聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Matthew

23

1经学家和法利赛人有祸了(可12:38-39;路20:45-46)
1Kisha Yesu akauambia umati wa watu pamoja na wanafunzi wake,
2“经学家和法利赛人坐在摩西的座位上,
2"Walimu wa Sheria na Mafarisayo wana mamlaka ya kufafanua Sheria ya Mose.
3所以凡他们吩咐你们的,你们都要遵守,但不可效法他们的行为,因为他们只会说而不去作。
3Kwa hiyo shikeni na kutekeleza chochote watakachowaambieni. Lakini msiyaige matendo yao, maana hawatekelezi yale wanayoyahubiri.
4他们把重担捆起来,压在人的肩头上,但自己连一个指头也不肯动。
4Hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani, lakini wao wenyewe hawataki kunyosha hata kidole wapate kuibeba.
5他们所作的一切,都是要作给人看:他们把经文的匣子做大了,衣服的繸子做长了;
5Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa tepe zenye maandishi ya Sheria juu ya panda la uso na mikononi na hupanua pindo za makoti yao.
6他们喜欢筵席上的首位、会堂里的高位;
6Hupenda nafasi za heshima katika karamu na viti vya heshima katika masunagogi.
7又喜欢人在市中心向他们问安,称呼他们‘拉比’。
7Hupenda kusalimiwa kwa heshima sokoni na kupendelea kuitwa na watu: Mwalimu.
8然而你们不要被人称为‘拉比’,因为只有一位是你们的老师,你们都是弟兄。
8Lakini ninyi msiitwe kamwe Mwalimu, maana mwalimu wenu ni mmoja tu, nanyi nyote ni ndugu.
9不要称呼地上的人为父,因为只有一位是你们的父,就是天父。
9Wala msimwite mtu yeyote Baba hapa duniani, maana Baba yenu ni mmoja tu aliye mbinguni.
10你们也不要被人称为师傅,因为只有一位是你们的师傅,就是基督。
10Wala msiitwe Viongozi, maana kiongozi wenu ni mmoja tu, ndiye Kristo.
11你们中间最大的,必作你们的仆人。
11Aliye mkubwa miongoni mwenu ni lazima awe mtumishi wenu.
12凡高抬自己的,必被降卑;凡自己谦卑的,必被升高。
12Anayejikweza atashushwa, na anayejishusha atakwezwa.
13“虚伪的经学家和法利赛人哪,你们有祸了!你们在人面前关了天国的门,自己不进去,连正要进去的人,你们也不准他们进去。
13"Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnaufunga mlango wa Ufalme wa mbinguni mbele ya macho ya watu. Ninyi wenyewe hamwingii ndani, wala hamwaruhusu wanaotaka kuingia waingie.
14(有些抄本有第14节:“虚伪的经学家和法利赛人哪,你们有祸了!你们吞没了寡妇的房产,假装作冗长的祷告,所以你们必受更重的刑罚。”)
14Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnawanyonya wajane na kujisingizia kuwa watu wema kwa kusali sala ndefu. Kwa sababu hiyo mtapata adhabu kali.
15“虚伪的经学家和法利赛人哪,你们有祸了!你们走遍海洋陆地,要使一个人入教;当他入了教,你们却使他沦为地狱之子,比你们更甚。
15"Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate dini yenu. Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika moto wa Jehanamu kuliko ninyi wenyewe.
16“你们这些瞎眼的向导有祸了!你们说:‘凡指着圣所而起的誓,是没有用的;但指着圣所的金子而起的誓,就必须遵守。’
16"Ole wenu viongozi vipofu! Ninyi mwasema ati mtu akiapa kwa Hekalu, kiapo hicho si kitu; lakini akiapa kwa dhahabu ya Hekalu, kiapo hicho kinamshika.
17你们这些瞎眼的愚昧人哪,到底是金子大,还是使金子成圣的圣所大呢?
17Enyi vipofu wapumbavu! Kipi kilicho cha maana zaidi: dhahabu au Hekalu linalofanya hiyo dhahabu kuwa takatifu?
18你们又说:‘凡指着祭坛所起的誓,是没有用的;但指着坛上的祭物所起的誓,就必须遵守。’
18Tena mwasema ati mtu akiapa kwa madhabahu si kitu; lakini akiapa kwa zawadi iliyowekwa juu ya madhabahu, kiapo hicho humshika.
19瞎眼的人哪!到底是祭物大,还是使祭物成圣的祭坛大呢?
19Enyi vipofu! Ni kipi kilicho cha maana zaidi: ile zawadi, au madhabahu ambayo hufanya hiyo zawadi kuwa takatifu?
20所以,凡指着祭坛起誓的,他就是指着祭坛和坛上的一切起誓;
20Anayeapa kwa madhabahu ameapa kwa hiyo madhabahu, na kwa chochote kilichowekwa juu yake.
21指着圣所起誓的,就是指着圣所和住在那里的 神起誓;
21Na anayeapa kwa Hekalu ameapa kwa hilo Hekalu na pia kwa yule akaaye ndani yake.
22指着天起誓的,就是指着 神的宝座和坐在宝座上的起誓。
22Na anayeapa kwa mbingu ameapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa huyo aketiye juu yake.
23“虚伪的经学家和法利赛人哪,你们有祸了!你们把薄荷、茴香、芹菜,献上十分之一,却忽略律法上更重要的,就如正义、怜悯和信实;这些更重要的是你们应当作的,但其他的也不可忽略。
23Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnatoza watu zaka, hata juu ya majani yenye harufu nzuri, bizari na jira, na huku mnaacha mambo muhimu ya Sheria kama vile haki, huruma na imani. Haya ndiyo hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine.
24你们这些瞎眼的向导啊,你们把蚊虫滤出来,却把骆驼吞下去。
24Viongozi vipofu! Mnatoa nzi katika kinywaji, lakini mnameza ngamia!
25“虚伪的经学家和法利赛人哪,你们有祸了!你们洗净杯盘的外面,里面却装满了抢夺和放荡。
25"Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafisha kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata kwa unyang'anyi na uchoyo.
26瞎眼的法利赛人哪,先把杯和盘的里面洗净,好使外面也可以干净。
26Mfarisayo kipofu! Kisafishe kikombe ndani kwanza na nje kutakuwa safi pia.
27“虚伪的经学家和法利赛人哪,你们有祸了!你们好像粉饰了的坟墓,外面好看,里面却装满了死人的骨头和各样的污秽;
27"Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mko kama makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri, lakini ndani yamejaa mifupa ya maiti na kila namna ya uchafu.
28照样,你们外面看来像义人,里面却充塞着虚伪和不法。
28Hali kadhalika ninyi mnaonekana na watu kwa nje kuwa wema, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.
29“虚伪的经学家和法利赛人哪,你们有祸了!你们建造先知的墓,修饰义人的碑,
29"Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya watu wema.
30并且说:‘我们若活在我们祖先的时代,决不会与他们一同流先知的血。’
30Mwasema: Kama sisi tungaliishi nyakati za wazee wetu hatungalishirikiana nao katika mauaji ya manabii!
31这样,你们就指证自己是杀害先知的人的子孙了。
31Hivyo mnathibitisha ninyi wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa watu waliowaua manabii.
32那么,去完成你们祖先的罪孽吧!
32Haya, kamilisheni ile kazi wazee wenu waliyoianza!
33你们这些蛇,这些毒蛇所生的啊,你们怎能逃脱地狱的刑罚呢?
33Enyi kizazi cha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepa hukumu ya moto wa Jehanamu?
34因此,我差派先知、智慧人和经学家到你们那里;有些你们要杀害又钉在十字架上,有些你们要在会堂里鞭打,从一个城赶逐到另一个城。
34Ndiyo maana mimi ninawapelekea ninyi manabii, watu wenye hekima na walimu; mtawaua na kuwasulubisha baadhi yao, na wengine mtawapiga viboko katika masunagogi yenu na kuwasaka katika kila mji.
35所以,从义人亚伯的血起,到巴拉加的儿子撒迦利亚的血为止,他就是你们在圣所和祭坛中间所杀的,所有义人在地上所流的血,都要归在你们身上。
35Hivyo lawama yote itawapateni kwa ajili ya damu yote ya watu wema iliyomwagwa juu ya ardhi. Naam, tangu kuuawa kwa Abeli ambaye hakuwa na hatia, mpaka kuuawa kwa Zakariya, mwana wa Barakia, ambaye mlimuua Hekaluni kati ya patakatifu na madhabahu.
36我实在告诉你们,这一切都必临到这个世代。
36Nawaambieni kweli, kizazi hiki kitapata adhabu kwa sababu ya mambo haya.
37为耶路撒冷叹息(参路13:34-35)“耶路撒冷,耶路撒冷啊,你杀害先知,又用石头把奉派到你们那里的人打死。我多次想招聚你的儿女,好像母鸡招聚小鸡到翅膀底下,只是你们不愿意。
37"Yerusalemu, Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimejaribu kuwakusanya watoto wako kwangu, kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.
38你看,你们的家必成为荒场,留给你们。
38Haya basi, nyumba yako itaachwa mahame.
39我告诉你们,从今以后,你们一定见不到我,直等到你们说:‘奉主名来的,是应当称颂的。’”
39Nakwambia kweli, hutaniona tena mpaka wakati utakaposema: Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana."