1失羊的比喻(太18:12-14)
1Siku moja, watoza ushuru na wahalifu wengi walikwenda kumsikiliza Yesu.
2法利赛人和经学家,纷纷议论说:“这个人接待罪人,又和他们一起吃饭。”
2Mafarisayo na walimu wa Sheria wakaanza kunung'unika: "Mtazameni mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi, na tena anakula nao."
3耶稣就对他们讲了这个比喻,说:
3Yesu akawajibu kwa mfano:
4“你们中间谁有一百只羊,失去一只,不把九十九只留下在旷野,去寻找那失落的,直到找着呢?
4"Hivi, mtu akiwa na kondoo mia, akigundua kwamba mmoja wao amepotea, atafanya nini? Atawaacha wale tisini na tisa mbugani, na kwenda kumtafuta yule aliyepotea mpaka ampate.
5既找着了,就欢欢喜喜地放在肩上,
5Akimpata, atambeba mabegani kwa furaha.
6回到家里,请朋友邻舍来,对他们说:‘请大家和我一同欢乐,因为我失去的羊已经找到了!’
6Anapofika nyumbani, atawaita rafiki zake akiwaambia, Furahini pamoja nami, kwa sababu nimempata yule kondoo wangu aliyepotea.
7我告诉你们,因为一个罪人悔改,天上也要这样为他欢乐,比为九十九个不用悔改的义人欢乐更大。
7Kadhalika nawaambieni, ndivyo kutakavyokuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya kutubu kwa mwenye dhambi mmoja, kuliko kwa ajili ya watu tisini na tisa wanaojiona kuwa wema, wasiohitaji kutubu.
8失银币的比喻“或是一个女人,有十个银币,失去一个,哪能不点上灯,打扫屋子,细细地找,直到找着呢?
8"Au mwaonaje? Tuseme mwanamke fulani ana sarafu kumi za fedha, akipoteza moja, atafanya nini? Atawasha taa, aifagie nyumba na kuitafuta kwa uangalifu mpaka aipate.
9既找着了,就请朋友邻舍来,说:‘请大家和我一同欢乐,因为我失去的那个银币,已经找到了。’
9Akiipata, atawaita rafiki na jirani zake akisema, Furahini pamoja nami, kwa sababu nimeipata ile sarafu yangu iliyopotea.
10我告诉你们,因为一个罪人悔改, 神的使者也必这样为他欢乐。”
10Kadhalika nawaambieni, ndivyo watakavyofurahi malaika wa Mungu kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja anayetubu."
11浪子的比喻耶稣又说:“某人有两个儿子。
11Yesu akaendelea kusema, "Kulikuwa na mtu mmoja mwenye wana wawili.
12小儿子对父亲说:‘爸爸,请把我应得的家业给我。’父亲就把财产分给他们两兄弟。
12Yule mdogo, alimwambia baba yake: Baba, nipe urithi wangu. Naye akawagawia mali yake.
13过了不多几天,小儿子收拾一切,到远方去了,在那里生活放荡,浪费钱财。
13Baada ya siku chache, yule mdogo aliuza urithi wake, akasafiri na fedha aliyopata, akaenda nchi ya mbali ambako aliitumia ovyo.
14他花尽了一切所有的,那地方又遇上了严重的饥荒,就穷困起来;
14Alipomaliza kutumia kila kitu, kukatokea njaa kali katika nchi ile, naye akaanza kuhangaika.
15于是他去投靠当地的一个居民。那人打发他到田里去放猪,
15Akaomba kazi kwa mwananchi mtu mmoja wa huko naye akampeleka shambani mwake kulisha nguruwe.
16他恨不得吃猪所吃的豆荚,可是没有人给他。
16Alitamani kula maganda waliyokula wale nguruwe, ila hakuna mtu aliyempa kitu.
17他醒悟过来,说:‘我父亲有那么多雇工,又有丰富的食物,我却要在这里饿死吗?
17Alipoanza kupata akili akafikiri: Mbona kuna wafanyakazi wengi wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa?
18我要起来,到我父亲那里去,对他说:爸爸,我得罪了天,也得罪了你,
18Nitarudi kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia.
19不配再称为你的儿子,把我当作一个雇工吧!’
19Sistahili hata kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wa wafanyakazi wako.
20于是他起来往父亲那里去。他还在远处时,他父亲看见了他,就动了慈心,跑过去抱着他,连连与他亲嘴。
20Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu.
21儿子说:‘爸爸,我得罪了天,也得罪了你,不配再称为你的儿子。’
21"Mwanawe akamwambia: Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia. Sistahili hata kuitwa mwanao.
22父亲却吩咐仆人说:‘快把那最好的袍子拿来给他穿,把戒指戴在他手上,把鞋穿在他脚上,
22Lakini baba yake akawaambia watumishi wake: Haraka! Leteni nguo nzuri mkamvike! Mvisheni pete na viatu!
23把肥牛犊牵来宰了,我们要吃喝快乐,
23Mchinjeni ndama mnono; tule kusherehekea!
24因为我这儿子是死而复活、失而又得的。’他们就欢乐起来。
24Kwa sababu huyu mwanangu alikuwa amekufa, kumbe yu mzima alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana. Wakaanza kufanya sherehe.
25“那时,大儿子正在田里。他回来离家不远的时候,听见音乐跳舞的声音,
25"Wakati huo kaka yake alikuwa bado shambani. Alipokuwa akirudi na kukaribia nyumbani akasikia vifijo na ngoma.
26就叫了一个仆人来,问他这是怎么一回事。
26Akamwita mmoja wa watumishi, akamwuliza: Kuna nini?
27仆人说:‘你弟弟回来了,你父亲因为他平安无恙地回来,就宰了肥牛犊。’
27Huyo mtumishi akamwambia: Ndugu yako amerudi nyumbani, na baba yako amemchinjia ndama mnono kwa kuwa amempata akiwa salama salimini.
28大儿子就生气,不肯进去;父亲出来劝他。
28Huyo kijana mkubwa akawaka hasira hata akakataa kuingia nyumbani. Baba yake akatoka nje na kumsihi aingie.
29他对父亲说:‘你看,我服事你这么多年,从来没有违背过你的命令,可是你没有给我一只山羊羔,叫我和朋友一同欢乐。
29Lakini yeye akamjibu: Kumbuka! Miaka yote nimekutumikia, sijavunja amri yako hata mara moja. Umenipa nini? Hujanipa hata mwana mbuzi mmoja nikafanye sherehe pamoja na rafiki zangu!
30但你这个儿子,常常跟娼妓在一起,花尽了你的财产,他一回来,你倒为他宰杀肥牛犊!’
30Lakini mtoto wako huyu aliyekula mali yako pamoja na makahaba, mara tu alipokuja umemchinjia yule ndama mnono.
31父亲对他说:‘孩子,你常跟我在一起,我的一切都是你的。
31Baba yake akamjibu: Mwanangu, wewe uko pamoja nami siku zote, na kila nilicho nacho ni chako.
32只是因为你这个弟弟是死而复活、失而又得的,我们应该欢喜快乐。’”
32Ilitubidi kufanya sherehe na kufurahi, kwa sababu huyu ndugu yako alikuwa amekufa, kumbe yu mzima; alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana."