangwani mpaka alipojionyesha rasmi kwa watu wa Israeli.