1Jūs patys, broliai, žinote, kad mūsų apsilankymas pas jus nebuvo veltui.
1Ndugu, ninyi wenyewe mnafahamu kwamba ziara yetu kwenu haikuwa bure.
2Prieš tai, kaip patys žinote, nukentėję ir paniekinti Filipuose, buvome drąsūs Dieve ir skelbėme jums Evangeliją esant dideliam pasipriešinimui.
2Mnajua jinsi tulivyodhulumiwa na kutukanwa kule Filipi kabla ya kufika kwenu Thesalonike. Ingawa kulikuwa na upinzani mwingi, Mungu wetu alitujalia uhodari wa kuwahubirieni Habari Njema yake.
3Juk mūsų skelbimas plaukia ne iš klaidos, nei iš netyro nusistatymo, nei iš klastingumo.
3Jambo tunalosisitiza kwenu si jambo linalotegemea uongo au nia mbaya; wala hatupendi kumdanganya mtu yeyote.
4Dievo pripažinti tinkami, kad mums būtų patikėta Evangelija, ją ir skelbiame taip, kad patiktume ne žmonėms, bet Dievui, kuris tiria mūsų širdis.
4Sisi twanena daima kama atakavyo Mungu kwani yeye alituona kwamba tunafaa, akatukabidhi hii Habari Njema. Si nia yetu kuwapendeza watu hata kidogo, bali twataka kumpendeza Mungu ambaye anajua mioyo yetu mpaka ndani.
5Kaip žinote, niekada nepasižymėjome pataikaujančiomis kalbomis ir paslėptu godumu,Dievas yra liudytojas,
5Ninyi mnajua kwamba sisi hatukuja kwenu na maneno matamu ya kubembeleza wala hatukutumia maneno ya kijanja ya kuficha ubinafsi fulani; Mungu ni shahidi!
6niekada neieškojome žmonių garbės, nei tarp jūsų, nei kitur. Būdami Kristaus apaštalai, galėjome būti jums našta,
6Hatukutafuta sifa kutoka kwa watu, wala kutoka kwenu, wala kutoka kwa mtu yeyote,
7vis dėlto pas jus buvome švelnūs, tarsi maitinanti motina, globojanti savo kūdikius.
7ingawa sisi tukiwa mitume wa Kristo, tungeweza kudai mambo fulani kwenu. Lakini sisi tulikuwa Wapole kati yenu kama alivyo mama kwa watoto wake.
8Taip jus mylėdami, troškome pasidalyti su jumis ne tik Dievo Evangelija, bet ir savo gyvybe, nes tapote mums brangūs.
8Tuliwapenda ninyi sana hata tukawa tayari kuwashirikisha si tu Habari Njema ya Mungu, bali pia na maisha yetu. Ndivyo mlivyokuwa wapenzi wetu!
9Jūs, broliai, atsimenate mūsų triūsą ir pastangas: dirbdami per dienas ir naktis, kad neapsunkintume nė vieno iš jūsų, skelbėme jums Dievo Evangeliją.
9Ndugu, mnakumbuka jinsi tulivyofanya kazi na kutaabika. Tulipowaleteeni Habari Njema ya Mungu tulifanya kazi mchana na usiku kusudi tusiwe mzigo kwa mtu yeyote miongoni mwenu.
10Ir jūs, ir Dievas gali paliudyti, kaip šventai, teisingai ir nepriekaištingai elgėmės su jumis, įtikėjusiais.
10Ninyi mnaweza kushuhudia, na Mungu pia ni shahidi, jinsi mwenendo wetu kati yenu ninyi mnaoamini ulivyokuwa mzuri, mwadilifu na usio na lawama.
11Jūs žinote, kaip kiekvieną iš jūsų raginome, kalbinome, maldavome, tarsi tėvas savo vaikus,
11Mnajua kwamba sisi tulimtendea kila mmoja wenu kama vile baba anavyowatendea watoto wake mwenyewe.
12kad elgtumėtės kaip dera prieš Dievą, kuris jus šaukia į savo karalystę ir šlovę.
12Tuliwapeni moyo, tuliwafarijini na kuwahimiza ili mpate kuishi maisha yampendezayo Mungu ambaye aliwaiteni mshiriki Utawala na utukufu wake.
13Todėl ir mes be paliovos dėkojame Dievui, kad, priėmę Dievo žodį, kurį girdėjote iš mūsų, priėmėte jį ne kaip žmonių žodį, bet, kas jis iš tikro yra,kaip Dievo žodį, kuris ir veikia jumyse, tikinčiuosiuose.
13Tena tunayo sababu nyingine ya kumshukuru Mungu: tulipowaleteeni ujumbe wa Mungu, ninyi mliusikia mkaupokea, si kama vile ujumbe wa binadamu, bali kama ujumbe wa Mungu, na kweli ndivyo ulivyo. Maana Mungu anafanya kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.
14Jūs, broliai, tapote sekėjais Dievo bažnyčių Kristuje Jėzuje, kurios yra Judėjoje. Jūs tą patį iškentėjote nuo savo tautiečių, kaip ir jos nuo žydų,
14Ndugu, ninyi mmepatwa na mambo yaleyale yaliyoyapata makanisa ya Mungu kule Yudea, mambo yaliyowapata watu walio wake Kristo Yesu. Ninyi mlidhulumiwa na wananchi wenzenu kama vile wao walivyodhulumiwa na wenzao Wayahudi,
15kurie nužudė Viešpatį Jėzų ir savo pranašus ir persekiojo mus. Jie nepatinka Dievui ir yra priešiški visiems žmonėms,
15ambao walimuua Bwana Yesu na manabii, wakatutesa na sisi pia. Watu hao wanamchukiza Mungu, tena ni adui za kila mtu!
16nes draudžia mums skelbti Evangeliją pagonims, kad šie būtų išgelbėti. Taip jie nuolat pildo savo nuodėmių saiką, ir jiems artinasi galutinė Dievo rūstybė.
16Hata walijaribu kutuzuia kuwahubiria watu wa mataifa mengine ujumbe utakaowaletea wokovu. Ndivyo walivyokamilisha orodha ya dhambi zote walizotenda siku zote. Lakini sasa hasira ya Mungu imewaangukia.
17O mes, broliai, kuriam laikui atskirti nuo jūsų,žinoma, tik kūnu, ne širdimi,be galo pasiilgę, labai troškome išvysti jūsų veidus.
17Ndugu, kuachana kwetu nanyi kulikuwa kwa muda tu, tena kuachana huko kulikuwa kwa mwili tu na si kwa roho. Kitambo kifupi baadaye, tulishikwa na hamu kubwa ya kuwaoneni tena!
18Todėl ruošėmės atvykti pas jus,bent jau aš, Paulius, ruošiausi kartą ir kitą,tačiau mums sutrukdė šėtonas.
18Kwa hiyo tuliamua kuwatembeleeni tena. Nami, Paulo, nilijaribu kuja kwenu zaidi ya mara moja, lakini Shetani alituzuia.
19Kas gi yra mūsų viltis, džiaugsmas ir pasigyrimo vainikas? Argi ne jūs prieš mūsų Viešpatį Jėzų Kristų Jo atėjimo metu?
19Je, tutakaposimama mbele ya Bwana Yesu wakati atakapokuja, fahari ya ushindi wetu itakuwa nini? Itakuwa ni ninyi wenyewe; ninyi ndio tumaini letu na furaha yetu.
20Taip, jūs esate mūsų šlovė ir džiaugsmas!
20Naam, ninyi ni utukufu wetu na furaha yetu!