聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Revelation

12

1生子的女人和大龙
1Kisha ishara kubwa ikaonekana mbinguni. Palikuwa hapo mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!
2她怀了孕,在生产的痛苦中疼痛呼叫。
2Alikuwa mja mzito, na akapaaza sauti kwa maumivu na uchungu wa kujifungua mtoto.
3天上又出现了另一个景象。看哪!有一条大红龙,有七头十角,七头上戴着七个皇冠。
3Ishara nyingine ikatokea mbinguni: joka kubwa jekundu na lenye pembe kumi na vichwa saba; na kila kichwa kilikuwa na taji.
4它的尾巴拖着天上三分之一的星辰,把它们摔在地上。龙站在那快要生产的妇人面前,等她生产了,就要吞吃她的孩子。
4Joka hilo liliburuta kwa mkia wake theluthi moja ya nyota za anga na kuzitupa duniani. Nalo lilisimama mbele ya huyo mama aliyekuwa karibu kujifungua mtoto, tayari kabisa kummeza mtoto, mara tu atakapozaliwa.
5她生了一个男孩子,就是将来要用铁杖治理列国的。她的孩子被提取到 神和他宝座那里去。
5Kisha mama huyo akajifungua mtoto wa kiume, ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Lakini mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi.
6妇人就逃到旷野去了,那里有 神为她预备的地方。她在那里得供养一千二百六十天。
6Huyo mama akakimbilia jangwani, ambako Mungu alikuwa amemtayarishia mahali pa usalama ambapo angehifadhiwa kwa muda wa siku elfu moja mia mbili na sitini.
7天上发生了战争:米迦勒和他的天使与龙作战。龙和它的天使也起来应战,
7Kisha kukazuka vita mbinguni: Mikaeli na malaika wake walipigana na hilo joka, nalo likawashambulia pamoja na malaika wake.
8龙却抵挡不住,天上再也没有它们的地方了。
8Lakini joka hilo halikuweza kuwashinda, na hatimaye hapakuwa tena na nafasi mbinguni kwa ajili yake na malaika wake.
9于是那大龙被摔了下来。它就是那古蛇,名叫魔鬼,又叫撒但,是迷惑普天下的人的。它被摔在地上,它的天使也跟它一同被摔了下来。
9Basi, joka hilo kuu likatupwa nje. Joka hilo ndiye yule nyoka wa kale ambaye huitwa pia Ibilisi au Shetani. Ndiye anayeudanganya ulimwengu wote. Naam, alitupwa duniani, na malaika wake wote pamoja naye.
10我又听见天上有大声音说:“我们 神的救恩、能力、国度和他所立的基督的权柄,现在都已经来到了!因为那昼夜在我们 神面前控告我们弟兄的控告者,已经被摔下来了!
10Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema: "Sasa ukombozi utokao kwa Mungu umefika! Nguvu na Utawala wa Mungu wetu umedhihirika. Na Kristo wake ameonyesha mamlaka yake! Maana yule mdhalimu wa ndugu zetu, aliyesimama mbele ya Mungu akiwashtaki usiku na mchana, sasa ametupwa nje.
11弟兄胜过它,是因着羊羔的血,也因着自己所见证的道,他们虽然至死,也不爱惜自己的性命。
11Ndugu zetu wameshinda kwa damu ya Mwanakondoo na kwa nguvu ya ukweli walioutangaza; maana hawakuyathamini maisha yao kuwa kitu sana, wakawa tayari kufa.
12所以,众天和住在其中的,你们都欢乐吧!可是地和海有祸了!因为魔鬼知道自己的时日无多,就大大发怒下到你们那里去了。”
12Kwa sababu hiyo, furahini enyi mbingu na vyote vilivyomo ndani yenu. Lakini, ole wenu nchi na bahari, maana Ibilisi amewajieni akiwa na ghadhabu kuu, kwa sababu anajua kwamba siku zake zilizobakia ni chache."
13龙见自己被摔在地上,就迫害那生了男孩子的妇人。
13Joka lilipotambua kwamba limetupwa chini duniani, likaanza kumwinda yule mama aliyekuwa amejifungua mtoto wa kiume.
14于是有大鹰的两个翅膀赐给了那妇人,使她可以飞到旷野,到自己的地方,在那里得供养一年两年半年,离开那蛇的面。
14Lakini mama huyo akapewa mabawa mawili ya tai apate kuruka mbali sana na hilo joka, mpaka mahali, pake jangwani ambapo angehifadhiwa salama kwa muda wa miaka mitatu na nusu.
15蛇在妇人后面,从口中吐出水来,好像江河一样,要把妇人冲去。
15Basi, joka likatapika maji mengi kama mto, yakamfuata huyo mama nyuma ili yamchukue.
16地却帮助了那妇人,张开口,把从龙口中吐出来的河水吞了。
16Lakini nchi ikamsaidia huyo mama: ikajifunua kama mdomo na kuyameza maji hayo yaliyotoka kinywani mwa hilo joka.
17龙就向妇人发怒,去和她其余的子孙作战,就是和那遵守 神命令坚持耶稣见证的人作战。 [ (Revelation 12:18) 那时,龙站在海边的沙上。 ]
17Basi, joka hilo likamkasirikia huyo mama, likajiondokea, likaenda kupigana na wazawa wengine wa huyo mama, yaani wote wanaotii amri za Mungu na kuuzingatia ukweli wa Yesu.