1预言圣殿被毁(可13:1-2;路21:5-6)
1Yesu alitoka Hekaluni, na alipokuwa akienda zake, wanafunzi wake walimwendea, wakamwonyesha majengo ya Hekalu.
2他对门徒说:“你们不是看见了这一切吗?我实在告诉你们,将来在这里必没有一块石头留在另一块石头上面,每一块都要拆下来。”
2Yesu akawaambia, "Sawa, mnaweza kuyatazama haya yote! Kweli nawaambieni, hakuna hata jiwe moja litakalosalia hapa juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa."
3这世代终结的预兆(可13:3-13;路21:7-19)耶稣坐在橄榄山上,门徒暗中前来问他:“请告诉我们,什么时候会有这些事呢?你的降临和这世代的终结,有什么预兆呢?”
3Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni, wanafunzi walimwendea faraghani, wakamwuliza, "Twambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonyesha kuja kwako na mwisho wa nyakati?"
4耶稣回答他们:“你们要小心,不要被人迷惑;
4Yesu akawajibu, "Jihadharini msije mkadanganywa na mtu.
5因为许多人要假冒我的名而来,说:‘我就是基督’,并且要迷惑许多的人。
5Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu wakisema: Mimi ndiye Kristo, nao watawapotosha watu wengi.
6你们要听见战争,也听见战争的风声;你们要小心,不要惊慌,因为这是免不了的,不过结局还没有到。
6Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
7一个民族要起来攻打另一个民族,一个国家要起来攻打另一个国家,到处都有饥荒和地震,
7Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi.
8这一切不过是痛苦的开始。
8Yote hayo ni kama mwanzo wa maumivu ya kujifungua mtoto.
9那时人要把你们送去受苦,也要杀害你们,你们要因我的名被万民恨恶。
9"Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa ajili ya jina langu.
10那时许多人会失去信仰,彼此出卖,互相恨恶;
10Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana.
11也有许多假先知出现,要迷惑许多人。
11Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi.
12因为不法的事增加,许多人的爱心就冷淡了。
12Kwa sababu ya ongezeko la uhalifu, upendo wa watu wengi utafifia.
13唯有坚忍到底的,必然得救。
13Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokoka.
14这天国的福音要传遍天下,向万民作见证,然后结局才来到。
14Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya Ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote.
15大灾难的日子(可13:14-23;路21:20-24)“当你们看见但以理先知所说的‘那造成荒凉的可憎者’,站在圣地的时候(读者必须领悟),
15"Basi, mtakapoona Chukizo Haribifu lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake),
16那时,住在犹太的应当逃到山上;
16hapo, walioko Yudea na wakimbilie milimani.
17在房顶的不要下来拿家里的东西;
17Aliye juu ya paa la nyumba yake asishuke kuchukua kitu nyumbani mwake.
18在田里的也不要回去取衣服。
18Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake.
19当那些日子,怀孕的和乳养孩子的有祸了!
19Ole wao kina mama waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo!
20你们应当祈求,叫你们逃难的时候,不是在冬天或安息日,
20Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe siku za baridi au siku ya Sabato!
21因为那时必有大灾难,这是从世界的开始到现在未曾有过的,以后也必不会再有。
21Maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka leo, wala haitapata kutokea tena.
22如果那些日子不减少,没有一个人可以存活;但是为了选民,那些日子必会减少。
22Kama siku hizo hazingalipunguzwa, hakuna binadamu yeyote ambaye angeokoka; lakini siku hizo zitapunguzwa kwa ajili ya wale walioteuliwa.
23那时,如果有人对你们说:‘看哪,基督在这里!’或说:‘他在那里!’你们不要信,
23"Basi, mtu akiwaambieni siku hizo: Kristo yuko hapa au Yuko pale, msimsadiki.
24因为必有假基督和假先知出现,显大神迹和奇事;如果可以的话,他们连选民也要迷惑。
24Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Watafanya ishara kubwa na maajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekana hata wateule wa Mungu.
25你们看!我已经事先告诉你们了。
25Sikilizeni, nimekwisha kuwaonya kabla ya wakati.
26如果他们对你们说:‘看!基督在旷野里。’你们不要出去;或说:‘看!他在房子里。’也不要相信。
26Basi, wakiwaambieni, Tazameni, yuko jangwani, msiende huko; au, Tazameni, amejificha ndani, msisadiki;
27电光怎样从东方闪出来,一直照到西方,人子降临的时候,也是这样。
27maana, kama vile umeme uangazavyo toka mashariki hadi magharibi, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu.
28尸首在哪里,鹰也必聚在哪里。
28Pale ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.
29人子必驾云降临(可13:24-31;路21:25-33)“那些日子的灾难刚过去:太阳就变黑了,月亮也不发光,众星从天坠落,天上的万象震动。
29"Mara baada ya dhiki ya siku hizo, jua litatiwa giza, mwezi hautaangaza, nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa.
30“那时,人子的征兆要显在天上,地上的万族都要哀号,并且看见人子带着能力,满有荣耀,驾着天上的云降临。
30Kisha, ishara ya Mwana wa Mtu itaonekana angani, na hapo makabila yote duniani yatalalamika; watamwona Mwana wa Mtu akija juu ya mawingu ya angani mwenye nguvu na utukufu mwingi.
31当号筒发出响声,他要差派使者,把他的选民从四方,从天这边到天那边都招聚来。
31Naye atawatuma malaika wake wenye tarumbeta la kuvuma sana, nao watawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, toka mwisho huu wa mbingu hadi mwisho huu.
32“你们应该从无花果树学个功课:树枝长出嫩芽生出叶子的时候,你们就知道夏天近了;
32"Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
33同样,当你们看见这一切,就知道人子已经近在门口了。
33Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo haya yote yakitendeka, jueni kwamba yuko karibu sana.
34我实在告诉你们,这一切都必要发生,然后这世代才会过去。
34Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia.
35天地都要过去,但我的话决不会废去。
35Naam, mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
36警醒准备(可13:32-37;路17:26-30、34-36)“至于那日子和时间,没有人知道,连天上的使者和子也不知道,只有父知道。
36"Lakini, juu ya siku au saa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake ndiye ajuaye.
37挪亚的时代怎样,人子降临的时候也是这样。
37Kwa maana kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu.
38洪水之前的时代,人们吃喝嫁娶,直到挪亚进入方舟的那一天;
38Maana nyakati hizo, kabla ya gharika kuu, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka Noa alipoingia ndani ya ile safina.
39等到洪水来到,把他们冲去,他们才明白过来;人子降临的时候也是这样。
39Hawakujua kuna nini mpaka ile gharika ilipotokea, ikawakumba wote. Ndivyo itakavyokuwa wakati Mwana wa Mtu atakapokuja.
40那时,两个人在田里工作,一个被接去,一个撇下来;
40Wakati huo watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.
41两个女人在磨坊推磨,一个被接去,一个撇下来。
41Kina mama wawili watakuwa wanasaga nafaka, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.
42因此,你们要警醒,因为不知道你们的主什么时候要来。
42Basi, kesheni, kwa maana hamjui siku atakayokuja Bwana wenu.
43你们都知道,家主若晓得窃贼晚上什么时候会来,就会提高警觉,不让他摸进屋里。
43Lakini kumbukeni jambo hili: kama mwenye nyumba angejua siku mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe.
44所以,你们也要准备妥当,因为在想不到的时候,人子就来了。
44Kwa hiyo, nanyi pia muwe tayari, kwa maana Mwana wa Mtu atakuja saa msiyoitazamia."
45忠心的仆人有福了(路12:42-46)“谁是忠心和精明的仆人,被主人指派管理全家,按时分派粮食的呢?
45Yesu akaendelea kusema, "Ni nani basi mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watu wake, awape chakula kwa wakati wake?
46主人来到,看见他这样作,那仆人就有福了。
46Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakapokuja atamkuta akifanya hivyo.
47我实在告诉你们,主人要指派他管理自己的一切财产。
47Kweli nawaambieni, atamweka mtumishi huyo aisimamie mali yake yote.
48如果他是个坏的仆人,心里说‘我的主人不会那么快回来’,
48Lakini kama mtumishi mbaya akijisemea moyoni: Bwana wangu anakawia kurudi,
49就动手打其他的仆人,又和醉酒的人吃喝。
49kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, akaanza kula na kunywa pamoja na walevi,
50在他想不到的日子,不知道的时间,那仆人的主人要来,
50bwana wake atakuja siku asiyoitazamia na saa asiyoijua.
51严厉地处罚他,使他和虚伪的人同在一起;在那里必要哀哭切齿。”
51Atamkatilia mbali na kumweka kundi moja na wanafiki. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.