Darby's Translation

Swahili: New Testament

Luke

23

1And the whole multitude of them, rising up, led him to Pilate.
1Kisha, wote kwa jumla, wakasimama, wakampeleka Yesu mbele ya Pilato.
2And they began to accuse him, saying, We have found this [man] perverting our nation, and forbidding to give tribute to Caesar, saying that he himself is Christ, a king.
2Wakaanza kumshtaki wakisema: "Tulimkuta mtu huyu akiwapotosha watu wetu, akipinga kulipa kodi kwa Kaisari na kujiita ati yeye ni Kristo, Mfalme."
3And Pilate demanded of him saying, Art *thou* the king of the Jews? And he answering him said, Thou sayest.
3Pilato akamwuliza Yesu, "Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?" Yesu akamjibu, "Wewe umesema."
4And Pilate said to the chief priests and the crowds, I find no guilt in this man.
4Pilato akawaambia makuhani wakuu na umati wa watu, "Sioni kosa lolote katika mtu huyu."
5But they insisted, saying, He stirs up the people, teaching throughout all Judaea, beginning from Galilee even on to here.
5Lakini wao wakasisitiza wakisema: "Anawachochea watu kwa mafundisho yake katika nchi yote ya Yudea; alianza Galilaya, na sasa yuko hapa."
6But Pilate, having heard Galilee [named], demanded if the man were a Galilaean;
6Pilato aliposikia hayo, akauliza, "Je, mtu huyu ni mwenyeji wa Galilaya?"
7and having learned that he was of Herod's jurisdiction, remitted him to Herod, who himself also was at Jerusalem in those days.
7Alipojua kwamba Yesu alikuwa chini ya utawala wa Herode, akampeleka kwa Herode, ambaye wakati huo alikuwa Yerusalemu.
8And when Herod saw Jesus he greatly rejoiced, for he had been a long while desirous of seeing him, because of hearing many things concerning him, and he hoped to see some sign done by him;
8Herode alifurahi sana alipomwona Yesu. Alikuwa amekwisha sikia habari zake, na hivyo alikuwa anatazamia kwa muda mrefu kumwona kwa macho yake mwenyewe. Zaidi ya hayo, alikuwa anatumaini kumwona Yesu akitenda mwujiza.
9and he questioned him in many words, but *he* answered him nothing.
9Basi, akamwuliza maswali mengi kwa muda mrefu, lakini Yesu hakumjibu neno.
10And the chief priests and the scribes stood and accused him violently.
10Makuhani wakuu na walimu wa Sheria wakajitokeza mbele, wakatoa mashtaka yao kwa nguvu sana.
11And Herod with his troops having set him at nought and mocked him, having put a splendid robe upon him, sent him back to Pilate.
11Basi, herode pamoja na maaskari wake, wakamwaibisha Yesu na kumfanyia mzaha; kisha wakamvika vazi la kifalme, wakamrudisha kwa Pilato.
12And Pilate and Herod became friends with one another the same day, for they had been at enmity before between themselves.
12Herode na Pilato, ambao hapo awali walikuwa maadui, tangu siku hiyo wakawa marafiki.
13And Pilate, having called together the chief priests and the rulers and the people,
13Basi, Pilato akaitisha mkutano wa makuhani wakuu, viongozi na watu,
14said to them, Ye have brought to me this man as turning away the people [to rebellion], and behold, I, having examined him before you, have found nothing criminal in this man as to the things of which ye accuse him;
14akawaambia, "Mmemleta mtu huyu kwangu mkisema kwamba alikuwa anawapotosha watu. Sasa sikilizeni! Baada ya kuchunguza jambo hilo mbele yenu, sikumpata na kosa lolote kuhusu mashtaka yenu juu yake.
15nor Herod either, for I remitted you to him, and behold, nothing worthy of death is done by him.
15Wala si mimi tu, bali hata Herode hakuona kosa lolote, kwa maana amemrudisha kwangu. Ni dhahiri kwamba mtu huyu hakufanya chochote kinachostahili adhabu ya kifo.
16Having chastised him therefore, I will release him.
16Hivyo, nitaamuru apigwe viboko, halafu nitamwachilia."
17( Now he was obliged to release one for them at the feast.)
17Kila sikukuu ya Pasaka, ilimlazimu Pilato kuwafungulia mfungwa mmoja.
18But they cried out in a mass saying, Away with this [man] and release Barabbas to us;
18Lakini wote wakapiga kelele pamoja: "Mwondoe huyo, utufungulie Baraba!"
19who was one who, for a certain tumult which had taken place in the city, and [for] murder, had been cast into prison.
19(Baraba alikuwa ametiwa ndani kwa kusababisha uasi katika mji na pia kwa sababu ya kuua.)
20Pilate therefore, desirous to release Jesus, again addressed [them].
20Pilato alitaka kumwachilia Yesu, hivyo akasema nao tena;
21But they cried out in reply saying, Crucify, crucify him.
21lakini wao wakapiga kelele: "Msulubishe, msulubishe!"
22And he said the third time to them, What evil then has this [man] done? I have found no cause of death in him: I will chastise him therefore and release him.
22Pilato akawaambia mara ya tatu, "Amefanya kosa gani? Sioni kosa lolote kwake linalomstahili auawe; kwa hiyo nitampiga viboko, halafu nimwachilie."
23But they were urgent with loud voices, begging that he might be crucified. And their voices [and those of the chief priests] prevailed.
23Lakini wao wakazidi kupiga kelele kwa nguvu sana, kwamba Yesu ni lazima asulubiwe. Mwishowe, sauti zao zikashinda.
24And Pilate adjudged that what they begged should take place.
24Basi, Pilato akaamua kwamba matakwa yao yatimizwe.
25And he released him who, for tumult and murder, had been cast into prison, whom they begged for, and Jesus he delivered up to their will.
25Akamfungua kutoka gerezani yule waliyemtaka, ambaye alikuwa ametiwa gerezani kwa sababu ya uasi na kuua; akamtoa Yesu kwao, wamfanyie walivyotaka.
26And as they led him away, they laid hold on a certain Simon, a Cyrenian, coming from the field, and put the cross upon him to bear it behind Jesus.
26Walipokuwa wakimpeleka, walikutana na mtu mmoja, aitwaye Simoni wa Kurene, aliyekuwa anatoka shambani. Basi, walimkamata, wakamtwika ule msalaba auchukue nyuma ya Yesu.
27And a great multitude of the people, and of women who wailed and lamented him, followed him.
27Watu, umati kwa umati, walimfuata; miongoni mwao wakiwemo wanawake waliokuwa wanaomboleza na kumlilia.
28And Jesus turning round to them said, Daughters of Jerusalem, do not weep over me, but weep over yourselves and over your children;
28Yesu akawageukia, akasema, "Enyi kina mama wa Yerusalemu! Msinililie mimi, ila lieni kwa ajili yenu wenyewe na kwa ajili ya watoto wenu.
29for behold, days are coming in which they will say, Blessed [are] the barren, and wombs that have not borne, and breasts that have not given suck.
29Maana, hakika siku zitakuja ambapo watasema: Heri yao wale walio tasa, ambao hawakupata kuzaa wala kunyonyesha watoto!
30Then shall they begin to say to the mountains, Fall upon us; and to the hills, Cover us:
30Wakati huo, ndipo watu wataanza kuiambia milima: Tuangukieni! na vilima, Tufunikeni!
31for if these things are done in the green tree, what shall take place in the dry?
31Kwa maana, kama watu wanautendea mti mbichi namna hiyo, itakuwaje kwa mti mkavu?"
32Now two others also, malefactors, were led with him to be put to death.
32Waliwachukua pia watu wengine wawili, wahalifu, wauawe pamoja naye.
33And when they came to the place which is called Skull, there they crucified him, and the malefactors, one on the right hand, the other on the left.
33Walipofika mahali paitwapo, "Fuvu la Kichwa," ndipo wakamsulubisha Yesu pamoja na wale wahalifu wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wake wa kushoto.
34And Jesus said, Father, forgive them, for they know not what they do. And, parting out his garments, they cast lots.
34Yesu akasema, "Baba, uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya." Kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
35And the people stood beholding, and the rulers also [with them] sneered, saying, He has saved others; let him save himself if this is the Christ, the chosen one of God.
35Watu wakawa wamesimama pale wakitazama. Nao viongozi wakamdhihaki wakisema: "Amewaokoa wengine; sasa na ajiokoe mwenyewe, kama yeye ndiye Kristo, mteule wa Mungu!"
36And the soldiers also made game of him, coming up offering him vinegar,
36Askari nao walimdhihaki pia; walimwendea wakampa siki
37and saying, If *thou* be the king of the Jews, save thyself.
37wakisema: "Kama kweli wewe ni Mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe."
38And there was also an inscription [written] over him in Greek, and Roman, and Hebrew letters: This is the King of the Jews.
38Vilevile maandishi haya yalikuwa yameandikwa na kuwekwa juu yake: "Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi."
39Now one of the malefactors who had been hanged spoke insultingly to him, saying, Art not thou the Christ? save thyself and us.
39Mmoja wa wale wahalifu waliotundikwa msalabani, alimtukana akisema: "Je, si kweli kwamba wewe ndiwe Kristo? Basi, jiokoe mwenyewe, utuokoe na sisi pia."
40But the other answering rebuked him, saying, Dost *thou* too not fear God, thou that art under the same judgment?
40Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake akisema: "Wewe humwogopi Mungu hata kidogo? Wewe umepata adhabu hiyohiyo.
41and *we* indeed justly, for we receive the just recompense of what we have done; but this [man] has done nothing amiss.
41Wewe na mimi tunastahili, maana haya ni malipo ya yale tuliyotenda. Lakini mtu huyu hakufanya chochote kibaya."
42And he said to Jesus, Remember me, [Lord,] when thou comest in thy kingdom.
42Kisha akasema, "Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako."
43And Jesus said to him, Verily I say to thee, To-day shalt thou be with me in paradise.
43Yesu akamwambia, "Nakwambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi."
44And it was about [the] sixth hour, and there came darkness over the whole land until [the] ninth hour.
44Ilikuwa yapata saa sita mchana; jua likaacha kuangaza, giza likafunika nchi yote mpaka saa tisa,
45And the sun was darkened, and the veil of the temple rent in the midst.
45na pazia lililokuwa limetundikwa Hekaluni likapasuka vipande viwili.
46And Jesus, having cried with a loud voice, said, Father, into thy hands I commit my spirit. And having said this, he expired.
46Yesu akalia kwa sauti kubwa: "Baba, naiweka roho yangu mikononi mwako." Alipokwisha sema hayo, akakata roho.
47Now the centurion, seeing what took place, glorified God, saying, In very deed this man was just.
47Hapo, yule jemadari alipoona yaliyotukia akamsifu Mungu akisema: "Hakika huyu alikuwa mtu mwema."
48And all the crowds who had come together to that sight, having seen the things that took place, returned, beating [their] breasts.
48Watu wale wote waliokuwa wamekusanyika hapo kwa ajili ya tukio hilo, walipoona hayo yaliyotukia, walirudi makwao wakijipiga vifua kwa huzuni.
49And all those who knew him stood afar off, the women also who had followed him from Galilee, beholding these things.
49Marafiki zake wote pamoja na wale wanawake walioandamana naye kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali kutazama tukio hilo.
50And behold, a man named Joseph, who was a councillor, a good man and a just
50Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yosefu, mwenyeji wa kijiji kimoja cha Wayahudi kiitwacho Armathaya. Alikuwa mtu mwema anayeheshimika;
51(this [man] had not assented to their counsel and deed), of Arimathaea, a city of the Jews, who also waited, [himself also,] for the kingdom of God
51Alikuwa akitazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. Ingawa alikuwa mmoja wa Baraza kuu la Wayahudi, hakuwa amekubaliana nao katika kitendo chao.
52-- he having gone to Pilate begged the body of Jesus;
52Basi, yeye alikwenda kwa Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu.
53and having taken it down, wrapped it in fine linen and placed him in a tomb hewn in the rock, where no one had ever been laid.
53Kisha, akaushusha mwili huo kutoka msalabani, akauzungushia sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa kwenye mwamba, ambalo halikuwa limetumika.
54And it was preparation day, and [the] sabbath twilight was coming on.
54Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, na maandalio ya siku ya Sabato yalikuwa yanaanza.
55And women, who had come along with him out of Galilee, having followed, saw the sepulchre and how his body was placed.
55Wale wanawake walioandamana na Yesu kutoka Galilaya walimfuata Yosefu, wakaliona lile kaburi na jinsi mwili wake Yesu ulivyowekwa
56And having returned they prepared aromatic spices and ointments, and remained quiet on the sabbath, according to the commandment.
56Halafu, walirudi nyumbani, wakatayarisha manukato na marashi kuyapaka mwili wa Yesu. Siku ya Sabato walipumzika kama ilivyoamriwa na sheria.