聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Titus

3

1要常常留心作善工
1Wakumbushe watu kuwastahi watawala na wenye mamlaka, kuwatii na kuwa tayari kwa kila namna kutenda mambo yote mema.
2不可毁谤人,要与人无争,谦恭有礼,向众人表现充分温柔的心。
2Waambie wasimtukane mtu yeyote; bali waishi kwa amani na masikizano, wawe daima wapole kwa kila mtu.
3我们从前也是无知、不顺服、受了迷惑、被各种私欲和逸乐所奴役,生活在恶毒和嫉妒之中,是可憎可恶的,并且互相仇视。
3Maana, wakati mmoja sisi tulikuwa wapumbavu, wakaidi na wapotovu. Tulikuwa watumwa wa tamaa na anasa za kila aina. Tuliishi maisha ya uovu na wivu; watu walituchukia nasi tukawachukia.
4然而,到了 神我们的救主显明他的恩慈和怜爱的时候,
4Lakini wakati wema na upendo wa Mungu, Mwokozi wetu, ulipofunuliwa,
5他就救了我们,并不是由于我们所行的义,而是照着他的怜悯,借着重生的洗和圣灵的更新。
5alituokoa. alituokoa si kwa sababu ya jambo lolote jema tulilotenda sisi, bali alituokoa kwa sababu ya huruma yake, kwa njia ya Roho Mtakatifu anayetujalia tuzaliwe upya na kuwa na maisha mapya kwa kutuosha kwa maji.
6圣灵就是 神借着我们的救主耶稣基督丰丰富富浇灌在我们身上的,
6Mungu alitumiminia Roho Mtakatifu bila kipimo kwa njia ya Yesu Kristo, Mwokozi wetu,
7使我们既然因着他的恩典得称为义,就可以凭着永生的盼望成为后嗣。
7ili kwa neema yake tupate kukubaliwa kuwa waadilifu na kuupokea uzima wa milele tunaoutumainia.
8这话是可信的,我愿你确实地强调这些事,使信 神的人常常留心作善工;这些都是美事,并且是对人有益的。
8Jambo hili ni kweli. Ninakutaka uyatilie mkazo mambo haya, ili wale wanaomwamini Mungu, wawe na hamu ya kuutumia wakati wao katika kutenda mema, ambayo ni mambo mazuri na ya manufaa kwa watu.
9你要远避愚昧的辩论、家谱、纷争和律法上的争执,因为这都是虚妄无益的。
9Lakini jiepushe na ubishi wa kipumbavu, ugomvi na mabishano juu ya Sheria. Mambo hayo hayana faida yoyote na ni ya bure tu.
10分门结党的人,警戒一两次之后,就要和他绝交。
10Mtu anayesababisha mafarakano mpe onyo la kwanza na la pili, kisha achana naye.
11你知道这种人已经背道,常常犯罪,定了自己的罪。
11Wajua kwamba mtu wa namna hiyo amepotoka kabisa, na dhambi zake zathibitisha kwamba amekosea.
12嘱咐和问安我派亚提马或推基古到你那里去的时候,你要赶快到尼哥波立来见我,因为我已决定在那里过冬。
12Baada ya kumtuma kwako Artema au Tukiko, fanya bidii kuja Nikopoli unione, maana nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya baridi.
13你要尽力资助西纳律师和亚波罗的旅程,使他们不致缺乏。
13Jitahidi kumsaidia mwana sheria Zena na Apolo ili waweze kuanza ziara zao na uhakikishe kwamba wana kila kitu wanachohitaji.
14我们自己的人也应当学习作善工,供应日常的需要,免得不结果子。
14Ni lazima watu wetu wajifunze kuutumia wakati wao katika kutenda mema ili wasaidie katika mahitaji ya kweli, na maisha yao yawe ya kufaa.
15同我在一起的人都向你问安。请你问候那些因信而爱我们的人。愿恩惠与你们众人同在。
15Watu wote walio pamoja nami wanakusalimu. Wasalimu rafiki zetu katika imani. Nawatakieni nyote neema ya Mungu.