聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Luke

17

1饶恕、信心、服事等教训(太18:6-7、21-22;可9:42)
1Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Haiwezekani kabisa kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha.
2就算拿一块大磨石拴在他的颈项上,把他沉在深海里,比他使这小子中的一个犯罪还好。
2Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutoswa baharini, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa.
3你们应当谨慎。如果你弟兄得罪你,就劝戒他;他若懊悔,就饶恕他。
3Jihadharini! Kama ndugu yako akikukosea, mwonye; akitubu, msamehe.
4如果他一天七次得罪你,又七次回转,对你说:‘我懊悔了!’你总要饶恕他。”
4Na kama akikukosea mara saba kwa siku, na kila mara akarudi kwako akisema Nimetubu, lazima umsamehe."
5使徒对主说:“请你加添我们的信心。”
5Mitume wakamwambia Bwana, "Utuongezee imani."
6主说:“如果你们有信心像一粒芥菜种,就是对这棵桑树说:‘拔起根来,栽到海里去!’它也必听从你们。
6Naye Bwana akajibu, "Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: Ng'oka ukajipandikize baharini, nao ungewatii.
7“你们中间谁有仆人去耕地或是放羊,从田里回来,你就对他说:‘快过来坐下吃饭’;
7"Tuseme mmoja wenu ana mtumishi ambaye analima shambani au anachunga kondoo. Je, anaporudi kutoka shambani, atamwambia: Haraka, njoo ule chakula?
8而不对他说:‘给我预备晚餐,束起腰来服事我,等我吃喝完了,你才吃喝’呢?
8La! Atamwambia: Nitayarishie chakula, ujifunge tayari kunitumikia mpaka nitakapomaliza kula na kunywa, ndipo nawe ule na unywe.
9仆人作了所吩咐的事,主人还谢谢他吗?
9Je utamshukuru huyo mtumishi kwa sababu ametimiza aliyoamriwa?
10你们也是这样,作完一切吩咐你们的事,应该说:‘我们是无用的仆人,我们只作了应分作的。’”
10Hali kadhalika na ninyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni: Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa kufanya."
11治好十个痲风病人耶稣往耶路撒冷去,经过撒玛利亚和加利利的边境。
11Yesu akiwa safarini kwenda Yerusalemu alipitia mipakani mwa Samaria na Galilaya.
12他走进一个村庄,有十个痲风病人迎面而来,远远地站着,
12Alipokuwa anaingia katika kijiji kimoja, watu kumi wenye ukoma walikutana naye, wakasimama kwa mbali.
13大声说:“主耶稣啊,可怜我们吧!”
13Wakapaza sauti wakisema, "Yesu Mwalimu, tuonee huruma!"
14他看见了,就对他们说:“你们去给祭司检查吧。”他们去的时候就洁净了。
14Alipowaona akawaambia, "Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani." Basi, ikawa walipokuwa wanakwenda, wakatakasika.
15内中有一个人见自己已经好了,就回来大声颂赞 神,
15Mmoja wao alipoona kwamba ameponywa alirudi akimtukuza Mungu kwa sauti kubwa.
16在耶稣脚前把脸伏在地上感谢他。他是一个撒玛利亚人。
16Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru. Huyo alikuwa Msamaria.
17耶稣说:“洁净了的不是有十个人吗?那九个在哪里?
17Hapo Yesu akasema, "Je, si watu kumi walitakaswa? Wale tisa wako wapi?
18除了这外族人,再没有一个回来颂赞 神吗?”
18Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuza Mungu ila tu huyu mgeni?"
19耶稣就对他说:“起来,走吧,你的信使你痊愈了。”
19Halafu akamwambia huyo mtu, "Simama, uende zako; imani yako imekuponya."
20 神的国降临的情形(太24:37-41)法利赛人问耶稣:“ 神的国什么时候来到呢?”他回答:“ 神的国来到,是眼睛看不见的。
20Wakati mmoja, Mafarisayo walimwuliza Yesu, "Ufalme wa Mungu utakuja lini?" Naye akawajibu, "Ufalme wa Mungu hauji kwa namna itakayoweza kuonekana.
21人不能说:‘看哪!在这里’,或说:‘在那里’;因为 神的国就在你们里面。”
21Wala hakuna atakayeweza kusema, Uko hapa, au Uko pale. Kwa kweli Ufalme wa Mungu uko kati yenu."
22他又对门徒说:“日子将到,你们渴望看见人子的一个日子,却见不到。
22Halafu akawaambia wanafunzi wake, "Siku zinakuja ambapo mtatamani kuona mojawapo ya siku za Mwana wa Mtu, lakini hamtaiona.
23有人会对你们说:‘看哪,在那里;看哪,在这里!’你们不要出去,也不要追随他们。
23Na watu watawaambieni: Tazameni yuko hapa; ninyi msitoke wala msiwafuate.
24电光怎样从天这边一闪,直照到天那边,人子在他的日子也是这样。
24Kwa maana kama vile umeme unavyotokea ghafla na kuangaza anga upande mmoja hadi mwingine, ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa siku yake.
25但他必须先受许多苦,被这个世代弃绝。
25Lakini kabla ya hayo, itambidi ateseke sana na kukataliwa na kizazi hiki.
26挪亚的时代怎样,人子的时代也是怎样。
26Kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Mtu.
27当时人们吃喝嫁娶,直到挪亚进入方舟的那一天,洪水来了,把他们全都灭掉。
27Watu waliendelea kula na kunywa, kuoa na kuolewa mpaka wakati ule Noa alipoingia katika safina. Gharika ikatokea na kuwaangamiza wote.
28在罗得的时代也是这样,人们吃喝买卖,耕种建造,
28Itakuwa kama ilivyotokea wakati wa Loti. Watu waliendelea kula na kunywa, kununua na kuuza, kupanda mbegu na kujenga.
29直到罗得离开所多玛的那一天,火与硫磺从天上降下来,把他们全都灭掉。
29Lakini siku ile Loti alipoondoka Sodoma, moto na kiberiti vikanyesha kama mvua kutoka mbinguni na kuwaangamiza wote.
30人子显现的日子也是这样。
30Ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Mtu atakapofunuliwa.
31当那日,人在房顶上,器具在屋里,不要下来拿;在田里的,照样不要回家。
31"Siku hiyo, yeyote atakayekuwa juu ya paa asishuke nyumbani kuchukua mali yake. Kadhalika, naye atakayekuwa shambani asirudi nyuma.
32应当记着罗得的妻子的教训。
32Kumbukeni yaliyompata mke wa Loti.
33凡是想保全生命的,必丧掉生命;凡是牺牲生命的,却必保全生命。
33Yeyote anayetaka kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na yeyote anayeipoteza, ataiokoa.
34我告诉你们,当那夜,两个人在一张床上,一个被接去,一个被撇下。
34Nawaambieni, siku ile usiku watu wawili watakuwa wanalala pamoja, mmoja atachukuliwa na yule mwingine ataachwa.
35两个女人一起推磨,一个被接去,一个被撇下。”
35Wanawake wawili watakuwa wakisaga nafaka pamoja; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa."
36(有些抄本有第36节:“两个人在田里,一个被接去,一个撇下来。”)
36Watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.
37门徒问耶稣:“主啊,这些事会在哪里发生呢?”主说:“尸首在哪里,鹰也会聚集在哪里。”
37Hapo wakamwuliza, "Ni wapi Bwana?" Naye akawaambia, "Ulipo mzoga, ndipo tai watakapokusanyikia."