1安息日的主(太12:1-8;可2:23-28)
1Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano, na wanafunzi wake wakaanza kukwanyua masuke ya ngano, wakaondoa punje zake kwa mikono, wakala.
2有几个法利赛人说:“你们为什么作安息日不可作的事呢?”
2Baadhi ya Mafarisayo wakawauliza, "Mbona mnafanya jambo ambalo si halali siku ya Sabato?"
3耶稣回答:“大卫和跟他在一起的人,在饥饿的时候所作的,你们没有念过吗?
3Yesu akawajibu, "Je, hamjasoma jinsi alivyofanya Daudi pamoja na wenzake wakati walipokuwa na njaa?
4他不是进了 神的殿,吃了陈设饼,也给跟他在一起的人吃吗?这饼除了祭司以外,别的人是不可以吃的。”
4Yeye aliingia ndani ya nyumba ya Mungu, akachukua ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu, akala na kuwapa wenzake. Kisheria, ni makuhani tu peke yao ndio walioruhusiwa kula mikate hiyo."
5他又对他们说:“人子是安息日的主。”
5Hivyo akawaambia, "Mwana wa Mtu ni Bwana wa Sabato."
6治好手枯的人(太12:9-14;可3:1-6)另一个安息日,耶稣进入会堂教导人,在那里有一个人,右手枯干,
6Siku nyingine ya Sabato, Yesu aliingia katika sunagogi, akafundisha. Mle ndani mlikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kuume ulikuwa umepooza.
7经学家和法利赛人要看他会不会在安息日治病,好找把柄控告他。
7Walimu wa Sheria na Mafarisayo walitaka kupata kisingizio cha kumshtaki Yesu na hivyo wakawa wanangojea waone kama angemponya mtu siku ya Sabato.
8耶稣知道他们的意念,就对那一只手枯干了的人说:“起来,站在当中!”那人就起来站着。
8Lakini Yesu alijua mawazo yao, akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, "Inuka, simama katikati." Yule mtu akaenda akasimama katikati.
9耶稣对他们说:“我问你们:在安息日哪一样是可以作的呢:作好事还是坏事?救命还是害命?”
9Kisha Yesu akawaambia, "Nawaulizeni, je, ni halali siku ya Sabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au kuyaangamiza?"
10他环视周围所有的人,就对那人说:“伸出你的手来!”他把手一伸,手就复原了。
10Baada ya kuwatazama wote waliokuwa pale, akamwambia yule mtu, "Nyosha mkono wako." Naye akafanya hivyo, na mkono wake ukawa mzima tena.
11他们却大怒,彼此商议怎样对付耶稣。
11Lakini wao wakakasirika sana, wakajadiliana jinsi ya kumtendea Yesu maovu.
12选立十二使徒(太10:2-4;可3:16-19。参徒1:13)在那些日子,有一次耶稣出去到山上祷告,整夜祷告 神。
12Siku moja Yesu alikwenda mlimani kusali, akakesha huko usiku kucha akimwomba Mungu.
13天亮以后,他把门徒叫来,从他们中间挑选了十二个人,称他们为使徒,
13Kesho yake aliwaita wanafunzi wake, na miongoni mwao akachagua kumi na wawili ambao aliwaita mitume:
14就是西门(又给他起名叫彼得),和他弟弟安得烈,以及雅各、约翰、腓力、巴多罗迈、
14Simoni (ambaye Yesu alimpa jina Petro) na Andrea ndugu yake, Yakobo na Yohane, Filipo na Bartholomayo,
15马太、多马、亚勒腓的儿子雅各、称为激进派的西门、
15Mathayo na Thoma, Yakobo wa Alfayo na Simoni (aliyeitwa Zelote),
16雅各的儿子犹大,和出卖主的加略人犹大。
16Yuda wa Yakobo na Yuda Iskarioti ambaye baadaye alikuwa msaliti.
17论福论祸(太5:1-12)耶稣和他们下了山,站在平地上,有一大群门徒同他在一起,又有一大批从犹太全地、耶路撒冷和推罗、西顿海边来的人。
17Baada ya kushuka mlimani pamoja na mitume, Yesu alisimama mahali palipokuwa tambarare. Hapo palikuwa na kundi kubwa la wanafunzi wake na umati wa watu waliotoka pande zote za Yudea na Yerusalemu na pwani ya Tiro na Sidoni. Wote walifika kumsikiliza Yesu na kuponywa magonjwa yao.
18他们要听他讲道,也要他们的疾病得医好。还有一些被污灵缠扰的也痊愈了。
18Aliwaponya pia wote waliokuwa wanasumbuliwa na pepo wachafu.
19群众都设法摸他,因为有能力从他身上出来,治好众人。
19Watu wote walitaka kumgusa, kwa maana nguvu ilikuwa inatoka ndani yake na kuwaponya wote.
20耶稣抬头看着门徒,说:“贫穷的人有福了,因为 神的国是你们的。
20Yesu akawageukia wanafunzi wake, akasema: "Heri ninyi mlio maskini, maana Ufalme wa Mungu ni wenu.
21饥饿的人有福了,因为你们要得饱足。哀哭的人有福了,因为你们将要喜乐。
21Heri ninyi mnaosikia njaa sasa, maana baadaye mtashiba. Heri ninyi mnaolia sasa, maana baadaye mtacheka kwa furaha.
22世人为人子的缘故憎恨你们、排斥你们、辱骂你们,弃绝你们的名好像弃绝恶物,你们就有福了。
22"Heri yenu ninyi iwapo watu watawachukia, watawatenga, watawatukana na kuwaharibieni jina kwa ajili ya Mwana wa Mtu!
23那时你们应该欢喜跳跃,因为你们在天上的赏赐是大的,他们的祖先对待先知也是这样。
23Wakati hayo yatakapotokea, furahini na kucheza, maana hakika tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Kwa maana wazee wao waliwatendea manabii vivyo hivyo.
24“然而你们富有的人有祸了,因为你们已经得了你们的安慰。
24Lakini ole wenu ninyi mlio matajiri, maana mmekwisha pata faraja yenu.
25你们饱足的人有祸了,因为你们将要饥饿。你们喜乐的人有祸了,因为你们将要痛哭。
25Ole wenu ninyi mnaoshiba sasa, maana baadaye mtasikia njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka kwa furaha sasa, maana baadaye mtaomboleza na kulia.
26人都说你们好的时候,你们就有祸了,因为你们的祖先对待假先知也是这样。
26Ole wenu ninyi iwapo watu wote wanawasifu, maana wazee wao waliwafanyia manabii wa uongo vivyo hivyo.
27当爱仇敌(太5:39-42)“只是我告诉你们听道的人:当爱你们的仇敌,善待恨你们的人。
27"Lakini nawaambieni ninyi mnaonisikiliza: wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale wanaowachukieni.
28咒诅你们的,要为他们祝福,凌辱你们的,要为他们祷告。
28Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya.
29有人打你一边的脸,把另一边也转给他打;有人拿你的外衣,连内衣也让他拿去。
29Mtu akikupiga shavu moja mgeuzie na la pili. Mtu akikunyang'anya koti lako mwachie pia shati lako.
30向你求的,就给他;有人拿去你的东西,不用再要回来。
30Yeyote anayekuomba mpe, na mtu akikunyang'anya mali yako usimtake akurudishie.
31你们愿意人怎样待你们,你们就应当怎样待人。
31Watendeeni wengine kama mnavyotaka wawatendee ninyi.
32如果单爱那些爱你们的人,那有什么好处呢?罪人也爱那些爱他们的人。
32"Na ikiwa mnawapenda tu wale wanaowapenda ninyi, je, mtapata tuzo gani? Hakuna! Kwa maana hata wenye dhambi huwapenda wale wanaowapenda wao.
33如果只善待那些善待你们的人,那有什么好处呢?罪人也会这样行。
33Tena, kama mkiwatendea mema wale tu wanaowatendeeni mema, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo!
34如果借给人,又指望向人收回,那有什么好处呢?罪人也借给罪人,要如数收回。
34Na kama mnawakopesha wale tu mnaotumaini watawalipeni, je, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao ili warudishiwe kima kilekile!
35你们要爱仇敌,善待他们;借出去,不要指望偿还;这样你们的赏赐就大了,你们也必作至高者的儿子,因为 神自己也宽待忘恩的和恶人。
35Ila nyinyi wapendeni adui zenu, na kuwatendea mema; kopesheni bila kutazamia malipo, na tuzo lenu litakuwa kubwa, nanyi mtakuwa watoto wa Mungu aliye juu. Kwa maana yeye ni mwema kwa wale wasio na shukrani na walio wabaya.
36你们要仁慈像你们的父仁慈一样。
36Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma.
37不可判断(太7:1-5)“你们不要判断人,就必不受判断;不要定人的罪,就必不被定罪;要饶恕人,就必蒙饶恕;
37"Msiwahukumu wengine, nanyi hamtahukumiwa; msiwalaumu wengine, nanyi hamtalaumiwa; wasameheni wengine, nanyi mtasamehewa.
38要给人,就必有给你们的;并且要用十足的升斗,连按带摇,上尖下流地倒在你们怀里;因为你们用什么升斗量给人,就必用什么升斗量给你们。”
38Wapeni wengine wanavyohitaji, nanyi mtapewa. Naam, mtapokea mikononi mwenu kipimo kilichojaa, kikashindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika. Kwa maana kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho ambacho Mungu atatumia kwenu."
39耶稣又用比喻对他们说:“瞎子怎能给瞎子领路呢?两个人不都要掉在坑里吗?
39Akawaambia mfano huu: "Je, kipofu anaweza kumwongoza kipofu mwenzake? La! Wote wataanguka shimoni.
40学生不能胜过老师,所有学成的,不过和老师一样。
40Mwanafunzi hamshindi mwalimu wake, lakini kila mwanafunzi akisha hitimu huwa kama mwalimu wake.
41为什么看得见你弟兄眼中的木屑,却想不到自己眼中的梁木呢?
41Unawezaje kukiona kibanzi kilicho katika jicho la mwenzio, usione boriti iliyo katika jicho lako mwenyewe?
42你不看见自己眼中的梁木,怎能对你弟兄说:‘弟兄,容我除去你眼中的木屑’呢?伪君子啊!先去掉自己眼中的梁木,才能看得清楚,好去掉弟兄眼中的木屑。
42Au, unawezaje kumwambia mwenzako, Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi katika jicho lako, na huku huioni boriti iliyoko katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako, na hivyo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho katika jicho la ndugu yako.
43坏树不能结好果子(太7:16-20,12:33-35)“因为好树不能结坏果子,坏树不能结好果子。
43"Mti mwema hauzai matunda mabaya, wala mti mbaya hauzai matunda mazuri.
44凭着果子就可以认出树来。人不能从荆棘上采无花果,也不能从蒺藜里摘葡萄。
44Watu huutambua mti kutokana na matunda yake. Ni wazi kwamba watu hawachumi tini katika michongoma, wala hawachumi zabibu katika mbigili.
45良善的人从心中所存的良善发出良善,邪恶的人从心中所存的邪恶发出邪恶;因为心中所充满的,口里就说出来。
45Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina bora iliyo moyoni mwake; na mtu mbaya hutoa yaliyo mabaya katika hazina mbaya iliyo moyoni mwake, kwa maana mtu huongea kutokana na yale yaliyojaa moyoni mwake.
46听道要行道(太7:24-27)“你们为什么称呼我‘主啊!主啊!’却不遵行我的吩咐呢?
46"Mbona mwaniita Bwana, Bwana, na huku hamtimizi yale ninayosema?
47每一个到我跟前,听我的话并且去行的,我要指示你们他像什么人。
47Nitawapeni mfano unaofaa kuonyesha alivyo yeyote yule anayekuja kwangu, akasikia maneno yangu na kuyatimiza:
48他像一个人建造房屋,挖深了地,把根基建在磐石上。大水泛滥的时候,急流冲击那房屋,不能使它动摇,因为它建造得好。
48Huyo anafanana na mtu ajengaye nyumba, ambaye amechimba chini na kuweka msingi wake juu ya mwamba; kukatokea mafuriko ya mto, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, lakini haukuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa imara.
49但那听见而不遵行的,就像人在地上建屋,没有根基,急流一冲,就立刻倒塌,毁坏得很厉害。”
49Lakini yeyote anayesikia maneno yangu lakini asifanye chochote, huyo anafanana na mtu aliyejenga nyumba juu ya udongo, bila msingi. Mafuriko ya mto yakatokea, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, ikaanguka na kuharibika kabisa!"