聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Revelation

17

1骑着兽的大淫妇
1Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na bakuli akaja, akaniambia, "Njoo, mimi nitakuonyesha adhabu aliyopewa yule mzinzi mkuu, mji ule uliojengwa juu ya maji mengi.
2地上的众王都跟她行过淫,住在地上的人也都喝她淫乱的酒醉了。”
2Wafalme wa dunia wamefanya uzinzi pamoja naye; na wakazi wa dunia wamelewa divai ya uzinzi wake."
3我在灵里被天使带到旷野去,看见一个妇人,骑着朱红色的兽,这兽布满了亵渎的名号,有七头十角。
3Kisha, Roho akanikumba, akaniongoza mpaka jangwani. Huko nikamwona mwanamke ameketi juu ya mnyama mwekundu. Mnyama huyo alikuwa ameandikwa kila mahali majina ya makufuru; alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
4那妇人穿着紫色和朱红色的衣服,佩戴着金子、宝石和珍珠的装饰,手里拿着金杯,盛满了可憎的物,和她淫乱的污秽。
4Mwanamke huyo alikuwa amevaa vazi la rangi ya zambarau na nyekundu; alikuwa amejipamba kwa dhahabu, mawe ya thamani na lulu. Mkononi mwake alishika kikombe cha dhahabu ambacho kilikuwa kimejaa machukizo na mambo machafu yanayoonyesha uzinzi wake.
5她额上写着一个名号:“奥秘,大巴比伦,地上的淫妇和可憎的物之母。”
5Alikuwa ameandikwa juu ya paji la uso wake jina la fumbo "Babuloni mkuu, mama wa wazinzi na wa mambo yote ya kuchukiza sana duniani."
6我又看见那妇人喝圣徒的血,和那为耶稣作见证的人的血,喝醉了。我看见了她,就大大惊奇。
6Nikamwona huyo mwanamke amelewa damu ya watu wa Mungu, na damu ya watu waliouawa kwa sababu ya kumtangaza Yesu. Nilipomwona nilishangaa mno.
7天使对我说:“你为什么惊奇呢?我要把这妇人的奥秘,和驮着她的那七头十角的兽的奥秘告诉你。
7Lakini malaika akaniambia, "Kwa nini unashangaa? Mimi nitakuambia maana iliyofichika ya mwanamke huyu na mnyama huyo amchukuaye ambaye ana vichwa saba na pembe kumi.
8你看见的那兽,先前在、现今不在、将来要从无底坑上来,然后走向灭亡。住在世上的人,凡是名字在创世以来没有记在生命册上的,看见了那先前在、现今不在、将来还要出现的兽,就都要惊奇。
8Huyo mnyama uliyemwona alikuwa hai hapo awali, lakini sasa amekufa. Hata hivyo, karibu sana atapanda kutoka shimoni kuzimu, lakini ataangamizwa. Wanaoishi duniani watashangaa; naam, watu wote ambao majina yao hayakupata kuandikwa katika kitabu cha uzima tangu mwanzo wa ulimwengu, watashangaa kumwona huyo mnyama ambaye hapo awali, aliishi, kisha akafa na sasa anatokea tena!
9在这里需要有智慧的心。七头就是那妇人所坐的七座山,
9"Hapa panahitaji akili na hekima! Hivyo vichwa saba ni vilima saba, na huyo mwanamke anaketi juu yake. Vichwa hivyo pia ni wafalme saba.
10也就是七位王:五位已经倒了,一位还在,另一位还没有来到;他来的时候,必须存留一会儿。
10Kati ya hao wafalme saba, watano wamekwisha angamia, mmoja anatawala bado, na yule mwingine bado hajafika; na atakapofika atabaki kwa muda mfupi.
11那先前在、现今不在的兽,就是第八位。他也是出于那七位中的一位的,并且正在走向灭亡。
11Huyo mnyama ambaye alikuwa anaishi hapo awali lakini sasa haishi tena ni mfalme wa nane, naye pia ni miongoni mwa hao saba, na anakwenda zake kuharibiwa.
12你看见的那十角,就是十王,他们还没有取得王权;但要跟兽一同得着权柄,作王一个时期。
12"Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme ambao bado hawajaanza kutawala. Lakini watapewa mamlaka ya kutawala kwa muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.
13他们同心合意,把自己的权力权柄交给那兽。
13Shabaha ya hawa kumi ni moja, na watampa yule mnyama nguvu na mamlaka yao yote.
14他们要跟羊羔作战,羊羔必胜过他们,因为他是万主之主,万王之王。那些与羊羔同在、蒙召、被选、有忠心的,也必胜过他们。”
14Watapigana na Mwanakondoo, lakini Mwanakondoo pamoja na wale aliowaita na kuwachagua, ambao ni waaminifu, atawashinda kwa sababu yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme."
15天使又对我说:“你所看见那淫妇坐着的众水,就是多种民族、群众、邦国,方言的人。
15Malaika akaniambia pia, "Yale maji uliyoyaona pale alipokaa yule mzinzi, ni mataifa, watu wa kila rangi na lugha.
16你看见的十角和那兽,都要恨那淫妇,使她荒凉赤身,又要吃她的肉,用火把她烧掉。
16Pembe zile kumi ulizoziona na yule mnyama watamchukia huyo mzinzi. Watachukua kila kitu alicho nacho na kumwacha uchi; watakula nyama yake na kumteketeza kwa moto.
17 神要众王行他的旨意,就把意念放在他们心中,叫他们同心把自己的国献给那兽,直到 神的话都实现为止。
17Maana Mungu ametia mioyoni mwao nia ya kutekeleza shabaha yake, yaani kwa kukubaliana wao kwa wao na kumpa huyo mnyama mamlaka yao ya kutawala, mpaka hapo neno la Mungu litakapotimia.
18你看见的那妇人,就是有权统治地上的众王的那座大城。”
18"Na yule mwanamke uliyemwona ndio ule mji mkuu unaowatawala wafalme wa dunia."