1跟从耶稣的妇女
1Baada ya hayo, Yesu alipitia katika miji na vijiji akitangaza Habari Njema za Ufalme wa Mungu. Wale kumi na wawili waliandamana naye.
2还有几个蒙了医治、脱离污鬼与疾病的妇女,其中有称为抹大拉的马利亚,曾有七个鬼从她身上赶出来;
2Pia wanawake kadhaa ambao Yesu alikuwa amewatoa pepo wabaya na kuwaponya magonjwa, waliandamana naye. Hao ndio akina Maria (aitwaye Magdalene), ambaye alitolewa pepo wabaya saba;
3有希律的管家古撒的妻子约亚拿,又有苏珊娜,和许多别的妇女,她们都用自己的财物供给耶稣和门徒。
3Yoana, mke wa Kuza, mfanyakazi mkuu wa Herode; Susana na wengine kadhaa. Hao wanawake walikuwa wakiwatumikia kwa mali yao wenyewe.
4撒种的比喻(太13:2-9;可4:1-9)当时有许多人聚在一起,还有人从各城来到耶稣那里,他就用比喻说:
4Kundi kubwa la watu lilikuwa linakusanyika, na watu walikuwa wanamjia Yesu kutoka kila mji. Naye akawaambia mfano huu:
5“有一个撒种的出去撒种,撒的时候,有的落在路旁,被人践踏,或给空中的小鸟吃掉。
5"Mpanzi alikwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akipanda zile mbegu, nyingine zilianguka njiani, na wapita njia wakazikanyaga, na ndege wakazila.
6有的落在石头地上,一长出来就枯萎了,因为得不着滋润。
6Nyingine zilianguka penye mawe, na baada ya kuota zikanyauka kwa kukosa maji.
7有的落在荆棘丛中,荆棘也一齐生长,把它挤住了。
7Nyingine zilianguka kati ya miti ya miiba. Ile miti ya miiba ilipoota ikazisonga.
8有的落在好土里,就生长起来,结出百倍的果实。”他说了这些话,就大声说:“有耳可听的,就应当听!”
8Nyingine zilianguka katika udongo mzuri, zikaota na kuzaa asilimia mia." Baada ya kusema hayo, akapaaza sauti, akasema, "Mwenye masikio na asikie!"
9用比喻的目的(太13:10-17;可4:10-12)门徒问他这比喻是什么意思。
9Wanafunzi wake wakamwuliza Yesu maana ya mfano huo.
10他说:“ 神的国的奥秘,只给你们知道,对别人就用比喻,叫他们看却看不见,听却听不明白。
10Naye akajibu, "Ninyi mmejaliwa kujua siri za Ufalme wa Mungu, lakini hao wengine sivyo; ila hao huambiwa kwa mifano, ili wakitazama wasiweze kuona, na wakisikia wasifahamu.
11解释撒种的比喻(太13:18-23;可4:13-20)“这比喻是说,种子是 神的道,
11"Basi, maana ya mfano huu ni hii: mbegu ni neno la Mungu.
12那落在路旁的,就是人听了,魔鬼随即来到,从他们心里把道夺去,恐怕他们相信就得救了。
12Zile zilizoanguka njiani zinaonyesha watu wale wanaosikia lile neno, halafu Ibilisi akaja na kuliondoa mioyoni mwao wasije wakaamini na hivyo wakaokoka.
13那落在石头地上的,就是人听了,欢欢喜喜地接受,但是没有根,不过是暂时相信,一旦遭遇试炼,就倒退了。
13Zile zilizoanguka penye mawe zinaonyesha watu wale ambao wanaposikia juu ya lile neno hulipokea kwa furaha. Hata hivyo, kama zile mbegu, watu hao hawana mizizi maana husadiki kwa kitambo tu, na wanapojaribiwa hukata tamaa.
14那落在荆棘里的,就是人听了,走开以后,被今世的忧虑、财富和宴乐挤住了,结不出成熟的子粒来。
14Zile zilizoanguka kwenye miti ya miiba ni watu wale wanaosikia lile neno, lakini muda si muda, wanapokwenda zao, husongwa na wasiwasi, mali na anasa za maisha, na hawazai matunda yakakomaa.
15但那落在好土里的,就是人用诚实良善的心来听,把道持守住,忍耐着结出果实。
15Na zile zilizoanguka kwenye udongo mzuri ndio watu wale wanaolisikia lile neno, wakalizingatia kwa moyo mwema na wa utii. Hao huvumilia mpaka wakazaa matunda.
16隐藏的事终必显露(可4:21-25)“没有人点灯用器皿盖上,或放在床底下,而是放在灯台上,叫进来的人都看得见光。
16"Watu hawawashi taa na kuifunika kwa chombo au kuiweka mvunguni. Lakini huiweka juu ya kinara ili watu wanapoingia ndani wapate kuona mwanga.
17因为没有什么隐藏的事不被显明,也没有什么掩盖的事不被人知道而暴露出来。
17"Chochote kilichofichwa kitafichuliwa na siri yoyote itagunduliwa na kujulikana hadharani.
18所以你们应当留心怎样听,因为凡是有的,还要给他;凡是没有的,连他自以为有的,也要拿去。”
18"Kwa hiyo, jihadharini jinsi mnavyosikia; maana aliye na kitu ataongezewa, lakini yule asiye na kitu, hata kile anachodhani kuwa anacho, kitachukuliwa."
19谁是耶稣的母亲和弟兄(太12:46-50;可3:31-35)耶稣的母亲和弟弟来到他那里,因为人多,不能到他跟前。
19Hapo mama na ndugu zake Yesu wakamjia, lakini hawakuweza kumkaribia kwa sababu ya umati wa watu.
20有人转告耶稣:“你母亲和弟弟站在外面要见你。”
20Yesu akapewa habari kwamba mama na ndugu zake walikuwa nje, wanataka kumwona.
21他回答他们:“听了 神的道而遵行的人,才是我的母亲,我的弟兄。”
21Lakini Yesu akawaambia watu wote, "Mama yangu na ndugu zangu ni wale wanaolisikia neno la Mungu na kulishika."
22平静风浪(太8:23-27;可4:35-41)有一天,耶稣和门徒上了船,他对他们说:“我们渡到海那边去吧。”他们就开了船。
22Siku moja, Yesu alipanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, "Tuvuke ziwa twende mpaka ng'ambo." Basi, wakaanza safari.
23船行的时候,他睡着了。海上忽然起了狂风,他们全身湿透,非常危险。
23Walipokuwa wanasafiri kwa mashua, Yesu alishikwa na usingizi, akalala. Dhoruba kali ikaanza kuvuma, maji yakaanza kuingia ndani ya mashua, wakawa katika hatari.
24门徒来叫醒耶稣,说:“主啊!主啊!我们没命了!”他醒过来,斥责风浪,风浪就止息、平静了。
24Wale wanafunzi wakamwendea Yesu, wakamwamsha wakisema, "Bwana, Bwana! Tunaangamia!" Yesu akaamka, akaikemea dhoruba na mawimbi, navyo vikatulia, kukawa shwari.
25耶稣对他们说:“你们的信心在哪里?”他们又惧怕、又希奇,彼此说:“这到底是谁?他吩咐风浪,连风浪也听从他。”
25Kisha akawaambia, "Iko wapi imani yenu?" Lakini wao walishangaa na kuogopa huku wakiambiana, "Huyu ni nani basi, hata anaamuru dhoruba na mawimbi, navyo vinamtii?"
26治好鬼附的格拉森人(太8:28-34;可5:1-20)船到了格拉森人的地区,正在加利利对面,
26Wakaendelea na safari, wakafika pwani ya nchi ya Wagerase inayokabiliana na Galilaya, ng'ambo ya ziwa.
27耶稣一上岸,就有城里一个被鬼附着的人,迎面而来。这人已经很久不穿衣服,不住在家里,只住在坟墓里。
27Alipokuwa anashuka pwani, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo alimjia kutoka mjini. Kwa muda mrefu mtu huyo, hakuwa anavaa nguo, wala hakuwa anaishi nyumbani bali makaburini.
28他一见耶稣,就俯伏喊叫,大声说:“至高 神的儿子耶稣,我跟你有什么关系呢?求你不要使我受苦。”
28Alipomwona Yesu, alipiga kelele na kujitupa chini mbele yake, na kusema kwa sauti kubwa "We, Yesu Mwana wa Mungu Aliye Juu una shauri gani nami? Ninakusihi usinitese!"
29因为耶稣已经吩咐这污灵从那人身上出来。原来这污灵屡次抓住那人;那人被铁链和脚链捆锁,而且有人看管,他竟挣断锁链,被鬼赶入旷野。
29Alisema hivyo kwa kuwa Yesu alikwishamwambia huyo pepo mchafu amtoke mtu huyo. Pepo huyo mchafu alikuwa anamvamia mtu huyo mara nyingi, na ingawa watu walimweka ndani na kumfunga kwa minyororo na pingu, lakini kila mara alivivunja vifungo hivyo, akakimbizwa na pepo huyo mchafu hadi jangwani.
30耶稣问他:“你叫什么名字?”他说:“群。”因为进到那人里面的鬼很多。
30Basi, Yesu akamwuliza, "Jina lako nani?" Yeye akajibu, "Jina langu ni Jeshi" --kwa sababu pepo wengi walikuwa wamempagaa.
31他们求耶稣,不要赶他们进入无底坑。
31Hao pepo wakamsihi asiwaamuru wamtoke na kwenda kwenye shimo lisilo na mwisho.
32那里有一大群猪正在山上吃东西。他们求耶稣准他们进入猪群。耶稣准许了,
32Kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakilisha mlimani. Basi, hao pepo wakamsihi awaruhusu wawaingie. Naye Yesu akawapa ruhusa.
33鬼就从那人身上出来,进入猪群,猪群闯下山崖,掉在海里淹死了。
33Kwa hiyo pepo hao wakamtoka yule mtu, wakawaingia wale nguruwe, nao wakaporomoka kwenye ule mteremko mkali, wakatumbukia ziwani, wakazama majini.
34放猪的看见所发生的事就逃跑,到城里和各乡村把这事传开。
34Wale wachungaji walipoona yote yaliyotokea walikimbia, wakaenda kuwapa watu habari, mjini na mashambani.
35众人就出来看发生了什么事。来到耶稣那里,看见鬼已经离开的那人,穿着衣服,神志清醒,坐在耶稣脚前,他们就害怕。
35Watu wakaja kuona yaliyotokea. Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mtu aliyetokwa na pepo ameketi karibu na Yesu, amevaa nguo, ana akili zake, wakaogopa.
36当时看见的人,把被鬼附过的人怎样得到医治,说给他们听。
36Wale watu walioshuhudia tukio hilo waliwaeleza hao jinsi yule mtu alivyoponywa.
37格拉森一带的人,都要求耶稣离开他们,因为他们大大惧怕。他就上船回去了。
37Wakazi wa nchi ya Gerase walishikwa na hofu kubwa. Kwa hiyo wakamwomba Yesu aondoke, aende zake. Hivyo Yesu alipanda tena mashua, akaondoka.
38鬼已经离开的那人求耶稣,要跟他在一起;但耶稣打发他回去,说:
38Yule mtu aliyetokwa na wale pepo akamsihi aende pamoja naye. Lakini Yesu hakumruhusu, bali akamwambia,
39“你回家去,述说 神为你作了怎样的事。”他就走遍全城,传讲耶稣为他作了怎样的事。
39"Rudi nyumbani ukaeleze yote Mungu aliyokutendea." Basi, yule mtu akaenda akitangaza kila mahali katika mji ule mambo yote Yesu aliyomtendea.
40治好血漏病的女人(太9:18-22;可5:21-34)耶稣回来的时候,众人欢迎他,因为大家都在等着他。
40Yesu aliporudi upande mwingine wa ziwa, kundi la watu lilimkaribisha, kwa maana wote walikuwa wanamngojea.
41那时,有一个人来了,名叫叶鲁,他是一位会堂主管。他俯伏在耶稣脚前,求他往他家里去,
41Hapo akaja mtu mmoja aitwaye Yairo, ofisa wa sunagogi. Alijitupa miguuni pa Yesu, akamwomba aende nyumbani kwake,
42因为他的独生女,约十二岁,快要死了。耶稣去的时候,群众拥挤着他。
42kwa kuwa binti yake wa pekee, mwana wa pekee mwenye umri wa miaka kumi na miwili, alikuwa mahututi. Yesu alipokuwa akienda, watu wakawa wanamsonga kila upande.
43有一个女人,患了十二年的血漏病,在医生手里花尽了全部养生的(有些抄本无“在医生手里花尽了全部养生的”一句),没有一个能医好她。
43Kulikuwa na mwanamke mmoja kati ya lile kundi la watu, ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, ingawa alikuwa amekwisha tumia mali yake yote kwa waganga, hakuna aliyefaulu kumponya.
44她从后面挤来,一摸耶稣的衣裳繸子,血就立刻止住。
44Huyo mwanamke alimfuata Yesu nyuma, akagusa pindo la vazi lake. Papo hapo akaponywa ugonjwa wake wa kutokwa damu.
45耶稣说:“摸我的是谁?”众人都不承认。彼得说:“主啊,众人都拥挤着你。”
45Yesu akasema, "Ni nani aliyenigusa?" Wote wakasema kwamba hapakuwa na mtu aliyemgusa. Naye Petro akasema, "Mwalimu, umati wa watu umekuzunguka na kukusonga!"
46耶稣说:“必定有人摸我,因为我觉得有能力从我身上出去。”
46Lakini Yesu akasema, "Kuna mtu aliyenigusa, maana nimehisi nguvu imenitoka."
47那女人见不能隐瞒,就战战兢兢地过来,向他俯伏,把摸他的缘故,和怎样立刻得到医治,在众人面前说出来。
47Yule mwanamke alipoona kwamba hawezi kujificha, akajitokeza akitetemeka kwa hofu, akajitupa mbele ya Yesu. Hapo akaeleza mbele ya wote kisa cha kumgusa Yesu na jinsi alivyoponyeshwa mara moja.
48耶稣对她说:“女儿,你的信使你痊愈了,平安地去吧!”
48Yesu akamwambia, "Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani."
49使女孩复活(太9:23-26;可5:35-43)耶稣还在说话的时候,有人从会堂主管家里来,说:“你的女儿死了,不必再劳动老师了。”
49Alipokuwa bado akiongea, Yairo akaletewa habari kutoka nyumbani: "Binti yako ameshakufa, ya nini kumsumbua Mwalimu zaidi?"
50耶稣听见就对他说:“不要怕,只要信,她必得痊愈。”
50Yesu aliposikia hayo akamwambia Yairo, "Usiogope; amini tu, naye atapona."
51到了那家,除了彼得、约翰、雅各和女孩的父母以外,他不准任何人同他进屋里去。
51Alipofika nyumbani hakumruhusu mtu kuingia ndani pamoja naye, isipokuwa Petro, Yohane, Yakobo na wazazi wa huyo msichana.
52众人都在痛哭哀号,他说:“不要哭!她不是死了,而是睡着了。”
52Watu wote walikuwa wakilia na kuomboleza kwa ajili yake. Lakini Yesu akawaambia, "Msilie, kwa maana mtoto hajafa, amelala tu!"
53他们明知女孩已经死了,就嘲笑他。
53Nao wakamcheka kwa sababu walijua kwamba alikuwa amekufa.
54他进去拉着女孩的手,叫她说:“孩子,起来!”
54Lakini Yesu akamshika mkono akasema, "Mtoto amka!"
55她的灵魂回来了,她就立刻起来。耶稣吩咐给她东西吃。
55Roho yake ikamrudia, akaamka mara. Yesu akaamuru wampe chakula.
56她父母非常惊奇。耶稣嘱咐他们不要把他所作的事告诉人。
56Wazazi wake walishangaa, lakini Yesu akawaamuru wasimwambie mtu yeyote hayo yaliyotendeka.