聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Matthew

18

1天国里谁最大(可9:33-37;路9:46-48)
1Wakati ule wanafunzi walimwendea Yesu, wakamwuliza, "Ni nani aliye mkuu katika Ufalme wa mbinguni?"
2耶稣叫了一个小孩子站在他们当中,说:
2Yesu akamwita mtoto mmoja, akamsimamisha kati yao,
3“我实在告诉你们,如果你们不回转,变成像小孩子一样,一定不能进天国。
3kisha akasema, "Nawaambieni kweli, msipogeuka na kuwa kama watoto, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.
4所以,凡谦卑像这小孩子的,他在天国里是最大的。
4Yeyote anayejinyenyekesha kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkubwa katika Ufalme wa mbinguni.
5凡因我的名接待一个这样的小孩子的,就是接待我;
5Yeyote anayemkaribisha mtoto mmoja kama huyu kwa jina langu, ananikaribisha mimi.
6但无论谁使一个信我的小弟兄犯罪,倒不如拿一块大磨石拴在他的颈项上,把他沉在深海里。
6"Yeyote atakayemkosesha mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini, ingekuwa afadhali afungwe shingoni jiwe kubwa la kusagia na kuzamishwa kwenye kilindi cha bahari.
7坚拒犯罪(可9:42-48;路17:1-2)“这世界有祸了,因为充满使人犯罪的事。这些事是免不了的,但那使人犯罪的有祸了!
7Ole wake ulimwengu kwa sababu ya vikwazo vinavyowaangusha wengine. Vikwazo hivyo ni lazima vitokee lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha.
8如果你的一只手或一只脚使你犯罪,就把它砍下来丢掉;你一只手或一只脚进永生,总比有两只手或两只脚被投进永火里好。
8"Kama mkono au mguu wako ukikukosesha, ukate na kuutupa mbali nawe. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima bila mkono au mguu, kuliko kutupwa katika moto wa milele ukiwa na mikono miwili na miguu yako miwili.
9如果你的一只眼睛使你犯罪,就把它挖出来丢掉;你一只眼睛进永生,总比有两只眼睛被投进地狱的火里好。
9Na kama jicho lako likikukosesha, ling'oe na kulitupa mbali nawe. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa chongo, kuliko kutupwa katika moto wa Jehanamu ukiwa na macho yako yote mawili.
10迷羊的比喻(路15:4-7)“你们要小心,不要轻视这些小弟兄中的一个。我告诉你们,他们的使者在天上,常常见到我天父的面。
10"Jihadharini! Msimdharau mmojawapo wa wadogo hawa. Nawaambieni, malaika wao huko mbinguni wako daima mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
11(有些抄本有第11节:“人子来,是要拯救失丧的人。”)
11Maana Mwana wa Mtu alikuja kuwaokoa wale waliopotea.
12你们认为怎样?有一个人,他有一百只羊,如果失了一只,他会不把九十九只留在山上,去寻找那迷失的吗?
12Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, akimpoteza mmoja, hufanyaje? Huwaacha wale tisini na tisa mlimani, na huenda kumtafuta yule aliyepotea.
13我实在告诉你们,他若找到了,就为这一只羊欢喜,胜过为那九十九只没有迷失的。
13Akimpata, nawaambieni kweli, humfurahia huyo kuliko awafurahiavyo wale tisini na tisa ambao hawakupotea.
14照样,你们在天上的父是不愿意这些小弟兄中有一个失丧的。
14Hali kadhalika, Baba yenu wa mbinguni hapendi hata mmoja wa hawa wadogo apotee.
15怎样对待犯了罪的弟兄“如果你的弟兄犯了罪(“犯了罪”有些抄本作“得罪你”),你趁着和他单独在一起的时候,要去指出他的过失来。如果他肯听,你就得着你的弟兄。
15"Ndugu yako akikukosea, mwendee ukamwonye mkiwa ninyi peke yenu. Akikusikia utakuwa umempata ndugu yako.
16如果他不肯听,就另外带一两个人同去,好使一切话,凭两三个证人的口,可以确定。
16Asipokusikia, chukua mtu mmoja au wawili pamoja nawe, ili kwa mawaidha ya mashahidi wawili au watatu, kila tatizo litatuliwe.
17如果他再不听,就告诉教会;如果连教会他也不听,就把他看作教外人和税吏吧。
17Asipowasikia hao, liambie kanisa. Na kama hatalisikia kanisa, na awe kwako kama watu wasiomjua Mungu na watoza ushuru.
18“我实在告诉你们,你们在地上捆绑的,在天上也被捆绑;你们在地上释放的,在天上也被释放。
18"Nawaambieni kweli, mtakachofunga duniani kitafungwa mbinguni, na mtakachofungua duniani kitafunguliwa mbinguni.
19我又告诉你们,你们当中若有两个人,在地上同心为什么事祈求,我在天上的父必为他们成全。
19Tena nawaambieni, wawili miongoni mwenu wakikubaliana hapa duniani kuhusu jambo lolote la kuomba, Baba yangu wa mbinguni atawafanyia jambo hilo.
20因为无论在哪里,有两三个人奉我的名聚会,我就在他们中间。”
20Kwa maana popote pale wanapokusanyika wawili au watatu kwa jina langu, mimi nipo hapo kati yao."
21不饶恕人的也得不着饶恕那时,彼得前来问耶稣:“主啊,如果我的弟兄得罪我,我要饶恕他多少次?七次吗?”
21Kisha Petro akamwendea Yesu, akamwuliza, "Je, ndugu yangu akinikosea, nimsamehe mara ngapi? Mara saba?"
22耶稣对他说:“我告诉你,不是七次,而是七十个七次。
22Yesu akamjibu, "Sisemi mara saba tu, bali sabini mara saba.
23因此,天国好像一个王,要和他的仆人算帐,
23Ndiyo maana Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyeamua kukagua hesabu za watumishi wake.
24刚算的时候,有人带了一个欠下六千万银币的人来。
24Ukaguzi ulipoanza, akaletewa mtu mmoja aliyekuwa na deni la fedha talanta elfu kumi.
25他没有钱偿还,主人就下令叫人把他和他的妻子儿女,以及一切所有的都卖掉,用来偿还。
25Mtu huyo hakuwa na chochote cha kulipa; hivyo bwana wake aliamuru wauzwe, yeye, mke wake, watoto wake na vitu vyote alivyokuwa navyo, ili deni lilipwe.
26那仆人就跪下拜他,说:‘请宽容我,我会把一切还给你的。’
26Basi, huyo mtumishi akapiga magoti mbele yake, akasema, Unisubiri nami nitakulipa deni lote.
27主人动了慈心,把那仆人放了,并且免了他的债。
27Yule bwana alimwonea huruma, akamsamehe lile deni, akamwacha aende zake.
28那仆人出来,遇见一个欠了他一百个银币的仆人,就抓住他,扼着他的喉咙,说:‘把你欠我的钱还给我。’
28"Lakini huyo mtumishi akaondoka, akamkuta mmoja wa watumishi wenzake aliyekuwa na deni lake fedha denari mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akisema, Lipa deni lako!
29那和他一同作仆人的就跪下求他,说:‘请宽容我,我会还给你的。’
29Huyo mtumishi mwenzake akapiga magoti, akamwomba, Unisubiri nami nitalipa deni langu lote.
30他却不肯,反而把他带走,关在监里,等他把所欠的还清。
30Lakini yeye hakutaka, bali alimtia gerezani mpaka hapo atakapolipa lile deni.
31其他的仆人看见这事,非常难过,就去向主人报告这一切事情。
31"Basi, watumishi wenzake walipoona jambo hilo walisikitika sana, wakaenda kumpasha habari bwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia.
32于是主人叫他来,对他说:‘你这个恶仆,你求我,我就免了你欠我的一切。
32Hapo yule bwana alimwita huyo mtumishi, akamwambia, Wewe ni mtumishi mbaya sana! Uliniomba, nami nikakusamehe deni lako lote.
33难道你不应该怜悯你的同伴,好像我怜悯你一样吗?’
33Je, haikukupasa nawe kumhurumia mtumishi mwenzako kama nilivyokuhurumia?
34于是主人大怒,把他送去服刑,等他把所欠的一切还清。
34"Basi, huyo bwana alikasirika sana, akamtoa huyo mtumishi aadhibiwe mpaka hapo atakapolipa deni lote.
35如果你们各人不从心里饶恕你的弟兄,我的天父也必这样待你们。”
35Na baba yangu aliye mbinguni atawafanyieni vivyo hivyo kama kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kwa moyo wake wote."