聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Revelation

18

1大巴比伦倾倒
1Baada ya hayo, nilimwona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni. Alikuwa na uwezo mkuu, na dunia ikamulikwa na mng'ao wake.
2他用强有力的声音呼喊说:“倾倒了!大巴比伦倾倒了!成了鬼魔的住处,各样污灵的监狱,一切污秽可憎之雀鸟的牢笼,
2Basi, akapaaza sauti kwa nguvu akisema, "Umeanguka; Babuloni mkuu umeanguka! Sasa umekuwa makao ya mashetani na pepo wachafu; umekuwa makao ya ndege wachafu na wa kuchukiza mno.
3因为各国都喝她淫乱烈怒的酒醉了;地上的君王与她行淫,世上的商人因她奢华挥霍就发了财。”
3Maana mataifa yote yalileweshwa kwa divai kali ya uzinzi wake, nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi naye. Nao wafanyabiashara wa dunia wametajirika kutokana na anasa zake zisizo na kipimo."
4我听见另一个声音从天上来,说:“出来吧!我的子民,要从那城出来,免得在她的罪上有分,受她所受的灾难;
4Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, "Watu wangu, ondokeni kwake, ili msishirikiane naye katika dhambi zake, msije mkaipata adhabu yake.
5因为她的罪恶滔天, 神已经想起她的不义来。
5Kwa maana dhambi zake zimekuwa nyingi mno, zimelundikana mpaka mbinguni, na Mungu ameyakumbuka maovu yake.
6她怎样待人,你们也要怎样待她;照着她所作的,加倍报应她;用她调酒的杯,加倍调给她。
6Mtendeeni kama alivyowatendea ninyi; mlipeni mara mbili kwa yale aliyoyatenda. Jazeni kikombe chake kwa kinywaji kikali mara mbili zaidi ya kile alichowapeni.
7她怎样炫耀自己,怎样奢华挥霍,你们也要怎样给她痛苦悲哀。因为她心里常常说:‘我坐着作女王,我不是寡妇,决不会看见悲哀。’
7Mpeni mateso na uchungu kadiri ya kujigamba kwake, na kuishi kwake kwa anasa. Maana anajisemea moyoni: Ninaketi hapa; mimi ni malkia. Mimi si mjane, wala sitapatwa na uchungu!
8因此,在一日之内她的灾难必然来到,就是死亡、悲哀和饥荒;她还要在火中被烧掉,因为审判她的主 神是大有能力的。
8Kwa sababu hiyo mabaa yake yatampata kwa siku moja: ugonjwa, huzuni na njaa. Atachomwa moto, maana Bwana Mungu mwenye kumhukumu ni Mwenye Uwezo."
9“地上的众王,就是跟她一同行邪淫、骄奢无度的,看见焚烧她的烟的时候,就必为她痛哭捶胸。
9Wafalme wa Dunia waliofanya uzinzi naye na kuishi naye maisha ya anasa wataomboleza na kulia wakati watakapoona moshi wa mji huo unaoteketea.
10他们因为害怕她所受的痛苦,就远远地站着,说:‘有祸了!有祸了!这大城,巴比伦,这坚固的城啊!一时之间你的审判就来到了!’
10Wanasimama kwa mbali kwa sababu ya kuogopa mateso yake, na kusema, "Ole! Ole kwako Babuloni, mji maarufu na wenye nguvu! Kwa muda wa saa moja tu adhabu yako imekupata."
11“地上的商人也为她悲哀痛哭,因为没有人再买他们的货物:
11Wafanyabiashara wa dunia watalia na kumfanyia matanga, maana hakuna mtu anayenunua tena bidhaa zao;
12就是金、银、宝石、珍珠;细麻布、紫色布、丝绸、朱红色布;各样香木,各样象牙制品,各样极贵重的木器、铜器、铁器、大理石制品;
12hakuna tena wa kununua dhahabu yao, fedha, mawe ya thamani na lulu, kitani na nguo za rangi ya zambarau, hariri na nguo nyekundu; vyombo vya kila aina ya miti ya pekee, vyombo vya pembe za ndovu, vya miti ya thamani kubwa, vya shaba, chuma na marmari;
13肉桂、豆蔻、香料、香膏、乳香;酒、油、面粉、麦子;牛、羊、马、车、奴仆、人口。
13mdalasini, viungo, ubani, manemane, udi, divai, mafuta, unga na ngano, ng'ombe na kondoo, farasi na magari ya kukokotwa, watumwa wao na hata maisha ya watu.
14你所贪恋的果子离开你了!一切珍馐美味、华丽的美物,都从你那里消失,再也找不到了!
14Wafanyabiashara wanamwambia: "Faida yote uliyotazamia imetoweka, na utajiri na fahari vimekuponyoka; hutaweza kuvipata tena!"
15贩卖这些货物,借着她发了财的商人,因为害怕她受的痛苦,就远远地站着,痛哭悲哀,
15Wafanya biashara waliotajirika kutokana na mji huo, watasimama mbali kwa sababu ya hofu ya mateso yake, watalalamika na kuomboleza,
16说:‘有祸了!有祸了!这大城啊!就是一向穿着细麻布、紫色、朱红色的衣服,佩戴着金子、宝石和珍珠装饰的,
16wakisema, "Ole! Ole kwa mji huu mkuu. Ulizoea kuvalia nguo za kitani, za rangi ya zambarau na nyekundu, na kujipamba kwa dhahabu, mawe ya thamani na lulu!
17一时之间,这么大的财富竟荡然无存!’”所有船长、旅客、水手,以及凡是靠海谋生的,都远远地站着。
17Kwa saa moja tu utajiri wako umetoweka!" Halafu manahodha wote na wasafiri wao, wanamaji na wote wanaofanya kazi baharini, walisimama kwa mbali,
18他们看见了焚烧她的烟,就喊叫说:‘有哪一座城能与这大城相比呢?’
18na walipouona moshi wa moto ule uliouteketeza, wakalia kwa sauti: "Hakujapata kuwako mji kama mji huu mkuu!"
19他们又把尘土撒在自己头上,痛哭悲哀,喊着说:‘有祸了!有祸了!这大城啊!凡是有船航行海上的,都因这城的财宝发了财;一时之间她竟成了荒场!’
19Wakajimwagia vumbi juu ya vichwa vyao wakilia kwa sauti na kuomboleza: "Ole! Ole kwako mji mkuu! Ni mji ambamo wote wenye meli zisafirizo baharini walitajirika kutokana na utajiri wake. Kwa muda wa saa moja tu umepoteza kila kitu!"
20天哪,你要因她欢喜!众圣徒、众使徒、众先知啊,你们也要因她欢喜!因为 神已经在她身上为你们伸了冤。”
20Furahi ee mbingu, kwa sababu ya uharibifu wake. Furahini watu wa Mungu, mitume na manabii! Kwa maana Mungu ameuhukumu kwa sababu ya mambo uliyowatenda ninyi!
21有一位大力的天使,把一块好像大磨石一样的石头,举起来拋在海里,说:“巴比伦大城也必这样被猛力地拋下去,决不能再找到了!
21Kisha malaika mmoja mwenye nguvu sana akainua jiwe mfano wa jiwe kubwa la kusagia, akalitupa baharini akisema, "Ndivyo, Babuloni atakavyotupwa na kupotea kabisa.
22弹琴、奏乐、吹笛、吹号的声音,在你中间决不能再听到了!各样手艺技工,在你中间决不能再找到了!推磨的声音,在你中间决不能再听到了!
22Sauti za vinubi za muziki, sauti za wapiga filimbi na tarumbeta hazitasikika tena ndani yako. Hakuna fundi wa namna yoyote ile atakayepatikana tena ndani yako; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikika tena ndani yako.
23灯的亮光,在你中间决不能再照耀了!新郎新娘的声音,在你中间决不能再听到了!你的商人一向都是地上的大人物,万国都因你的邪术受了迷惑。
23Mwanga wa taa hautaonekana tena ndani yako; sauti za bwana arusi na bibi arusi hazitasikika tena ndani yako. Wafanyabiashara wako walikuwa wakuu duniani, na kwa uchawi wako mataifa yote yalipotoshwa!"
24先知、圣徒和地上一切被杀的人的血,都在这城里找到了!”
24Mji huo uliadhibiwa kwani humo mlipatikana damu ya manabii, damu ya watu wa Mungu na damu ya watu wote waliouawa duniani.