聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Revelation

15

1最后的七灾
1Kisha nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na ya kushangaza. Palikuwa hapo malaika saba wenye mabaa makubwa saba ya mwisho. Kwa mabaa hayo makubwa saba, ghadhabu ya Mungu imekamilishwa.
2我又看见好像有一个搀杂着火的玻璃海;也看见那些胜过了兽、兽像,以及兽名的数字的人。他们都站在玻璃海上,拿着 神的琴。
2Kisha nikaona kitu kama bahari ya kioo, imechanganywa na moto. Nikawaona pia wale watu waliomshinda yule mnyama na sanamu yake na ambaye jina lake lilitajwa kwa ile tarakimu. Watu hao walikuwa wamesimama kando ya hiyo bahari ya kioo, wakiwa na vinubi walivyopewa na Mungu.
3他们唱着 神仆人摩西的歌和羊羔的歌,说:“主啊!全能的 神,你的作为又伟大又奇妙!万国的王啊,你的道路又公义又真实!
3Walikuwa wakiimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwanakondoo: "Bwana Mungu Mwenye Uwezo, matendo yako ni makuu mno! Ewe Mfalme wa mataifa, njia zako ni za haki na za kweli!
4主啊!谁敢不敬畏你,不荣耀你的名呢?因为只有你是神圣的,万国都要来,在你面前下拜,因为你公义的作为已经显明出来了。”
4Bwana, ni nani asiyekucha wewe? Nani asiyelitukuza jina lako? Wewe peke yako ni Mtakatifu. Mataifa yote yatakujia na kukuabudu maana matendo yako ya haki yameonekana na wote."
5这些事以后,我观看,见天上安放约柜(“约柜”原文作“见证的柜”)的帐幕的圣所开了。
5Baada ya hayo nikaona Hekalu limefunguliwa mbinguni, na ndani yake hema ionyeshayo kuwapo kwa Mungu.
6那掌管着末后七灾的七位天使,从圣所出来,穿着清洁明亮的细麻衣,胸间束着金带。
6Basi, wale malaika saba wenye mabaa saba wakatoka humo Hekaluni, wakiwa wamevaa nguo za kitani safi zenye kung'aa, na kanda za dhahabu vifuani mwao.
7四个活物中有一个,把盛满了活到永永远远之 神的烈怒的七个金碗,交给了那七位天使。
7Kisha, mmojawapo wa vile viumbe vinne akawapa hao malaika saba mabakuli ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu, aishiye milele na milele.
8因着 神的荣耀和大能,圣所中充满了烟,在那七位天使降完七灾以前,没有人能进入圣所。
8Hekalu likajaa moshi uliosababishwa na utukufu na nguvu ya Mungu, na hakuna mtu aliyeweza kuingia Hekaluni mpaka mwisho wa mabaa makubwa saba ya wale malaika saba.