1祈求就必得着(太6:9-13,7:7-11)
1Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akisali. Alipomaliza kusali, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, "Bwana, tunakuomba utufundishe kusali kama Yohane mbatizaji alivyowafundisha wanafunzi wake."
2耶稣说:“你们祷告的时候,要说:‘父啊,愿你的名被尊为圣,愿你的国降临(有些抄本在此有“愿你的旨意行在地上,如同行在天上”一句);
2Yesu akawaambia, "Mnaposali, semeni: Baba! Jina lako litukuzwe; Ufalme wako ufike.
3我们需用的食物,求你每天赐给我们;
3Utupe daima chakula chetu cha kila siku.
4赦免我们的罪,因为我们也饶恕所有亏负我们的人;不要让我们陷入试探(有些抄本在此有“救我们脱离那恶者”一句)。’”
4Utusamehe dhambi zetu, maana sisi tunawasamehe wote waliotukosea; wala usitutie katika majaribu."
5耶稣又对他们说:“你们当中,谁有朋友半夜去找他,说:‘请你借给我三个饼,
5Kisha akawaambia, "Tuseme mmoja wenu anaye rafiki, akaenda kwake usiku wa manane, akamwambia: Rafiki, tafadhali niazime mikate mitatu,
6因为我有一个朋友旅行来到我这里,我没有什么可以招待他。’
6kwa kuwa rafiki yangu amepitia kwangu akiwa safarini nami sina cha kumpa.
7而他却在里面回答:‘不要麻烦我,门已经关好了,孩子也跟我在床上了,我不能起来拿给你。’
7Naye, akiwa ndani angemjibu: Usinisumbue! Nimekwisha funga mlango. Mimi na watoto wangu tumelala; siwezi kuamka nikupe!
8我告诉你们,即使不因为他是朋友而起来给他,也会因为他厚颜地直求,而起来照他所需要的给他。
8Hakika, ingawa hataamka ampe kwa sababu yeye ni rafiki yake, lakini, kwa sababu ya huyo mtu kuendelea kumwomba, ataamka ampe chochote anachohitaji.
9我又告诉你们,你们祈求,就给你们;寻找,就寻见;叩门,就给你们开门。
9Kwa hiyo, ombeni, nanyi mtapewa, tafuteni, nanyi mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa.
10因为所有祈求的就得着,寻找的就寻见,叩门的就给他开门。
10Maana yeyote aombaye hupewa, atafutaye hupata na abishaye hufunguliwa.
11你们中间作父亲的,哪有儿子求鱼,反拿蛇给他呢?
11Mtoto akimwomba baba yake samaki, je, atampa nyoka badala ya samaki?
12或求鸡蛋,反给他蝎子呢?
12Na kama akimwomba yai, je, atampa ng'e?
13你们虽然不好,尚且知道把好东西给自己的儿女,何况天父,岂不更把圣灵赐给求他的人吗?”
13Ninyi, ingawa ni waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri. Basi, baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi; atawapa Roho Mtakatifu wale wanaomwomba."
14耶稣靠 神的能力赶鬼(太12:22-30;可3:22-27)耶稣赶出一个哑巴鬼,鬼既出去,哑巴就说起话来,众人都希奇。
14Siku moja Yesu alikuwa anamfukuza pepo aliyemfanya mtu mmoja kuwa bubu. Basi, huyo pepo alipomtoka, yule mtu akaweza kuongea hata umati wa watu ukashangaa.
15有人说:“他靠鬼王别西卜赶鬼。”
15Lakini baadhi ya watu hao wakasema, "Anamfukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, mkuu wa pepo."
16又有人试探他,向他求一个从天上来的神迹。
16Wengine, wakimjaribu, wakamtaka afanye ishara kuonyesha kama alikuwa na idhini kutoka mbinguni.
17耶稣知道他们的心意,就对他们说:“如果一个国家自相纷争,就必定荒凉;如果一个家庭自相为敌,就必然败落。
17Lakini yeye, akiwa anayajua mawazo yao, akawaambia, "Ufalme wowote uliofarakana wenyewe, hauwezi kudumu; kadhalika, jamaa yeyote inayofarakana huangamia.
18如果撒但自相纷争,他的国怎能站立得住呢?你们说我靠别西卜赶鬼,
18Kama Shetani anajipinga mwenyewe, utawala wake utasimamaje? Mnasemaje, basi, kwamba ninawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli?
19我若靠别西卜赶鬼,你们的子孙赶鬼又靠谁呢?因此,他们必要作你们的审判官。
19Kama ninafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, watoto wenu huwafukuza kwa uwezo wa nani? Kwa sababu hiyo, wao ndio watakaowahukumu ninyi.
20我若靠 神的能力赶鬼,这就是 神的国临到你们了。
20Lakini ikiwa ninawafukuza pepo kwa uwezo wa Mungu, basi jueni kwamba Ufalme wa Mungu umekwisha fika kwenu.
21一个壮汉拿着武器,看守自己的家园,他的家财就平安无事。
21"Mtu mwenye nguvu anapolinda jumba lake kwa silaha, mali yake yote iko salama.
22但是一个比他更强的人来了,胜过了他,夺去他所倚靠的武器,就把他的家财当作掠物分了。
22Lakini akija mwenye nguvu zaidi akamshambulia na kumshinda, huyo huziteka silaha zake alizotegemea na kugawanya nyara.
23不站在我这一边的就是反对我的;不跟从一起收聚的就是分散的。
23Yeyote asiyejiunga nami, ananipinga; na yeyote asiyekusanya pamoja nami, hutawanya.
24污灵去而复返的教训(太12:43-45)“一个污灵离开了一个人,走遍干旱之地,寻找栖身的地方,却没有找到,就说:‘我要回到我从前离开了的那房子。’
24"Pepo mchafu akifukuzwa kwa mtu fulani, huzururazurura jangwani akitafuta mahali pa kupumzikia. Asipopata, hujisemea: Nitarudi kwenye makao yangu nilikotoka.
25到了之后,看见里面已经打扫干净,粉饰好了,
25Anaporudi, huikuta ile nyumba imefagiwa na kupambwa.
26他就去带了另外七个比自己更恶的污灵来,进去住在那里;那人后来的情况,比以前更坏了。”
26Basi, huenda na kuwachukua pepo wengine saba waovu zaidi kuliko yeye; wote huenda na kumwingia mtu yule. Hivyo, basi hali ya mtu huyo sasa huwa mbaya zaidi kuliko pale mwanzo."
27约拿的神迹(太12:39-42)耶稣正说这些话的时候,群众中有一个女人高声对他说:“怀你胎的和哺养你的有福了!”
27Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika lile kundi la watu, akasema kwa sauti kubwa: "Heri tumbo lililokuzaa, na maziwa yaliyokunyonyesha!"
28他说:“是的,却还不如听 神的道而遵守的人有福。”
28Lakini Yesu akasema, "Lakini heri zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulishika."
29众人聚集的时候,耶稣就说:“这世代是个邪恶的世代。这世代寻求神迹,可是除了约拿的神迹以外,再没有神迹给他们了。
29Umati wa watu ulipozidi kuongezeka, Yesu akawaambia, "Kizazi hiki ni kizazi kiovu. Kinataka ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ya Yona.
30约拿怎样成了尼尼微人的神迹,人子也照样成为这个世代的神迹。
30Jinsi Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninewi, ndivyo pia Mwana wa Mtu atakavyokuwa ishara kwa kizazi hiki.
31审判的时候,南方的女王要和这世代的人一同起来,她要定他们的罪,因为她从地极来到,要听所罗门智慧的话。你看,这里有一位是比所罗门更大的。
31Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, naye atashuhudia kwamba kina hatia. Yeye alisafiri kutoka mbali, akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni; kumbe hapa pana mkuu zaidi kuliko Solomoni.
32审判的时候,尼尼微人要和这世代的人一同起来,他们要定这个世代的罪,因为尼尼微人听了约拿所传的就悔改了。你看,这里有一位是比约拿更大的。
32Watu wa Ninewi watatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, na watashuhudia kwamba kizazi hiki kina hatia. Hao watu wa Ninewi walitubu kwa sababu ya mahubiri ya Yona; na hapa pana mkuu zaidi kuliko Yona!
33里面的光(太5:15,6:22-23)“没有人点了灯,把它放在地窖里,或量器底下,却放在灯台上,叫进来的人看得见光。
33"Hakuna mtu anayewasha taa na kuifunika kwa pishi, bali huiweka juu ya kinara ili watu wanaoingia ndani wapate kuona mwanga.
34你的眼睛就是你身体的灯,你的眼睛健全,全身就明亮;如果不健全,全身就黑暗。
34Jicho lako ni kama taa ya mwili wako; likiwa zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga. Jicho lako likiwa bovu, na mwili wako pia utakuwa katika giza.
35所以要谨慎,免得你里面的光黑暗了。
35Uwe mwangalifu basi mwanga ulio ndani yako usije ukawa giza.
36你若全身明亮,没有一点黑暗,你就完全明亮,好像明亮的灯光照你一样。”
36Basi, kama mwili wako wote una mwanga, bila kuwa na sehemu yoyote yenye giza, mwili huo utang'aa kikamilifu kama vile taa inavyokuangazia kwa mwanga wake."
37法利赛人和律法师有祸了(太23:1-36;可12:38-40)耶稣说话的时候,有一个法利赛人请耶稣和他一起吃饭;他就进去坐席。
37Yesu alipokuwa akiongea, Mfarisayo mmoja alimkaribisha chakula nyumbani kwake, naye akaenda, akaketi kula chakula.
38这个法利赛人见耶稣吃饭之前不洗手,觉得奇怪。
38Huyo Mfarisayo alistaajabu kuona kwamba alikula chakula bila kunawa.
39主对他说:“你们法利赛人把杯盘的外面洗净,但你们里面却充满了抢夺和邪恶。
39Bwana akamwambia, "Ninyi Mafarisayo huosha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani mmejaa udhalimu na uovu.
40无知的人哪,那造外面的,不也造里面吗?
40Wapumbavu ninyi! Je, aliyetengeneza nje si ndiye aliyetengeneza ndani pia?
41只要把里面的施舍出去,你们的一切就都洁净了。
41Toeni kwa maskini vile vitu vilivyomo ndani, na vingine vyote vitakuwa halali kwenu.
42然而你们法利赛人有祸了!因为你们把薄荷、茴香和各样菜蔬献上十分之一,却把公义和爱 神的事疏忽了;这些是你们应当作的,但其他的也不可疏忽。
42"Lakini ole wenu Mafarisayo, kwa sababu mnatoza watu zaka hata juu ya majani ya kukolezea chakula, mchicha na majani mengine, na huku hamjali juu ya haki na upendo kwa Mungu. Mambo haya iliwapasa muwe mmeyazingatia bila kuyasahau yale mengine.
43你们法利赛人有祸了!因为你们喜爱会堂里的高位和人在巿中心的问安。
43"Ole wenu ninyi Mafarisayo, kwa sababu mnapenda kuketi mbele mahali pa heshima katika masunagogi, na kusalimiwa kwa heshima hadharani.
44你们有祸了!因为你们好像不显露的坟墓,走在上面的人并不知道。”
44Ole wenu, kwa sababu mko kama makaburi yaliyofichika; watu hutembea juu yake bila kufahamu."
45律法师中有一个回答他:“老师,你这样说,把我们也侮辱了!”
45Mmoja wa walimu wa Sheria akamwambia, "Mwalimu, maneno yako yanatukashifu na sisi pia."
46耶稣说:“你们律法师也有祸了,因为你们把难担的担子叫人担,自己连一个指头也不动。
46Yesu akamjibu, "Na ninyi walimu wa Sheria, ole wenu; maana mnawatwika watu mizigo isiyochukulika, huku ninyi wenyewe hamnyoshi hata kidole kuwasaidia.
47你们有祸了!因为你们修造先知的坟墓,而那些先知正是你们祖先所杀的,
47Ole wenu, kwa kuwa mnajenga makaburi ya manabii wale ambao wazee wenu waliwaua.
48这样,你们就成了证人,对你们祖先的作为表示同意;他们杀害先知,你们修造先知的坟墓。
48Kwa hiyo mnashuhudia na kukubaliana na matendo ya wazee wenu; maana wao waliwaua hao manabii, nanyi mnajenga makaburi yao.
49所以, 神的智慧说:‘我要差遣先知和使徒到他们那里去,有的他们要杀害,有的他们要迫害,
49Kwa hiyo, Hekima ya Mungu ilisema hivi: Nitawapelekea manabii na mitume, lakini watawaua baadhi yao, na kuwatesa wengine.
50为要使创世以来众先知所流的血,从亚伯的血起,直到在祭坛和圣所之间受害的撒迦利亚的血为止,都向这一代追讨。’是的,我告诉你们,都要向这一代追讨。
50Matokeo yake ni kwamba kizazi hiki kitaadhibiwa kwa sababu ya damu ya manabii wote iliyomwagika tangu mwanzo wa ulimwengu;
51
51tangu kumwagwa damu ya Abeli mpaka kifo cha Zakariya ambaye walimuua kati ya madhabahu na mahali patakatifu. Naam, hakika kizazi hiki kitaadhibiwa kwa matendo haya.
52你们律法师有祸了!因为你们拿去知识的钥匙,自己不进去,又阻止要进去的人。”
52"Ole wenu ninyi walimu wa Sheria, kwa sababu mmeuficha ule ufunguo wa mlango wa elimu; ninyi wenyewe hamkuingia na mmewazuia waliokuwa wanaingia wasiingie."
53耶稣从那里出来,经学家和法利赛人非常敌视他,质问他很多问题,
53Alipokuwa akitoka pale, wale Mafarisayo na walimu wa Sheria wakaanza kumshambulia vikali na kumsonga kwa maswali mengi
54等机会从他的口中找把柄。
54ili wapate kumnasa kwa maneno yake.