聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Revelation

13

1海中的兽和地上的兽
1(G12-18) Na likajisimamia ukingoni mwa bahari. (G13-1) Kisha nikaona mnyama mmoja akitoka baharini. Alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na kila pembe ilikuwa na taji. Jina la kashfa lilikuwa limeandikwa juu ya vichwa hivyo.
2我所看见的兽,样子好像豹,脚像熊的脚,口像狮子的口。龙把自己的能力、王位和大权柄,都交给了它。
2Mnyama huyo niliyemwona alikuwa kama chui; miguu yake ilikuwa kama ya dubu, na kinywa chake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyama nguvu yake, kiti chake cha enzi na uwezo mkuu.
3兽的七头中有一个似乎受了致命伤,但那致命伤却医好了。全地的人都很惊奇,跟从那兽。
3Kichwa kimojawapo cha huyo mnyama kilionekana kama kilikwisha jeruhiwa vibaya sana, lakini jeraha hilo lilikuwa limepona. Dunia nzima ilishangazwa na huyo mnyama na kumfuata.
4因为龙把权柄交给了兽,大家就拜龙,也拜兽,说:“有谁可以跟这兽相比?有谁能与它作战呢?”
4Watu wote wakaliabudu lile joka kwa sababu lilimpa huyo mnyama uwezo wake. Wakamwabudu pia huyo mnyama wakisema, "Nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana naye?"
5龙又给了那兽一张说夸大和亵渎话的嘴巴,也给了它权柄可以任意而行四十二个月。
5Kisha huyo mnyama akaruhusiwa kusema maneno ya kujigamba na kumkufuru Mungu; akaruhusiwa kuwa na mamlaka kwa muda wa miezi arobaini na miwili.
6兽就开口向 神说亵渎的话,亵渎他的名和他的帐幕,以及那些住在天上的。
6Basi, akaanza kumtukana Mungu, kulitukana jina lake, makao yake, na wote wakaao mbinguni.
7它得了允许能跟圣徒作战,并且能胜过他们;又有权柄给了它,可以管辖各支派、各民族、各方言、各邦国。
7Aliruhusiwa kuwapiga vita na kuwashinda watu wa Mungu. Alipewa mamlaka juu ya watu wa kila kabila, ukoo, lugha na taifa.
8所有住在地上的人,名字没有记在创世以来被杀的羊羔之生命册上的,都要拜它。
8Wote waishio duniani watamwabudu isipokuwa tu wale ambao majina yao yameandikwa tangu mwanzo wa ulimwengu katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo aliyechinjwa.
9凡有耳的,就应当听!
9"Aliye na masikio, na asikie!
10如果人应该被俘掳,就必被俘掳;如果人应该被刀杀,就必被刀杀。在这里圣徒要有忍耐和信心!
10Waliokusudiwa kuchukuliwa mateka lazima watatekwa; waliokusudiwa kuuawa kwa upanga lazima watauawa kwa upanga. Kutokana na hayo ni lazima watu wa Mungu wawe na uvumilivu na imani."
11我又看见另一只兽从地里上来。它有两个角好像羊羔,说话好像龙。
11Kisha nikamwona mnyama mwingine anatoka ardhini. Alikuwa na pembe mbili kama pembe za kondoo, na aliongea kama joka.
12它在头一只兽面前,行使头一只兽的一切权柄。它使全地和住在地上的人,都拜那受过致命伤而医好了的头一只兽。
12Alikuwa na mamlaka kamili kutoka kwa yule mnyama wa kwanza, na akautumia uwezo huo mbele ya huyo mnyama. Akailazimisha dunia yote na wote waliomo humo kumwabudu huyo mnyama wa kwanza ambaye alikuwa na jeraha la kifo lililokuwa limepona.
13它又行大奇事,甚至在人面前叫火从天上降在地上。
13Basi, huyu mnyama wa pili akafanya miujiza mikubwa hata akasababisha moto kutoka mbinguni ushuke duniani mbele ya watu.
14它得了能力,在头一只兽面前能行奇事,迷惑了住在地上的人,吩咐住在地上的人,要为那受过刀伤而还活着的兽做个像。
14Aliwapotosha wakazi wa dunia kwa miujiza hiyo aliyojaliwa kutenda mbele ya mnyama wa kwanza. Aliwaambia wakazi wa dunia watengeneze sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi tena.
15又有能力赐给它,可以把气息给兽像,使兽像能够说话,并且能够杀害那些不拜兽像的人。
15Kisha alijaliwa kuipulizia uhai hiyo sanamu ya yule mnyama wa kwanza, hata ikaweza kuongea na kuwaua watu wote ambao hawakuiabudu.
16那从地里上来的兽,又要所有的人,无论大小贫富,自由的和作奴隶的,都在右手或额上,给自己作个记号。
16Aliwalazimisha wote, wadogo na wakubwa, matajiri na maskini, watu huru na watumwa, watiwe alama juu ya mikono yao ya kulia au juu ya paji za nyuso zao.
17这记号就是兽的名字或兽名的数字,除了那有记号的,谁也不能买,谁也不能卖。
17Akapiga marufuku mtu yeyote kununua au kuuza kitu isipokuwa tu mtu aliyetiwa alama hiyo, yaani jina la yule mnyama au tarakimu ya jina hilo.
18在这里要有智慧。有悟性的人,就让他计算兽的数字,因为这是人的数字,它的数字是六百六十六。
18Hapa ni lazima kutumia ujasiri! Mwenye akili anaweza kufafanua maana ya tarakimu ya mnyama huyo, maana ni tarakimu yenye maana ya mtu fulani. Tarakimu hiyo ni mia sita sitini na sita.