1But on the morrow of the sabbath, very early indeed in the morning, they came to the tomb, bringing the aromatic spices which they had prepared.
1Jumapili, alfajiri na mapema, wale wanawake walikwenda kaburini wakichukua yale manukato waliyotayarisha.
2And they found the stone rolled away from the sepulchre.
2Walikuta lile jiwe limeviringishwa mbali na kaburi.
3And when they had entered they found not the body of the Lord Jesus.
3Walipoingia ndani, hawakuona mwili wa Bwana Yesu.
4And it came to pass as they were in perplexity about it, that behold, two men suddenly stood by them in shining raiment.
4Walipokuwa bado wanashangaa juu ya jambo hilo, mara watu wawili waliovaa mavazi yenye kung'aa sana, wakasimama karibu nao.
5And as they were filled with fear and bowed their faces to the ground, they said to them, Why seek ye the living one among the dead?
5Hao wanawake wakaingiwa na hofu, wakainama chini. Ndipo wale watu wakawaambia, "Kwa nini mnamtafuta aliye hai kati ya wafu?
6He is not here, but is risen: remember how he spoke to you, being yet in Galilee,
6Hayuko hapa; amefufuka. Kumbukeni aliyowaambieni alipokuwa kule Galilaya:
7saying, The Son of man must be delivered up into the hands of sinners, and be crucified, and rise the third day.
7Ni lazima Mwana wa Mtu atolewe kwa watu waovu, nao watamsulubisha, na siku ya tatu atafufuka."
8And they remembered his words;
8Hapo wanawake wakayakumbuka maneno yake,
9and, returning from the sepulchre, related all these things to the eleven and to all the rest.
9wakarudi kutoka kaburini, wakawapa mitume wale kumi na mmoja na wengine habari za mambo hayo yote.
10Now it was Mary of Magdala, and Johanna, and Mary the [mother] of James, and the others with them, who told these things to the apostles.
10Hao waliotoa habari hizo kwa mitume ni: Maria Magdalene, Yoana na Maria mama wa Yakobo, pamoja na wanawake wengine walioandamana nao.
11And their words appeared in their eyes as an idle tale, and they disbelieved them.
11Mitume waliyachukua maneno hayo kama yasiyo na msingi, hivyo hawakuamini.
12But Peter, rising up, ran to the sepulchre, and stooping down he sees the linen clothes lying there alone, and went away home, wondering at what had happened.
12Lakini Petro alitoka, akaenda mbio hadi kaburini. Alipoinama kuchungulia ndani, akaiona tu ile sanda. Akarudi nyumbani huku akiwa anashangaa juu ya hayo yaliyotokea.
13And behold, two of them were going on the same day to a village distant sixty stadia from Jerusalem, called Emmaus;
13Siku hiyohiyo, wawili kati ya wafuasi wake Yesu wakawa wanakwenda katika kijiji kimoja kiitwacho Emau, umbali wa kilomita kumi na moja kutoka Yerusalemu.
14and they conversed with one another about all these things which had taken place.
14Wakawa wanazungumza juu ya hayo yote yaliyotukia.
15And it came to pass as they conversed and reasoned, that Jesus himself drawing nigh, went with them;
15Walipokuwa wakizungumza na kujadiliana, Yesu mwenyewe akatokea, akatembea pamoja nao.
16but their eyes were holden so as not to know him.
16Walimwona kwa macho, lakini hawakumtambua.
17And he said to them, What discourses are these which pass between you as ye walk, and are downcast?
17Akawauliza, "Mnazungumza nini huku mnatembea?" Nao wakasimama kimya, nyuso zao wamezikunja kwa huzuni.
18And one [of them], named Cleopas, answering said to him, Thou sojournest alone in Jerusalem, and dost not know what has taken place in it in these days?
18Mmoja, aitwaye Kleopa, akamjibu, "Je, wewe ni mgeni peke yako Yerusalemu ambaye hujui yaliyotukia huko siku hizi?"
19And he said to them, What things? And they said to him, The things concerning Jesus the Nazaraean, who was a prophet mighty in deed and word before God and all the people;
19Naye akawajibu, "Mambo gani?" Wao wakamjibu, "Mambo yaliyompata Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo wa kutenda na kufundisha mbele ya Mungu na mbele ya watu wote.
20and how the chief priests and our rulers delivered him up to [the] judgment of death and crucified him.
20Makuhani na watawala wetu walimtoa ahukumiwe kufa, wakamsulubisha.
21But *we* had hoped that *he* was [the one] who is about to redeem Israel. But then, besides all these things, it is now, to-day, the third day since these things took place.
21Lakini sisi tulitumaini kwamba yeye ndiye angeikomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu mambo hayo yalipotendeka.
22And withal, certain women from amongst us astonished us, having been very early at the sepulchre,
22Tena, wanawake wengine wa kwetu wametushtua. Walikwenda kaburini mapema asubuhi,
23and, not having found his body, came, saying that they also had seen a vision of angels, who say that he is living.
23wasiukute mwili wake. Wakarudi wakasema kwamba walitokewa na malaika waliowaambia kwamba alikuwa hai.
24And some of those with us went to the sepulchre, and found it so, as the women also had said, but him they saw not.
24Wengine wetu walikwenda kaburini wakashuhudia yale waliyosema hao wanawake; ila yeye hawakumwona."
25And *he* said to them, O senseless and slow of heart to believe in all that the prophets have spoken!
25Kisha Yesu akawaambia, "Mbona mu wapumbavu kiasi hicho na mioyo yenu ni mizito hivyo kusadiki yote yaliyonenwa na manabii?
26Ought not the Christ to have suffered these things and to enter into his glory?
26Je, haikumpasa Kristo kuteswa, na hivyo aingie katika utukufu wake?"
27And having begun from Moses and from all the prophets, he interpreted to them in all the scriptures the things concerning himself.
27Akawafafanulia mambo yote yaliyomhusu yeye katika Maandiko Matakatifu kuanzia Mose hadi manabii wote.
28And they drew near to the village where they were going, and *he* made as though he would go farther.
28Walipokikaribia kile kijiji walikokuwa wanakwenda, Yesu akafanya kana kwamba anaendelea na safari;
29And they constrained him, saying, Stay with us, for it is toward evening and the day is declining. And he entered in to stay with them.
29lakini wao wakamsihi wakisema, "Kaa pamoja nasi, maana kunakuchwa, na usiku unakaribia." Basi, akaingia kijijini, akakaa pamoja nao.
30And it came to pass as he was at table with them, having taken the bread, he blessed, and having broken it, gave it to them.
30Alipoketi kula chakula pamoja nao, akachukua mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.
31And their eyes were opened, and they recognised him. And he disappeared from them.
31Mara macho yao yakafumbuliwa, wakamtambua; lakini yeye akatoweka kati yao.
32And they said to one another, Was not our heart burning in us as he spoke to us on the way, [and] as he opened the scriptures to us?
32Basi, wakaambiana, "Je, mioyo yetu haikuwa inawaka ndani yetu wakati alipokuwa anatufafanulia Maandiko Matakatifu kule njiani?"
33And rising up the same hour, they returned to Jerusalem. And they found the eleven, and those with them, gathered together,
33Wakaondoka saa ileile, wakarudi Yerusalemu: wakawakuta wale mitume kumi na mmoja na wale wengine waliokuwa pamoja nao, wamekusanyika
34saying, The Lord is indeed risen and has appeared to Simon.
34wakisema, "Hakika Bwana amefufuka, amemtokea Simoni."
35And they related what [had happened] on the way, and how he was made known to them in the breaking of bread.
35Basi, hao wafuasi wawili wakawajulisha yale yaliyowapata njiani, na jinsi walivyomtambua katika kumega mkate.
36And as they were saying these things, he himself stood in their midst, and says to them, Peace [be] unto you.
36Wanafunzi wote wawili walipokuwa wakiwaambia hayo, Yesu mwenyewe akasimama kati yao, akawaambia "Amani kwenu."
37But they, being confounded and being frightened, supposed they beheld a spirit.
37Wakashtuka na kushikwa na hofu wakidhani wameona mzimu.
38And he said to them, Why are ye troubled? and why are thoughts rising in your hearts?
38Lakini yeye akawaambia, "Kwa nini mnafadhaika? Mbona mnakuwa na mashaka mioyoni mwenu?
39behold my hands and my feet, that it is *I* myself. Handle me and see, for a spirit has not flesh and bones as ye see me having.
39Angalieni mikono na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe. Nipapaseni mkanione, maana mzimu hauna mwili na mifupa kama mnionavyo."
40And having said this he shewed them his hands and his feet.
40Baada ya kusema hayo, akawaonyesha mikono na miguu.
41But while they yet did not believe for joy, and were wondering, he said to them, Have ye anything here to eat?
41Wakiwa bado katika hali ya kutosadiki kwa sababu ya furaha yao, na wakiwa wanastaajabu, akawauliza, "Mnacho chakula chochote hapa?"
42And they gave him part of a broiled fish and of a honeycomb;
42Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa.
43and he took it and ate before them.
43Akakichukua, akala, wote wakimwona.
44And he said to them, These [are] the words which I spoke to you while I was yet with you, that all that is written concerning me in the law of Moses and prophets and psalms must be fulfilled.
44Halafu akawaambia, "Hii ndiyo maana ya maneno niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi: kwamba ilikuwa lazima kukamilisha yote yaliyoandikwa juu yangu katika Sheria ya Mose na katika vitabu vya manabii na katika kitabu cha Zaburi."
45Then he opened their understanding to understand the scriptures,
45Kisha, akaziangazia akili zao ili wapate kuelewa Maandiko Matakatifu.
46and said to them, Thus it is written, and thus it behoved the Christ to suffer, and to rise from among the dead the third day;
46Akawaambia, "Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka wafu,
47and that repentance and remission of sins should be preached in his name to all the nations beginning at Jerusalem.
47na kwamba ni lazima, kwa jina lake, mataifa yote kuanzia na Yerusalemu yahubiriwe juu ya kutubu na kusamehewa dhambi.
48And *ye* are witnesses of these things.
48Ninyi ni mashahidi wa mambo hayo.
49And behold, I send the promise of my Father upon you; but do ye remain in the city till ye be clothed with power from on high.
49Nami mwenyewe nitawapelekeeni yule ambaye Baba aliahidi kumtuma, lakini ngojeni huku mjini mpaka mtakapopewa ile nguvu itokayo juu."
50And he led them out as far as Bethany, and having lifted up his hands, he blessed them.
50Kisha akawaongoza nje ya mji hadi Bethania, akainua mikono yake juu, akawabariki.
51And it came to pass as he was blessing them, he was separated from them and was carried up into heaven.
51Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni.
52And *they*, having done him homage, returned to Jerusalem with great joy,
52Wao wakamwabudu, wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha kubwa:
53and were continually in the temple praising and blessing God.
53wakakaa muda wote Hekaluni wakimsifu Mungu.