1In [the] beginning was the Word, and the Word was with God, and the Word was God.
1Hapo Mwanzo, Neno alikuwako; naye alikuwa na Mungu, naye alikuwa Mungu.
2*He* was in the beginning with God.
2Tangu mwanzo Neno alikuwa na Mungu.
3All things received being through him, and without him not one [thing] received being which has received being.
3Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa; hakuna hata kiumbe kimoja kilichoumbwa pasipo yeye.
4In him was life, and the life was the light of men.
4Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu.
5And the light appears in darkness, and the darkness apprehended it not.
5Na mwanga huo huangaza gizani, nalo giza halikuweza kuushinda.
6There was a man sent from God, his name John.
6Mungu alimtuma mtu mmoja jina lake Yohane,
7He came for witness, that he might witness concerning the light, that all might believe through him.
7ambaye alikuja kuwaambia watu juu ya huo mwanga. Alikuja ili kwa ujumbe wake watu wote wapate kuamini.
8*He* was not the light, but that he might witness concerning the light.
8Yeye hakuwa huo mwanga, ila alikuja tu kuwaambia watu juu ya huo mwanga.
9The true light was that which, coming into the world, lightens every man.
9Huu ndio mwanga halisi, mwanga unaokuja ulimwenguni, na kuwaangazia watu wote.
10He was in the world, and the world had [its] being through him, and the world knew him not.
10Basi, Neno alikuwako ulimwenguni; na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa, lakini ulimwengu haukumtambua.
11He came to his own, and his own received him not;
11Alikuja katika nchi yake mwenyewe, nao walio wake hawakumpokea.
12but as many as received him, to them gave he [the] right to be children of God, to those that believe on his name;
12Lakini wale wote waliompokea na kumwamini, hao aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu.
13who have been born, not of blood, nor of flesh's will, nor of man's will, but of God.
13Hawa wamekuwa watoto wa Mungu si kwa uwezo wa kibinadamu, wala kwa nguvu za kimwili, wala kwa mapenzi ya mtu, bali Mungu mwenyewe ndiye baba yao.
14And the Word became flesh, and dwelt among us (and we have contemplated his glory, a glory as of an only-begotten with a father), full of grace and truth;
14Naye Neno akawa mwanadamu, akakaa kwetu. Nasi tumeuona utukufu wake, utukufu wake yeye aliye Mwana wa pekee wa Baba; amejaa neema na ukweli.
15(John bears witness of him, and he has cried, saying, This was he of whom I said, He that comes after me is preferred before me, for he was before me;)
15Yohane aliwaambia watu habari zake, akasema kwa sauti, "Huyu ndiye niliyemtaja wakati niliposema: Anakuja mtu mmoja baada yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa."
16for of his fulness we all have received, and grace upon grace.
16Kutokana na ukamilifu wake sisi tumepokea neema mfululizo.
17For the law was given by Moses: grace and truth subsists through Jesus Christ.
17Maana Mungu alitoa Sheria kwa njia ya Mose, lakini neema na kweli vimekuja kwa njia ya Kristo.
18No one has seen God at any time; the only-begotten Son, who is in the bosom of the Father, *he* hath declared [him].
18Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote ule. Mwana wa pekee aliye sawa na Mungu ambaye ameungana na Baba, ndiye aliyetujulisha habari za Mungu.
19And this is the witness of John, when the Jews sent from Jerusalem priests and Levites that they might ask him, Thou, who art thou?
19Huu ndio ushahidi Yohane alioutoa wakati viongozi wa Wayahudi kule Yerusalemu walipowatuma makuhani wa Walawi kwake wamwulize: "Wewe u nani?"
20And he acknowledged and denied not, and acknowledged, I am not the Christ.
20Yohane hakukataa kujibu swali hilo, bali alisema waziwazi, "Mimi siye Kristo."
21And they asked him, What then? Art thou Elias? And he says, I am not. Art thou the prophet? And he answered, No.
21Hapo wakamwuliza, "Basi, wewe ni nani? Je, wewe ni Eliya?" Yohane akajibu, "La, mimi siye." Wakamwuliza, "Je, wewe ni yule nabii?" Yohane akawajibu, "La!"
22They said therefore to him, Who art thou? that we may give an answer to those who sent us. What sayest thou of thyself?
22Nao wakamwuliza, "Basi, wewe ni nani? Wasema nini juu yako mwenyewe? Tuambie, ili tuwapelekee jibu wale waliotutuma."
23He said, I [am] [the] voice of one crying in the wilderness, Make straight the path of [the] Lord, as said Esaias the prophet.
23Yohane akawajibu, "Mimi ndiye yule ambaye nabii Isaya alisema habari zake: Sauti ya mtu imesikika jangwani: Nyoosheni njia ya Bwana."
24And they were sent from among the Pharisees.
24Hao watu walikuwa wametumwa na Mafarisayo.
25And they asked him and said to him, Why baptisest thou then, if thou art not the Christ, nor Elias, nor the prophet?
25Basi, wakamwuliza Yohane, "Kama wewe si Kristo, wala Eliya, wala yule nabii, mbona wabatiza?"
26John answered them saying, I baptise with water. In the midst of you stands, whom ye do not know,
26Yohane akawajibu, "Mimi nabatiza kwa maji, lakini yuko mmoja kati yenu, msiyemjua bado.
27he who comes after me, the thong of whose sandal I am not worthy to unloose.
27Huyo anakuja baada yangu, lakini mimi sistahili hata kumfungua kamba za viatu vyake."
28These things took place in Bethany, across the Jordan, where John was baptising.
28Mambo haya yalifanyika huko Bethania, ng'ambo ya mto Yordani ambako Yohane alikuwa anabatiza.
29On the morrow he sees Jesus coming to him, and says, Behold the Lamb of God, who takes away the sin of the world.
29Kesho yake, Yohane alimwona Yesu akimjia, akasema, "Huyu ndiye Mwana-kondoo wa Mungu aondoaye dhambi ya ulimwengu!
30He it is of whom I said, A man comes after me who takes a place before me, because he *was* before me;
30Huyu ndiye niliyesema juu yake: Baada yangu anakuja mtu mmoja aliye mkuu zaidi kuliko mimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa!
31and I knew him not; but that he might be manifested to Israel, therefore have I come baptising with water.
31Mimi mwenyewe sikumfahamu, lakini nimekuja kubatiza kwa maji ili watu wa Israeli wapate kumjua."
32And John bore witness, saying, I beheld the Spirit descending as a dove from heaven, and it abode upon him.
32Huu ndio ushahidi Yohane alioutoa: "Nilimwona Roho akishuka kama njiwa kutoka mbinguni na kutua juu yake.
33And I knew him not; but he who sent me to baptise with water, *he* said to me, Upon whom thou shalt see the Spirit descending and abiding on him, he it is who baptises with [the] Holy Spirit.
33Mimi sikumjua, lakini yule aliyenituma nikabatize watu kwa maji alikuwa ameniambia: Mtu yule utakayemwona Roho akimshukia kutoka mbinguni na kukaa juu yake, huyo ndiye anayebatiza kwa Roho Mtakatifu.
34And I have seen and borne witness that this is the Son of God.
34Mimi nimeona na ninawaambieni kwamba huyu ndiye Mwana wa Mungu."
35Again, on the morrow, there stood John and two of his disciples.
35Kesho yake, Yohane alikuwa tena mahali hapo pamoja na wanafunzi wake wawili.
36And, looking at Jesus as he walked, he says, Behold the Lamb of God.
36Alipomwona Yesu akipita akasema, "Tazameni! Huyu ndiye Mwana-kondoo wa Mungu."
37And the two disciples heard him speaking, and followed Jesus.
37Hao wanafunzi walimsikia Yohane akisema maneno hayo, wakamfuata Yesu.
38But Jesus having turned, and seeing them following, says to them, What seek ye? And *they* said to him, Rabbi (which, being interpreted, signifies Teacher), where abidest thou?
38Basi, Yesu aligeuka, na alipowaona hao wanafunzi wanamfuata, akawauliza, "Mnatafuta nini?" Nao wakamjibu, "Rabi (yaani Mwalimu), unakaa wapi?"
39He says to them, Come and see. They went therefore, and saw where he abode; and they abode with him that day. It was about the tenth hour.
39Yesu akawaambia, "Njoni, nanyi mtaona." Hao wanafunzi wakamfuata, wakaona mahali alipokuwa anakaa, wakashinda naye siku hiyo. Ilikuwa yapata saa kumi jioni.
40Andrew, the brother of Simon Peter, was one of the two who heard [this] from John and followed him.
40Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa hao wawili waliokuwa wamemsikia Yohane akisema hivyo, wakamfuata Yesu.
41He first finds his own brother Simon, and says to him, We have found the Messias (which being interpreted is Christ).
41Andrea alimkuta kwanza Simoni, ndugu yake, akamwambia, "Tumemwona Masiha" (maana yake Kristo).
42And he led him to Jesus. Jesus looking at him said, Thou art Simon, the son of Jonas; thou shalt be called Cephas (which interpreted is stone).
42Kisha akampeleka Simoni kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama Simoni akasema, "Wewe ni Simoni mwana wa Yohane. Sasa utaitwa Kefa." (maana yake ni Petro, yaani, "Mwamba.")
43On the morrow he would go forth into Galilee, and Jesus finds Philip, and says to him, Follow me.
43Kesho yake Yesu aliamua kwenda Galilaya. Basi, akamkuta Filipo, akamwambia, "Nifuate."
44And Philip was from Bethsaida, of the city of Andrew and Peter.
44Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji wa akina Andrea na Petro.
45Philip finds Nathanael, and says to him, We have found him of whom Moses wrote in the law, and the prophets, Jesus, the son of Joseph, who is from Nazareth.
45Naye Filipo akamkuta Nathanieli, akamwambia, "Tumemwona yule ambaye Mose aliandika juu yake katika kitabu cha Sheria, na ambaye manabii waliandika habari zake, yaani Yesu Mwana wa Yosefu, kutoka Nazareti."
46And Nathanael said to him, Can anything good come out of Nazareth? Philip says to him, Come and see.
46Naye Nathanieli akamwuliza Filipo, "Je, kitu chema chaweza kutoka Nazareti?" Filipo akamwambia, "Njoo uone."
47Jesus saw Nathanael coming to him, and says of him, Behold [one] truly an Israelite, in whom there is no guile.
47Yesu alipomwona Nathanieli akimjia alisema juu yake, "Tazameni! Huyo ni Mwisraeli halisi: hamna hila ndani yake."
48Nathanael says to him, Whence knowest thou me? Jesus answered and said to him, Before that Philip called thee, when thou wast under the fig-tree, I saw thee.
48Naye Nathanieli akamwuliza, "Umepataje kunijua?" Yesu akamwambia, "Ulipokuwa chini ya mtini hata kabla Filipo hajakuita, nilikuona."
49Nathanael answered and said to him, Rabbi, thou art the Son of God, thou art the King of Israel.
49Hapo Nathanieli akamwambia, "Mwalimu, wewe ni Mwana wa Mungu. Wewe ni Mfalme wa Israeli!"
50Jesus answered and said to him, Because I said to thee, I saw thee under the fig-tree, believest thou? Thou shalt see greater things than these.
50Yesu akamwambia, "Je, umeamini kwa kuwa nimekwambia kwamba nilikuona chini ya mtini? Utaona makubwa zaidi kuliko haya."
51And he says to him, Verily, verily, I say to you, Henceforth ye shall see the heaven opened, and the angels of God ascending and descending on the Son of man.
51Yesu akaendelea kusema, "Nawaambieni kweli, mtaona mbingu zinafunguka na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Mtu."