1 神配合的,人不可分开(可10:1-12)
1Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, alitoka Galilaya, akaenda katika mkoa wa Yudea, ng'ambo ya mto Yordani.
2有许多人跟着他;他在那里医好了他们。
2Watu wengi walimfuata huko, naye akawaponya.
3法利赛人前来试探耶稣,说:“人根据某些理由休妻,可以吗?”
3Mafarisayo kadhaa walimjia, wakamwuliza kwa kumtega, "Je, ni halali mume kumpa talaka mkewe kwa kisa chochote?"
4他回答:“造物者从起初‘造人的时候,就造男造女’。’因此人要离开父母,与妻子连合,二人成为一体。’这些话你们没有念过吗?
4Yesu akawajibu, "Je, hamkusoma katika Maandiko Matakatifu kwamba Mungu aliyemuumba mtu tangu mwanzo alimfanya mwanamume na mwanamke,
5
5na akasema: Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja?
6这样,他们不再是两个人,而是一体的了。所以 神所配合的,人不可分开。”
6Kwa hiyo wao si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asikitenganishe."
7他们就问:“为什么摩西却吩咐‘人若给了休书,就可以休妻’呢?”
7Lakini wao wakamwuliza, "Kwa nini basi, Mose alituagiza mwanamke apewe hati ya talaka na kuachwa?"
8他说:“摩西因为你们的心硬,才准许你们休妻,但起初并不是这样。
8Yesu akawajibu, "Mose aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu.
9我告诉你们,凡休妻另娶的,如果不是因为妻子不贞,就是犯奸淫了。”
9Lakini haikuwa hivyo tangu mwanzo. Basi nawaambieni, yeyote atakayemwacha mke wake isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, akaoa mke mwingine, anazini."
10门徒对他说:“夫妻的关系既然是这样,倒不如不结婚了。”
10Wanafunzi wake wakamwambia, "Ikiwa mambo ya mume na mkewe ni hivyo, ni afadhali kutooa kabisa."
11耶稣对他们说:“这话不是每个人都能领受的,只有赐给谁,谁才能领受。
11Yesu akawaambia, "Si wote wanaoweza kulipokea fundisho hili, isipokuwa tu wale waliojaliwa na Mungu.
12有些人是生来就不能结婚的,有些人不能结婚是因为人使他们这样,也有些人是为了天国的缘故自愿这样的。谁能领受就领受吧!”
12Maana kuna sababu kadhaa za kutoweza kuoa: wengine ni kwa sababu wamezaliwa hivyo, wengine kwa sababu wamefanywa hivyo na watu, na wengine wameamua kutooa kwa ajili ya Ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee."
13给小孩子按手祈祷(可10:13-16;路18:15-17)那时,有人带了小孩子到耶稣面前,求他给他们按手祈祷,门徒就责备那些人。
13Kisha watu wakamletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono na kuwaombea. Lakini wanafunzi wakawakemea.
14但耶稣说:“让小孩子到我这里来,不要禁止他们,因为天国是属于这样的人的。”
14Yesu akasema, "Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie; maana Ufalme wa mbinguni ni wa watu walio kama watoto hawa."
15于是他给他们按手,然后离开那里。
15Basi, akawawekea mikono, kisha akaondoka mahali hapo.
16有钱的人难进 神的国(可10:17-31;路18:18-30)有一个人前来见耶稣,说:“老师,我要作什么善事,才可以得着永生?”
16Mtu mmoja alimjia Yesu, akamwuliza, "Mwalimu, nifanye kitu gani chema ili niupate uzima wa milele?"
17耶稣说:“为什么问我关于善的事呢?只有一位是善的。如果你想进入永生,就应当遵守诫命。”
17Yesu akamwambia, "Mbona unaniuliza kuhusu jambo jema? Kuna mmoja tu aliye mwema. Ukitaka kuingia katika uzima, shika amri."
18他问:“什么诫命?”耶稣回答:“就是‘不可杀人,不可奸淫,不可偷盗,不可作假证供;
18Yule mtu akamwuliza, "Amri zipi?" Yesu akasema, "Usiue, usizini, usiibe, usitoe ushahidi wa uongo,
19当孝敬父母,当爱人如己’。”
19waheshimu baba yako na mama yako; na, mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe."
20那青年对他说:“这一切我都遵守了,还缺少什么呢?”
20Huyo kijana akamwambia, "Hayo yote nimeyazingatia tangu utoto wangu; sasa nifanye nini zaidi?"
21耶稣对他说:“如果你想要完全,就去变卖你所有的,分给穷人,你就必定有财宝在天上,而且你要来跟从我。”
21Yesu akamwambia, "Kama unapenda kuwa mkamilifu, nenda ukauze mali yako uwape maskini hiyo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoo unifuate."
22那青年听见这话,就忧忧愁愁地走了,原来他的财产很多。
22Huyo kijana aliposikia hayo, alienda zake akiwa mwenye huzuni, maana alikuwa na mali nyingi.
23耶稣对门徒说:“我实在告诉你们,有钱的人是很难进天国的。
23Hapo Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Kweli nawaambieni, itakuwa vigumu sana kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.
24我又告诉你们,骆驼穿过针眼,比有钱的人进 神的国还容易呢!”
24Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni."
25门徒听见了,十分惊奇,就问他:“这样,谁可以得救呢?”
25Wale wanafunzi waliposikia hivyo walishangaa, wakamwuliza, "Ni nani basi, awezaye kuokoka?"
26耶稣看着他们说:“在人这是不能的,在 神却凡事都能。”
26Yesu akawatazama, akasema, "Kwa binadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote huwezekana."
27那时彼得对他说:“你看,我们已经舍弃一切跟从了你,我们会得到什么呢?”
27Kisha Petro akasema, "Na sisi je? Tumeacha yote tukakufuata; tutapata nini basi?"
28耶稣对他们说:“我实在告诉你们,到了万物更新,人子坐在他荣耀的宝座上的时候,你们这些跟从我的人,也会坐在十二个宝座上,审判以色列的十二个支派。
28Yesu akawaambia, "Nawaambieni kweli, Mwana wa Mtu atakapoketi katika kiti cha enzi cha utukufu wake katika ulimwengu mpya, ninyi mlionifuata mtaketi katika viti kumi na viwili mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.
29凡为我的名撇下房屋、兄弟、姊妹、父母、儿女或田地的,他必得着百倍,并且承受永生。
29Na kila aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi, na kupata uzima wa milele.
30然而许多在前的将要在后,在后的将要在前。”
30Lakini walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.