1Paulius, Dievo valia Kristaus Jėzaus apaštalas, ir brolis TimotiejusDievo bažnyčiai Korinte ir visiems šventiesiems, gyvenantiems visoje Achajoje.
1Mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu Timotheo, tunawaandikia ninyi mlio kanisa la Mungu huko Korintho, na watu wote wa Mungu kila mahali katika Akaya.
2Malonė jums ir ramybė nuo Dievo, mūsų Tėvo, ir Viešpaties Jėzaus Kristaus!
2Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
3Tebūna palaimintas Dievas, mūsų Viešpaties Jėzaus Kristaus Tėvas, gailestingumo Tėvas ir visokios paguodos Dievas,
3Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba mwenye huruma na Mungu mwenye kuleta faraja yote.
4kuris guodžia mus kiekviename mūsų sielvarte, kad mes galėtume paguosti bet kokio sielvarto ištiktuosius ta paguoda, kuria patys Dievo guodžiami.
4Yeye hutufariji sisi katika taabu zetu zote, ili nasi tupate kuwafariji wengine katika kila taabu kwa faraja hiyohiyo tunayopokea kutoka kwa Mungu.
5Kaip gausėja mumyse Kristaus kentėjimai, taip gausėja per Kristų ir mūsų paguoda.
5Naam, kadiri mateso ya Kristo yanavyozidi ndani yetu, ni kadiri hiyohiyo tunazidi kufarijiwa naye.
6Jeigu patiriam sielvartą, tai jūsų paguodai ir išgelbėjimui, kuris padeda iškęsti tokius pačius kentėjimus, kokius mes kenčiame; o jeigu mes guodžiami, tai jūsų nusiraminimui ir išgelbėjimui.
6Ikiwa tunapata taabu, basi ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu. Tukifarijika, ni kwa ajili ya kuwafariji ninyi na kuwaunga mkono mpate nguvu ya kustahimili mateso yaleyale tunayoteseka sisi.
7Ir mūsų viltis jumis tvirta, nes žinome, kad, būdami kentėjimų dalininkai, būsite ir paguodos dalininkai.
7Tena, matumaini tuliyo nayo kwa ajili yenu ni imara; tunajua kwamba mkishiriki mateso yetu, mtashiriki pia faraja yetu.
8Mes nenorime, broliai, palikti jus nežinioje apie Azijoje mus ištikusią negandą. Mes buvome prislėgti daugiau nei mūsų jėgos leidžiataip, kad nebesitikėjome išliksią gyvi.
8Ndugu, tunataka kuwajulisheni taabu zilizotupata kule Asia; taabu hizo zilitulemea kupita kiasi, hata tukakata matumaini yote ya kuendelea kuishi.
9Bet patys savyje patyrėme mirties nuosprendį, kad pasitikėtume ne savimi, o Dievu, kuris prikelia mirusius.
9Naam, tulikuwa kama watu waliohukumiwa kuuawa, ili tufundishwe kumtegemea Mungu mwenye kuwafufua wafu, badala ya kutegemea nguvu zetu sisi wenyewe.
10Jis išgelbėjo mus iš mirties nasrų ir tebegelbsti. Juo mes pasitikime, kad Jis mus gelbės toliau,
10Yeye alituokoa katika hatari kubwa ya kifo, na anaendelea kutuokoa; sisi tumemwekea tumaini letu kwamba atatuokoa tena,
11jums padedant malda už mus, kad daugelis dėl mūsų dėkotų už dovaną, per daugelį suteiktą mums.
11ninyi mkiwa mnatuunga mkono kwa kutuombea. Hivyo neema tutakazokuwa tumepata kutokana na maombi ya watu wengi hivyo, ziwe sababu ya watu wengi zaidi kumshukuru Mungu kwa ajili yetu.
12Nes mūsų pasigyrimas yra toks: liudija mūsų sąžinė, kad pasaulyje, o ypač pas jus, mes elgėmės paprastai ir su dievišku nuoširdumu,ne kūniška išmintimi, bet Dievo malone.
12Sisi tunajivunia kitu kimoja: dhamiri yetu inatuhakikishia kwamba tumeishi ulimwenguni hapa, na hasa kati yenu, kwa unyenyekevu na unyofu tuliojaliwa na Mungu; hatukuongozwa na hekima ya kibinadamu bali neema ya Mungu.
13Nerašome jums nieko kito, kaip tik tai, ką jūs skaitote ir suprantate. Tikiuosi, kad ir iki galo suprasite,
13Tunawaandikia ninyi mambo mnayoweza kuyasoma na kuyaelewa. Ninatumaini kwamba mtaelewa vizuri kabisa,
14kaip iš dalies jau mus supratote, kad mes esame jūsų pasigyrimas, kaip ir jūs mūsųViešpaties Jėzaus dieną.
14maana mpaka sasa mmenielewa kiasi fulani tu. Tunajua kwamba katika ile Siku ya Bwana Yesu mtaweza kutuonea sisi fahari kama nasi tunavyowaonea ninyi fahari.
15Tokio pasitikėjimo kupinas, aš norėjau anksčiau pas jus atvykti, kad antrąkart gautumėt malonę,
15Nikiwa na matumaini hayo, nilikusudia kuja kwenu hapo awali ili mpate baraka maradufu.
16ir pro jus keliauti į Makedoniją, o iš Makedonijos vėl grįžti pas jus, kad jūs mane išlydėtumėte į Judėją.
16Nilikusudia kupita kwenu nikiwa safarini kwenda Makedonia, na wakati wa kurudi pia, ili nipate msaada wenu kwa safari yangu kwenda Yudea.
17Ar taip manydamas, elgiausi lengvabūdiškai? O gal mano sumanymai buvo pagal kūną, kad mano “taip, taip” yra ir “ne, ne”?
17Je, mnadhani nilipopanga hivyo nimekuwa kama mtu asiye na msimamo? Je, mnadhani kwamba ninafanya uamuzi wangu kwa fikira za kibinadamu na kwamba nasema "Ndiyo" na "Siyo" papo hapo?
18Bet kaip Dievas ištikimas, mūsų žodis jums nebuvo “taip” ir “ne”.
18Mungu ni ukweli mtupu; basi, kile tulichowaambia ninyi si jambo la "Ndiyo" na "Siyo".
19Nes Dievo Sūnus, Jėzus Kristus, kurį jums paskelbėme aš, Silvanas ir Timotiejus, nebuvo “taip” ir “ne”, bet Jame buvo “taip”.
19Maana Kristo Yesu, Mwana wa Mungu, ambaye mimi, Silwano na Timotheo, tulimhubiri kwenu, hakuwa mtu wa "Ndiyo" na "Siyo"; bali yeye daima ni "Ndiyo" ya Mungu.
20Nes visi Dievo pažadai Jame yra “taip” ir Jame “amen” Dievo šlovei per mus.
20Maana ndani yake ahadi zote za Mungu zimekuwa "Ndiyo". Kwa sababu hiyo, "Amina" yetu husemwa kwa njia ya Kristo kwa ajili ya kumtukuza Mungu.
21Tas, kuris sutvirtina mus su jumis Kristuje ir mus patepė, yra Dievas,
21Mungu mwenyewe ndiye mwenye kutuimarisha sisi na ninyi pia katika Kristo, na ndiye anayetuweka wakfu;
22kuris ir užantspaudavo mus ir davė kaip užstatą Dvasią į mūsų širdis.
22ndiye aliyetutia mhuri wa kuwa mali yake yeye na kutujalia Roho mioyoni mwetu kama dhamana ya mambo yote ambayo ametuwekea.
23Šaukiuosi Dievą liudytoju savo sielai, kad jūsų gailėdamas aš neatvykau į Korintą.
23Mungu ndiye shahidi wangu--yeye anajua moyo wangu! Mimi sikuja tena Korintho, kwa sababu tu ya kuwahurumieni.
24Mes juk neviešpataujame jūsų tikėjimui, bet esame jūsų džiaugsmo talkininkai, nes tikėjimu jūs stovite tvirtai.
24Hatutaki kutumia mabavu juu ya imani yenu; ninyi mko imara katika imani yenu. Wajibu wetu ni kufanya kazi pamoja kwa ajili ya furaha yenu.