聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Revelation

11

1两个见证人
1Kisha nikapewa mwanzi uliokuwa kama kijiti cha kupimia, nikaambiwa, "Inuka, ukalipime Hekalu la Mungu, madhabahu ya kufukizia ubani, na ukawahesabu watu wanaoabudu ndani ya Hekalu.
2但圣所外面的院子,不要量它,因为它已经给了外族人,他们要践踏圣城四十二个月。
2Lakini uache ukumbi ulio nje ya Hekalu; usiupime, maana huo umekabidhiwa watu wa mataifa mengine, ambao wataukanyanga mji Mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na miwili.
3我要赐能力给我那两个穿着麻衣的见证人,他们要传道一千二百六十天。”
3Nami nitawatuma mashahidi wangu wawili ili watangaze ujumbe wa Mungu kwa muda huo wa siku elfu moja mia mbili na sitini wakiwa wamevaa mavazi ya magunia."
4他们就是站在全地之主面前的两棵橄榄树和两个灯台。
4Hao mashahidi wawili ni miti miwili ya Mizeituni na taa mbili zinazosimama mbele ya Bwana wa dunia.
5如果有人想要伤害他们,就有火从他们口中出来,吞灭他们的仇敌。凡是想要伤害他们的,都必这样被杀。
5Kama mtu akijaribu kuwadhuru, moto hutoka kinywani mwao na kuwaangamiza adui zao; na kila mtu atakayejaribu kuwadhuru atakufa namna hiyo.
6他们有权柄在他们传道的日子叫天闭塞不下雨,又有权柄掌管众水,使水变成血,并且有权柄可以随时随意用各样灾难击打全地。
6Hao wanayo mamlaka ya kufunga anga, mvua isinyeshe wakati wanapotangaza ujumbe wa Mungu. Tena wanayo mamlaka ya kuzigeuza chemchemi zote za maji ziwe damu, na ya kusababisha maafa ya kila namna duniani kila mara wapendavyo.
7他们作完了见证的时候,那从无底坑上来的兽要跟他们作战,胜过他们,把他们杀死。
7Lakini wakisha maliza kutangaza ujumbe huo, mnyama atokaye shimoni kuzimu atapigana nao, atawashinda na kuwaua.
8他们的尸首要倒在大城的街道上。这城按着寓意叫所多玛,又叫埃及,就是他们的主被钉十字架的地方。
8Maiti zao zitabaki katika barabara za mji mkuu ambapo Bwana wao alisulubiwa; jina la kupanga la mji huo ni Sodoma au Misri.
9从各民族、各支派、各方言和各邦国中,都有人观看他们的尸首三天半,又不许人把尸首安放在坟墓里。
9Watu wa kila kabila, lugha, taifa na rangi wataziangalia maiti hizo kwa muda wa siku tatu na nusu, na hawataruhusu zizikwe.
10住在地上的人为了他们的缘故,就欢喜快乐,彼此送礼,因为这两位先知曾经使他们受痛苦。
10Watu waishio duniani watafurahia kifo cha hao wawili. Watafanya sherehe na kupelekeana zawadi maana manabii hawa wawili walikuwa wamewasumbua mno watu wa dunia.
11过了三天半,有生命的气息从 神那里来,进入他们里面,他们就站立起来,看见他们的人都非常惧怕。
11Lakini baada ya zile siku tatu na nusu pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu iliwaingia, nao wakasimama; wote waliowaona wakaingiwa na hofu kuu.
12他们听见从天上来的大声音,说:“上这里来!”他们就驾着云上了天,他们的仇敌也看见了。
12Kisha hao manabii wawili wakasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikiwaambia, "Njoni hapa juu!" Nao wakapanda juu mbinguni katika wingu, maadui wao wakiwa wanawatazama.
13就在那时,大地震发生了,那座城倒塌了十分之一,因着地震而死的有七千人,其余的人都很害怕,就把荣耀归给天上的 神。
13Wakati huohuo, kukatokea tetemeko kubwa la ardhi, sehemu moja ya kumi ya ardhi ikaharibiwa. Watu elfu saba wakauawa kwa tetemeko hilo la ardhi. Watu waliosalia wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.
14第二样灾祸过去了。看哪,第三样灾祸快要到了!
14Maafa ya pili yamepita; lakini tazama! Maafa ya tatu yanafuata hima.
15吹第七枝号第七位天使吹号,天上就有大声音说:“世上的国成了我们的主和他所立的基督的国,他要作王,直到永永远远!”
15Kisha malaika wa saba akapiga tarumbeta yake. Na sauti kuu zikasikika mbinguni zikisema, "Sasa utawala juu ya ulimwengu ni wa Bwana wetu na Kristo wake. Naye atatawala milele na milele!"
16那在 神面前,坐在自己座位上的二十四位长老,都面伏在地上敬拜 神,
16Kisha wale wazee ishirini na wanne walioketi mbele ya Mungu katika viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu,
17说:“主啊!全能的 神,昔在今在的,我们感谢你!因为你执掌了大权,作王了!
17wakisema: "Bwana Mungu Mwenye uwezo, uliyeko na uliyekuwako! Tunakushukuru, maana umetumia nguvu yako kuu ukaanza kutawala!
18列国忿怒了!你的震怒也临到了!时候已经到了!死人要受审判!你的众仆人、先知、圣徒,和所有老幼贵贱、敬畏你名的人,都要得赏赐!你也要毁灭那些败坏全地的人!”
18Watu wa mataifa waliwaka hasira, maana wakati wa ghadhabu yako umefika, wakati wa kuwahukumu wafu. Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wako manabii, watu wako na wote wanaolitukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo. Ni wakati wa kuwaangamiza wale wanaoangamiza dunia."
19于是,在天上 神的圣所开了,他的约柜就在他的圣所中显现出来。随即有闪电、响声、雷轰、地震、大冰雹。
19Hekalu la Mungu mbinguni likafunguliwa, na Sanduku la Agano lake likaonekana Hekaluni mwake. Kisha kukatokea umeme, sauti, ngurumo, tetemeko la ardhi, na mvua kubwa ya mawe.