1给以弗所教会的信“你要写信给在以弗所教会的使者,说:‘那右手拿着七星,在七个金灯台中间行走的,这样说:
1"Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika hivi: "Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye ashikaye nyota saba katika mkono wake wa kulia, na ambaye hutembea katikati ya vinara saba vya taa vya dhahabu.
2我知道你的行为、你的劳苦、你的忍耐,也知道你不能容忍恶人。你也曾经试验那些自称是使徒,而其实不是使徒的人,看出他们是假的。
2Najua mambo yako yote; najua bidii yako na uvumilivu wako. Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume na kumbe sio, ukagundua kwamba ni waongo.
3你有忍耐,曾为我的名的缘故忍受一切,并不困倦。
3Wewe unayo saburi, umestahimili taabu nyingi kwa ajili ya jina langu, wala hukuvunjika moyo.
4然而有一件事我要责备你,就是你已经离弃了你起初的爱。
4Lakini ninayo hoja moja juu yako: wewe hunipendi tena sasa kama pale awali.
5所以,你应当回想你是从哪里坠落的,并且要悔改,作起初所作的事。你若不悔改,我就要来到你那里,把你的灯台从原处移去。
5Basi, pakumbuke pale ulipokuwa kabla ya kuanguka, ukayaache madhambi yako, na kufanya kama ulivyofanya pale awali. La sivyo, naja kwako na kukiondoa kinara chako mahali pake.
6不过你有这一个优点,就是你恨恶尼哥拉党的作为,那也是我所恨恶的。
6Lakini nakusifu juu ya kitu kimoja: wewe unayachukia wanayoyatenda Wanikolai kama ninavyoyachukia mimi.
7圣灵向众教会所说的话,有耳的就应当听。得胜的,我必定把 神乐园里生命树的果子赐给他吃。’
7"Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! "Wale wanaoshinda nitawapa haki ya kula matunda ya mti wa uzima ulioko ndani ya bustani ya Mungu.
8给士每拿教会的信“你要写信给在士每拿教会的使者,说:‘那首先的、末后的、曾经死去而又活过来的,这样说:
8"Kwa malaika wa kanisa la Smurna andika hivi: "Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye wa kwanza na wa mwisho, ambaye alikufa na akaishi tena.
9我知道你的患难和贫穷,但你却是富足的。我也知道那些自称是犹太人所说毁谤的话,其实他们不是犹太人,而是撒但的党徒。
9Najua taabu zako; najua pia umaskini wako, ingawaje kwa kweli wewe ni tajiri; najua kashfa walizokufanyia wale wanaojiita Wayahudi lakini si Wayahudi wa kweli, bali ni kundi lake Shetani.
10你不要怕你将要受的苦。看哪!魔鬼将要把你们中间几个人下在监里,叫你们受试炼,你们要受患难十天。你要忠心至死,我就把那生命的冠冕赐给你。
10Usiogope hata kidogo yale ambayo itakulazimu kuteseka. Sikiliza! Ibilisi anataka kuwajaribu kwa kuwatia baadhi yenu gerezani; nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Muwe waaminifu hata mpaka kufa, nami nitawapeni taji ya uzima.
11圣灵向众教会所说的话,有耳的就应当听。得胜的,决不会受第二次死的害。’
11"Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! "Wale wanaoshinda hawataumizwa na kifo cha pili.
12给别迦摩教会的信“你要写信给在别迦摩教会的使者,说:‘那有一把两刃利剑的,这样说:
12"Kwa malaika wa kanisa la Pergamoni andika hivi: "Huu ndio ujumbe wake yeye aliye na upanga mkali wenye kuwili.
13我知道你居住的地方,就是撒但王座所在的地方。当我忠心的见证人安提帕在你们那里,就是在撒但居住的地方被杀的那些日子,你还持守我的名,没有否认对我的信仰。
13Najua unakoishi: Wewe unaishi kwenye makao makuu ya Shetani! Lakini bado unashikilia jina langu; hukuikana imani yako kwangu hata siku zile Antipa shahidi wangu mwaminifu, alipouawa pale mahali anapoishi Shetani.
14然而有几件事我要责备你,因为在你那里有些人持守巴兰的教训。这巴兰曾经教导巴勒把绊脚石放在以色列人面前,叫他们吃祭过偶像的食物,并且行淫乱。
14Lakini ninayo machache dhidi yako: baadhi yenu ni wafuasi wa Balaamu aliyemfundisha Balaki kuwatega wana wa Israeli wale vyakula vilivyotambikiwa sanamu za kufanya uzinzi.
15同样,你也有些人持守尼哥拉党的教训。
15Vivyo hivyo, wako pia miongoni mwenu watu wanaofuata mafundisho ya Wanikolai.
16所以,你应当悔改;如果不悔改,我就很快地来到你们那里,用我口中的剑跟他们作战。
16Basi, achana na madhambi yako. La sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga utokao kinywani mwangu.
17圣灵向众教会所说的话,有耳的就应当听。得胜的,我必定把那隐藏的吗哪赐给他,并且赐他一块白石,石上写着新的名字,这名字除了那领受的人以外,是没有人能知道的。’
17"Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! "Wale wanaoshinda nitawapa ile mana iliyofichika. Nitawapa pia jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya ambalo hakuna mtu aliyelijua isipokuwa tu wale wanaolipokea.
18给推雅推拉教会的信“你要写信给在推雅推拉教会的使者,说:‘ 神的儿子,那眼睛像火焰、两脚像光铜的,这样说:
18"Kwa malaika wa kanisa la Thuatira andika hivi: "Huu ndio ujumbe wa Mwana wa Mungu, ambaye macho yake yametameta kama moto, na miguu yake inang'aa kama shaba iliyosuguliwa.
19我知道你的行为,你的爱心、信心、服侍和忍耐,也知道你后来所作的比先前的还要多。
19Najua mambo yako yote. Najua upendo wako, imani yako, utumishi wako na uvumilivu wako. Wewe unafanya vizuri zaidi sasa kuliko pale awali.
20然而有一件事我要责备你,就是你容让那自称是先知的妇人耶洗别,教导和引诱我的众仆人行淫乱,吃祭过偶像的食物。
20Lakini nina hoja moja juu yako: wewe unamvumilia yule mwanamke Yezabeli anayejiita nabii wa Mungu. Yeye huwafundisha na kuwapotosha watumishi wangu wafanye uzinzi na kula vyakula vilivyotambikiwa sanamu.
21我曾给她时间,让她悔改,她却不肯为她的淫行悔改。
21Nimempa muda wa kutubu dhambi zake, lakini hataki kuachana na uzinzi wake.
22看哪,我要把她拋在大患难的床上;那些跟她行淫乱的人,如果不为她的行为悔改,我也要把他们拋在大患难中。
22Sikiliza! Sasa namtupa kitandani ambapo yeye pamoja na wote waliofanya uzinzi naye watapatwa na mateso makali. Naam, nitafanya hivyo, kama wasipotubu matendo yao mabaya waliyotenda naye.
23我必以死亡击杀她的儿女;众教会就都知道我是察验人肺腑心肠的,我要照着你们的行为报应你们各人。
23Tena nitawaua wafuasi wake, ili makanisa yote yatambue kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na fikira za watu.
24至于你们其余在推雅推拉的人,就是不跟从那教训,不认识所谓撒但深奥的事的人,我告诉你们,我不会把别的重担放在你们身上。
24"Lakini ninyi wengine mlioko huko Thuatira ambao hamfuati mafundisho yake Yezabeli, na ambao hamkujifunza kile wanachokiita Siri ya Shetani, nawaambieni kwamba sitawapeni mzigo mwingine.
25不过,你们要持守已经得着的,直到我来。
25Lazima mzingatie yale mliyo nayo sasa mpaka nitakapokuja.
26得胜的,又遵守我的旨意到底的,我必把统治列国的权柄赐给他,
26"Wanaoshinda, na wale watakaozingatia mpaka mwisho kutenda ninayotaka, nitawapa mamlaka juu ya mataifa.
27他必用铁杖治理他们,好像打碎陶器一样粉碎他们,(“我必把......粉碎他们”引自诗2:8-9)
27Naam, nitawapa uwezo uleule nilioupokea kwa Baba: yaani, watayatawala mataifa kwa fimbo ya chuma na kuyavunjavunja kama chombo cha udongo.
28好像我从父领受了权柄一样;我还要把晨星赐给他。
28Tena nitawapa nyota ya asubuhi.
29圣灵向众教会所说的话,有耳的就应当听。’”
29"Aliye na masikio, basi, na ayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa!