聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Revelation

14

1救赎的新歌
1Kisha nikaona mlima Sioni, na Mwanakondoo amesimama juu yake; pamoja naye walikuwa watu mia moja arobaini na nne elfu ambao juu ya paji za nyuso zao walikuwa wameandikwa jina la Mwanakondoo na jina la Baba yake.
2我听见有声音从天上来,好像众水的声音,好像大雷的声音;我所听见的声音,又像琴师弹奏的琴声。
2Basi, nikasikia sauti kutoka mbinguni, sauti iliyokuwa kama sauti ya maji mengi na kama sauti ya ngurumo kubwa. Sauti niliyosikia ilikuwa kama sauti ya wachezaji muziki wakipiga vinubi vyao.
3他们在宝座前,在四个活物和众长老面前唱新歌;除了从地上买来的那十四万四千人以外,没有人能学这歌。
3Walikuwa wanaimba wimbo mpya mbele ya kiti cha enzi na mbele ya wale viumbe hai wanne na wale wazee. Hakuna mtu aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao watu mia moja arobaini na nne elfu waliokombolewa duniani.
4这些人没有跟妇女在一起而使自己玷污,他们原是童身的。羊羔无论到哪里去,他们都跟随他。这些人是从世人中买来的,作初熟的果子归给 神和羊羔。
4Watu hao ndio wale waliojiweka safi kwa kutoonana kimwili na wanawake, nao ni mabikira. Wao humfuata Mwanakondoo kokote aendako. Wamekombolewa kutoka miongoni mwa binadamu wengine, wakawa wa kwanza kutolewa kwa Mungu na kwa Mwanakondoo.
5在他们口中找不着谎言;他们是没有瑕疵的。
5Hawakupata kamwe kuwa waongo; hawana hatia yoyote.
6三个天使的信息我又看见另一位天使在高空飞翔,有永远的福音要传给住在地上的人,就是各邦国、各支派、各方言、各民族的人。
6Kisha nikamwona malaika mwingine anaruka juu angani akiwa na Habari Njema ya milele ya Mungu, aitangaze kwa watu wote waishio duniani, kwa mataifa yote, makabila yote, watu wa lugha zote na rangi zote.
7他大声说:“应当敬畏 神,把荣耀归给他!因为他审判的时候到了,应当敬拜创造天、地、海和众水泉源的那一位!”
7Akasema kwa sauti kubwa, "Mcheni Mungu na kumtukuza! Maana saa imefika ya kutoa hukumu yake. Mwabuduni yeye aliyeumba mbingu na nchi, bahari na chemchemi za maji."
8又有第二位天使接着说:“倾倒了!大巴比伦倾倒了!它曾经叫列国喝它淫乱烈怒的酒。”
8Malaika wa pili alimfuata huyo wa kwanza akisema, "Ameanguka! Naam, Babuloni mkuu ameanguka! Babuloni ambaye aliwapa mataifa yote wainywe divai yake--divai kali ya uzinzi wake!"
9又有第三位天使接着他们大声说:“如果有人拜兽和兽像,又在自己的额上或手上受了记号,
9Na malaika wa tatu aliwafuata hao wawili akisema kwa sauti kubwa, "Yeyote anayemwabudu yule mnyama na sanamu yake na kukubali kutiwa alama yake juu ya paji la uso wake au juu ya mkono wake,
10他就必定喝 神烈怒的酒:这酒是斟在 神震怒的杯中,纯一不杂的。他必定在众天使和羊羔面前,在火与硫磺之中受痛苦。
10yeye mwenyewe atakunywa divai ya ghadhabu ya Mungu, ambayo imemiminwa katika kikombe cha ghadhabu yake bila kuchanganywa na maji. Mtu huyo atateseka ndani ya moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele ya Mwanakondoo.
11他们受痛苦的烟往上冒,直到永永远远。那些拜兽和兽像的,以及接受它名字的记号的人,日夜得不到安息。”
11Moshi wa moto unaowatesa kupanda juu milele na milele. Watu hao waliomwabudu huyo mnyama na sanamu yake, na kutiwa alama ya jina lake, hawatakuwa na nafuu yoyote usiku na mchana."
12在这里,那些遵守 神的命令和耶稣的信仰的圣徒,要有忍耐。
12Kutokana na hayo, ni lazima watu wa Mungu, yaani watu wanaotii amri ya Mungu na kumwamini Yesu, wawe na uvumilivu.
13我听见从天上有声音说:“你要写下来!从今以后,那在主里死去的人有福了!”圣灵说:“是的,他们脱离自己的劳苦,得享安息了,他们的作为也随着他们。”
13Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, "Andika! Heri watu ambao tangu sasa wanakufa wakiwa wameungana na Bwana." Naye Roho asema, "Naam! Watapumzika kutoka taabu zao; maana matunda ya jasho lao yatawafuata."
14收割地上的庄稼我又观看,见有一片白云,云上坐着一位好像人子的,头上戴着金冠,手里拿着锋利的镰刀。
14Kisha nikatazama, na kumbe palikuwapo wingu jeupe hapo. Na juu ya wingu hilo kulikuwa na kiumbe kama mtu. Alikuwa amevaa taji ya dhahabu kichwani, na kushika mundu mkononi mwake.
15有另一位天使从圣所出来,对那坐在云上的大声呼喊:“伸出你的镰刀来收割吧!因为收割的时候已经到了,地上的庄稼已经熟透了。”
15Kisha malaika mwingine akatoka Hekaluni, na kwa sauti kubwa akamwambia yule aliyekuwa amekaa juu ya wingu, "Tafadhali, tumia mundu wako ukavune mavuno, maana wakati wa mavuno umefika; mavuno ya dunia yameiva."
16于是那坐在云上的向地上挥动镰刀,地上的庄稼就被收割了。
16Basi, yule aliyekuwa amekaa juu ya wingu akautupa mundu wake duniani, na mavuno ya dunia yakavunwa.
17又有另一位天使从天上的圣所出来,他也拿着一把锋利的镰刀。
17Kisha malaika mwingine akatoka katika Hekalu mbinguni akiwa na mundu wenye makali.
18接着,又有一位天使从祭坛那里出来,是有权柄掌管火的;他向那拿着锋利镰刀的天使大声说:“伸出你锋利的镰刀来,收取地上葡萄树累累的果子吧!因为葡萄已经熟透了。”
18Kisha malaika mwingine msimamizi wa moto, akatoka madhabahuni akamwambia kwa sauti kubwa yule malaika mwenye mundu wenye makali, "Nawe tia huo mundu wako mkali, ukakate vichala vya mizabibu ya dunia, maana zabibu zake zimeiva!"
19于是,那天使向地上挥动镰刀,收取了地上的葡萄,把葡萄扔在 神烈怒的大压酒池里。
19Basi, malaika huyo akautupa mundu wake duniani, akakata zabibu za dunia, akazitia ndani ya chombo kikubwa cha kukamulia zabibu, chombo cha ghadhabu ya Mungu.
20那压酒池在城外被踹踏,就有血从压酒池流出来,涨到马的嚼环那么高,流到三百公里(“三百公里”原文作“一千六百司他町”)那么远。
20Zabibu zikakamuliwa ndani ya hilo shinikizo lililoko nje ya mji, na damu ikatoka katika shinikizo hilo mtiririko mrefu kiasi cha mita mia tatu na kina chake kiasi cha mita mia mbili.